Tuesday, September 30, 2014

Hizi Ni Sababu Kuu Tano Kwanini Lowassa Anafaa Kuwa Rais 2015



Hizi Ni Sababu Kuu Tano Kwanini Lowassa Anafaa Kuwa Rais 2015
Maisha ya watanzania yamekua magumu mno,sasa sukari ipo juu ikiwa ardhi na mabonde kama ruvu mtibwa na kageara tunayo, umeme usio wa uhakika wakati gesi ya mtwara na RUBADA, madawa hakuna hospitalini, viongozi wanatuziba masikio kwa vizungumkuti vya ESCROW huku madawati hakuna shuleni, vitendo vya kihalifu vimejaa kila kona watu wakisaka ridhiki kwa nguvu, tumaini la katiba mpya ni kizunguzungu kiasi kutuacha wakiwa Zaidi sisi masikini wakitanzania, huku tukijengewa chuki na serikali na watawala kwa upenyo wakushuka uzalendo na kiasi cha kusema watu kuikimbia nchi kwa vijana ni kawaida kutafuta maisha ughaibuni na kusema hii nchi sasa si ile ya NYERERE bali ni ya watawala makatili mno. Lakini kwa muktadha ule ule wa kidemokrasia ambao hata rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya tatu Mh. Benjamin Mkapa aliyasema pale alipo chagiza kabla kuteuliwa Dk Jakaya Kikwete ndani ya CCM kuwa achaguliwe mgombea ambaye vijana na wapiga kura wengi wanamtaka kitu ambacho kilipelekea Dk. Kikwete kushinda kwa kishindo ndani ya chama na hata katika uchaguzi mkuu 2005. Sasa zifuatazo ni sababu ambazo Lowassa atapitishwa kugombea URAIS kwani wanachama na watanzania wanamuhitaji.


1.MRITHI SAHIHI WA MWL. NYERERE KATIKA VITA DHIDI YA UJINGA

Edward Lowassa ni mwana siasa Pekee ambae ndani ya CCM,anaefaham Vission ya Mwalimu Nyerere 1961 Mwalimu alitangaza maadui watatu (1)Ujinga (2)Maradhi (3) Umasikini. Mwalimu katika miaka yake 24 alisimamia swala moja Elimu ya Kujigetemea na baada ya kuondoka mfumo huu uliharibika,Ili kupambana na Adui hao Mwalimu alianzisha Vijiji vya Ujamaa,msingi hapa ili kuongea Uzalishaji,huduma ya afya na Shule, akajenga shule za msingi katika kila kijiji. Mwaka 2005 Edward Lowassa aliamua kufufua upya utekelezaji wa Dira ya Mwalimu nayo ni kuwekeza kwenye Elimu na Kupambana na maadui 3.Alisimamia Ujenzi wa Miundo Mbinu ya Elimu kila kata( sekondari),Kupanua elimu ya Chuo Kikuu, Kusukuma Ujenzi wa vyuo vya kada ya kati (Veta) ili kujenga Kada la kati ya wataalam wa Ufundi mbali mbali, Kupanua Vyuo vya Ualimu ili kuziba pengo la upungufu wa waalim,mambo haya hayana tofauti mapambano alianzisha Mwl Nyerere baada ya uhuru kupambana na maadui watatu. Elimu imekua Agenda kuu ya Edward lowassa,Anaamini katika hilo Jambo kuwa msingi wa kupambana na Umasikini,Elimu itasaidia Uzalishaji,Elimu Itapambana na Maradhi,Elimu Itaondoa Ujinga miongoni mwa Jamii yetu, hii ni sababu pekee itakayo ifanya CCM kumpitisha kurudisha taswira ya chama.


2. MAAMUZI MAGUMU NA MAKINI KATIKA UONGOZI

Kwa kipindi kirefu sasa ndani ya nchi yetu tuna tatizo la maamuzi katika utekelezaji wa sera za serikali, viongozi wamekuwa wazito mno kutekeleza makubaliano ya vikao vyao wakiogopana au hata rushwa kutawala miongoni mwao hivyo kushindwa kutekeleza maamuzi hayo. Edward Lowassa ni kiongozi ambaye kwa kipindi chake alicho kuwa madarakani ameonyesha kuwa si kigeugeu kwa maana ya kwamba mara zote ambazo baraza la mawaziri katika vikao vyake vya ndani walipo fika makubaliano yeye alitekeleza, Utekelezaji wa ujenzi wa chuo kikuu Dodoma. Taarifa za ndani za viongozi zilionyesha ugumu mno wa utekelezaji wa sera hii ya chama, Lowassa ilifikia hatua kuwaeleza viongozi mbalimbali waandamizi katika ngazi za maamuzi na utekelezaji kama yeyote anaona ujenzi wa chuo kile hauwezekani aandike barua ya kujiuzulu na akabidhi kwake ampatie Rais Dk.Jakaya Kikwete, kitu ambacho kiliongeza ujasiri wa utekelezaji wa sera na sasa tunaona watoto wa masikini wakipata elimu. Alivunja mkataba wa city water, mkataba ambao ulifanya serikali kushtakiwa lakini na hata kuleta nafuu katika upatikanaji wa majia ndani ya jiji la dar es salaam pia bila kusahau alivunja mkataba wa kimataifa katika usambazaji wa maji kanda ya ziwa kitu kilicho mfanya mpaka aogepeke na jumuia za kimataifa akiwa anatetea haki ya Mtazania kwa hakika ni mzalendo na mtu pekee ndani ya CCM hii ya DK. Jakaya na Kinana anaefaa kuipeleka dira ya taifa mbele.

3. MPAMBANAJI ALIAZIMIA KUFUTA UMASIKINI

Lowassa ni Mwana siasa Pekee ndani ya CCM ambae Anaamini UMASIKINI si sifaa bora kwa Mtanzania kujisifia,Umasikini si Sifa ya Kiongozi,Umasikini unaendana na udhalilishaji na Ujinga na Maradhi,ni mwana Siasa pekee ambae hasifiii umasikini kwani ni vita katika vita kuu za taifa hili tangu tunapata uhuru. Hii imekuwa hulka ya viongozi kadhaa hasa wabunge wetu hutuhadaa wakisema tuwape ridhaa ya kutuongoza kwa sababu wao ni masikini wenzetu, siasa sasa ya leo na kimataifa imebadilika mno tukiangalia mataifa makubwa hata madogo , viongozi ni wale wenye majibu sahihi katika kuufuta umasikini na si kujisifia kuwa wewe ni masikini tukupe ridhaa tena ridhaa ambayo utahakikisha kujinufaisha wewe na famia yako kwanza, na CCM sasa inataka kujenga uchumi imara uchumi ambao utafuta umasikini kwa kumpa Mtanzania Elimu, kuimarisha miundombinu na kufungua biashara tujifunze haya toka Kenya waungwana.Pia ni miongoni mwa sababu zinazo wavutia wana CCM kumpa ridhaa ya kupeperusha bendera.

4.ANAPENDWA NA WATANZANIA WOTE NA WANAMUHITAJI

Ni mtu ambaye ana mvuto mkubwa kwa watanzania na ana sifa ya kuwa muadilifu, mtendaji mzuri, mbunifu, huheshimu mawazo ya wengine, anaijua Tanzania, Mfuatiliaji wa kazi, anatabia ya kuwapa watu matumaini Mpambanaji (fighter) na anaheshimika kikanda na kimataifa. Ni Mtanzania pekee anayependwa na kukubalika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndani na nje ya chama chake. Ni mtu ambaye ana Aura ya aina yake na huleta matumaini unapokaa naye na kusikiliza.Ni kweli kabisa..Edward Lowassa (is the chosen one) kaatika uhai wa siasa ya chama chochote inatakiwa kuwa na gombea anaye uzika, anayekubalika na ambaye ni tumaini la mahitaji wananchi husika, Lowassa amekidhi vigezo vyote na hakika anafaa ndani ya CCM na ndio chaguo sahihi kama chama kinahitaji uhai wa muda mrefu.

5.KIONGOZI ALIYEPITIA MENGI NA ANAYEIJUA NCHI.

Lowassa ni kiongozi alie pitia mengi kama rais wa awamu ya pili alhajj Ali Hassan Mwinyi kufikia hatua ya kujiuzulu na kuwajibika kama kiongozi ambaye anjua fika maadili ya kiongozi wa umma, Lowassa amengia katika mfumo wa chama na serikali tangu mwaka 1977 ambapo imepita miaka Zaidi ya 30 akipambana na shida na mahitaji ya watanzania, mwenyekujua nini Watanzania wanahitaji, mtu ambaye amepitia mengi na kuwa na ufahamu wa kutosha wa serikali na chama chake kiasi cha kufanya kuwa kiongozi pekee kwa sasa anayekijua chama na serikali. Chama cha Mapinduzi kimekosa mtu mwenye sifa hizi mtu ambaye amepitia mikiki mikiki ya kina katika kuwatetea wananchi, kiongozi ambaye amepambana mpaka na mahafidhina ndani ya chama na kiongozi ambae si rahisi kumpelekesha, kiongozi huyu ameweza kuwa adui mkubwa wa mahafidhina kwa sababu hana si ya woga dhidi yao, hawafumbii macho na naweza sema huyu ni kama TAKUKURU kwa mahafidhina sababu hafumbii macho machafu.

MWISHO.
Watanzania tunahitaji kiongozi ambae atakuwa mrithi sahihi wa serikali ya awamu ya tatu, mtu ambae atatuongoza katika kukabiliana na mahitaji yetu yaani nini watu wa namanyere, uvinza nantumbo na Tanzania kwa ujumla nini wanataka, Mtu ambaye atakuwa msikivu na mpambanaji wa mahitaji yetu , nashauri wote kwa pamoja tuwajadili watu wanaoweza kuiongoza nchi yetu bila kejeli, matusi au woga na aina yeyote ya kufumbia macho machafu , kuukuza uzalendo ni pamoja na kuukana woga wa kivuli chako. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

RAIS KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA MWENGE-TEGETA KESHO



RAIS KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA MWENGE-TEGETA KESHO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika tarehe 1 Oktoba 2014.

Ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.

Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Taarifa hii imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini(GCU)
Wizara ya Ujenzi


PROGRAMU MPYA YA KUJIFUNZA SOMO LA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MIKONONI YAZINDULIWA JIJINI DAR LEO





PROGRAMU MPYA YA KUJIFUNZA SOMO LA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MIKONONI YAZINDULIWA JIJINI DAR LEO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari kuhusiana na uzinduzi wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari katika ukumbi wa COSTECH,Sayansi Kijitonyama,jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu ya mikononi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo (wa tatu shoto) akioneshwa na mmoja wa wataalamuwa programu hiyo mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu ya mikononi,iliyozinduliwa leo inavyoweza kufanya kazi katika simu za mikononi.
 Mmoja wa Wataalamu wa mradi huo wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi,kutoka Nokia Mobile Mathematics,Bi.Riita Vanska akifafanua jambo kwa wanahabari na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa COSTECH,Sayansi Kijitonyama,jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  COSTECH,Dkt.Hassan Mshinda ambao pia ni sehemu ya mafanikio ya programu hiyo,akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi. 
  Baadhi ya wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.


Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano waanza jijini dar




Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano waanza jijini dar
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tekinologia ya Huawei Tanzania, Vincent Wen(kushoto) akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano ulioanza jana katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa HUAWEI.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano wakifatilia kwa makini mkutano huo ulioanza jana katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa HUAWEI.


ONESHO LA S!TE KUFUNGULIWA KESHO JUMATANO MLIMANI CITY,JIJINI DAR



ONESHO LA S!TE KUFUNGULIWA KESHO JUMATANO MLIMANI CITY,JIJINI DAR
ONESHO la kimataifa la utalii 'Swahili International Tourism Expo' (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa rasmi leo (kesho Jumatano) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na litamalizika Jumamosi.

Tayari maandalizi yote kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu wa taifa hili.

Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.

Wadhamini wengine ni pamoja na Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern Sun,NewAfrica, Hyatt Regency,Protea, Serena hotel, Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu.

Pamoja na washiriki wengine onesho hilo linatarajiwa kushirikisha wafanya biashara wakubwa na watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani pamoja na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.

Wakati Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.

Usafiri wa ardhini utadhaminiwa na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari, huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki (Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.

Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka Kenya, ambavyo wanatangaza onesho hili kupitia majarida yao.

Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano. Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania. 'Swahili International Tourism Expo' litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwepo wa onyesho la kimataifa la utalii 'Swahili International Tourism Expo' (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),litakalofunguliwa rasmi kesho Jumatano katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Devota Mdachi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu onyesho hilo la kimataifa la utalii 'Swahili International Tourism Expo' (SITE) litakalofunguliwa rasmi kesho Jumatano katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.


Kongamano la Akina mama




(no subject)



VODACOM NA BENKI YA TWIGA BANCORP ZAWALETEA HUDUMA YA "M-PESA SUPER AGENCY"



VODACOM NA BENKI YA TWIGA BANCORP ZAWALETEA HUDUMA YA "M-PESA SUPER AGENCY"
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Twiga Bancorp Prof.Amon Mbelle(wapili toka kulia) akipongezana na Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Herieth Koka,mara baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya "M-PESA SUPER AGENCY" Itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kupata huduma za kifedha kiurahisi kupitia simu za mkononi.Kushoto ni Kaimu Ofisa mkuu wa Benki hiyo Willace Msemo na Meneja uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kulia).
Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Herieth Koka(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na huduma ya "M-PESA SUPER AGENCY" Itakayowawezesha wateja wa benki ya Twiga Bancorp kupata huduma za kifedha kiurahisi kupitia simu za mkononi.katikati ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Prof.Amon Mbelle na kushoto ni Meneja uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.


MAAFISA KUTOKA AFRIKA KUSINI WATEMBELEA WIZARA YA NISHATI NA MADINI




MAAFISA KUTOKA AFRIKA KUSINI WATEMBELEA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Na Veronica Simba – Dar es Salaam

Maafisa Wakuu 35 kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini (South African National Defence College – NDC), wametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Septemba 30, 2014 kwa lengo la kujifunza kuhusu Sera ya Tanzania kuhusu vyanzo vya nishati nchini hususan mafuta, gesi, makaa ya mawe na uvumbuzi wa madini mengine na changamoto zake.

Maafisa hao waliongozwa na Mkuu wa Chuo Brigedia Jenerali G.M. Yekelo pamoja na Maafisa kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao ndiyo wenyeji wa wageni hao hapa nchini.

Wakiwa Wizarani, Maafisa hao walipokelewa na Viongozi na Maafisa Waandamizi wa Idara za Nishati na Madini na kupewa maelezo mafupi kuhusu vyanzo vya nishati nchini pamoja na rasilimali za madini.

Ujumbe huo upo nchini kuanzia Septemba 27 kwa ziara ya mafunzo na wanatarajia kurejea Afrika Kusini Oktoba 2, 2014.
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini (South African National Defense College – NDC), Brigedia Jenerali G.M. Yekelo akiuliza swali kuhusu rasilimali ya gesi asili kwa Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza (wa kwanza kushoto).
Mmoja wa Maafisa kutoka Chuo cha NDC akitoa salamu za shukrani kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya wenzake.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza (kushoto), akipeana mkono na mmoja wa Maafisa kutoka NDC, baada ya kukabidhiwa zawadi kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa maelezo kuhusu Kitabu chenye kueleza rasilimali za madini yaliyopo Tanzania kabla ya kukikabidhi kama zawadi kwa Ujumbe wa Maafisa wa NDC.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Ujumbe wa Maafisa kutoka NDC waliofika kutembelea Wizarani.


Programu ya kujitolea kwa Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu yamalizika leo


Programu ya kujitolea kwa Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu yamalizika leo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante OleGabriel akiongea na wahitimu wa programu ya kujitolea wa Vyuo Vikuu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa VSO International Tanzania Bw. Jean Van Wetter.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habar i Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante OleGabriel katikati akimpa Cheti Dada Ndidi Tumpe wakati wa kuhitimisha Programu ya kujitolea kwa Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuila ni Mkurugenzi Mkazi wa VSO International Tanzania Bw. Jean Van Wetter.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habar i Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante OleGabriel aleyekaa katikati katikapicha ya Pamoja na wahitimu wa Programu ya kujitolea kwa Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuila ni Mkurugenzi Mkazi wa VSO International Tanzania Bw. Jean Van Wetter.


KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO



KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO
Wahudumu wa Bunge wakibeba masanduku ya kura ili kuyapeleka kwenye chaumba cha kuhesabia kura baada ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kumaliza kazi ya kupiga kura Septemba 30, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka wakiteta bungeni Mjini Dodoma Septemba 30, 2014. Kushoto ni Spika wa Bunge, Anne Makinda.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kingunge Ngombale Mwiru (kulia) wakizungumza na Mama Loyce Samike, Mama mzazi wa Mjumbe wa Bunge hilo, Dkt. Angelina Samike (wapili kushoto) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 30, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Kundi la Orijino Komedy wajiunga na Huduma ya Bima itolewayo na CRDB Microfinance Insurance Brokers


Kundi la Orijino Komedy wajiunga na Huduma ya Bima itolewayo na CRDB Microfinance Insurance Brokers
CRDB Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote ikiwemo bima ya afya, moto, nyumbani na maisha wakishirikiana na kampuni zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania,wamefanikiwa kuwapatia huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao kupitia Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.

CRDB Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma hiyo,kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha jamii.Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na Isaya Mwakilasa 'Wakuvwanga', Mjuni Silvery 'Mpoki', Lucas Mhuvile 'Joti', Alex Chalamila 'McRegan' na Kiongozi wa kundi hilo,Sekioni David na wengine ni Herry pamoja na Jonas.

Huduma hii inawahamasisha wasanii wengine,wanahabari,wanamitindo na watanzania wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini Tanzania,ili waweze kupata huduma nzuri ya na haraka ya bima "ndani ya mikono salama" .
Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha (kushoto) akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company,Sekioni David (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni jijini Dar.
Msanii Lucas Mhuvile 'Joti' akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.
 Msanii Isaya Mwakilasa 'Wakuvwanga' (kulia) akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.(wa pili kulia) ni Meneja Mkuu wa African Life Assurance,Nura Masoud na Kushoto ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance,Majala Manyama.
Meneja Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Nargis Mohamed (kulia) akiwa na Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company,Mjuni Silvery 'Mpoki' katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.


RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA MAREKANI KWENYE MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA



RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI KUTOKA MAREKANI KWENYE MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na IGP Ernest Mangu, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa. PICHA NA IKULU


Jack Mugendi Zoka ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.


Jack Mugendi Zoka ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bw. Jack Mugendi Zoka (pichani) kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.

Bw. Zoka anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Alex Masinda, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Zoka alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.

IMETOLEWA NA
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam,
Septemba 30, 2014


Wakongwe wa siasa nchini Kenya wamtembelea Mh. Lowassa Monduli



Wakongwe wa siasa nchini Kenya wamtembelea Mh. Lowassa Monduli
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh Edward Lowassa (watatu kulia) akiwakaribisha Mawaziri wa zamani wa nchini Kenya William ole Ntimama (tai nyekundu) na John Keen (kushoto) nyumbani kwake Monduli. Wanasiasa hao wakongwe na wenye ushawishi mkubwa katika eneo la Maasai Land nchini Kenya walimtembelea Mh. Lowassa ambaye ni Laigwanan Mkuu wa Wamasai wote Afrika Mashariki, na kujadiliana naye masuala mbalimbali lakini zaidi ni juu ya suala la ardhi ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa jamii ya wamasai.Wazee hao wanatarajiwa kuhudhuria semina maalum katika jimbo la Monduli wiki ijayo kuzungumzia tatizo la ardhi.Semina iliyoandaliwa na Mh. Lowassa itawashirikisha viongozi wote wa wilaya hiyo pamoja na wakuu wa kimila.Akizungumzia suala la ardhi mzee John Keen alisema mtu anayeuza ardhi anauza utajiri na kununua umasikini.



WAKANDARASI UMEME WASIOWAJIBIKA KUNYANG’ANYWA TENDA



WAKANDARASI UMEME WASIOWAJIBIKA KUNYANG'ANYWA TENDA
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Meza Kuu-Katikati), akizungumza na wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zinazohusika kusambaza umeme vijijini kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhusu utekelezaji wa miradi husika.
Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zinazohusika kusambaza umeme vijijini kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na baadhi ya Mameneja wa Tanesco wa Mikoa husika, wakitoa mrejesho kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Meza Kuu – Katikati), kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Miradi husika. Kulia kwa Waziri Muhongo ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga na kushoto kwa Waziri ni Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Umeme, Mhandisi Innocent Luoga.


TANGAZO LA KIFO NA MAZISHI YA DR. HABIBA MUZA RAJABU



TANGAZO LA KIFO NA MAZISHI YA DR. HABIBA MUZA RAJABU
Marehemu Dr. Habiba Muza Rajabu wakati wa uhai wake.

Familia ya Marehemu Mzee Iddi Rajabu Mtoro wa Utemini, Singida inasikitika kutangaza kifo cha Dr. Habiba Muza Rajabu kilichotokea siku ya Jumamosi tarehe 27 Septemba 2014 hapa katika mji wa Trondheim, Norway.

Msiba uko Utemini, Singida na hapa Trondheim, Norway.

Dr. Habiba Muza Rajabu alishawahi kuwa Mhadhiri (Lecturer) katika Idara ya Chemistry, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dr. Habiba Muza Rajabu atazikwa hapa katika mji wa Trondheim, Norway siku ya Jumatano, 1 Octoba 2014 majira ya saa 7 mchana katika eneo la Svanholm Hallen at Moholt. Kumuaga kuanzia saa 7 mchana hadi saa 7:45. Baada ya hapo maziko ya Kiislam yatafanyika hapo hapo.

INALILAHI WAINA ILAHII RAJUUN (HAKIKA SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA)

Imetangazwa na: Rajabu Iddi Rajabu,


TBL YAPATA TUZO YA HESHIMA WIKI YA NENDA KWA USALAMA




TBL YAPATA TUZO YA HESHIMA WIKI YA NENDA KWA USALAMA
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Mbwilo, akimkabidhi Cheti cha kutambua chango mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Bia nchini (TBL) ambayo iliendesha zoezi la upimaji afya kwa madareva, Meneja wa Kiwanda cha Bia Arusha Moshi  Sarvatory Rweyemamundiye aliyepokea kwa niaba ya uongozi wa Kampuni hiyo wakati wa kufunga Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani iliyofanyika kitaifa mkoani Arusha.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Marrison Mwakyoma akipima macho yake kama sehemu ya kuhamasisha upimaji wa fya kwa madereva wa mabasi na magari ya mizigo wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani zoezi hilo lilifanyika eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha
Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akisisitia jambo wakati alipokuwa akipewa maelekezo ya namna wataalamu wanavyochukua vipimo vya afya kutoka kwa madereva wa mabasi na magari ya mizingo wakati wa zoezi la upimaji wa afya lililofanyika Makuyuni wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani


Tanzania yaendelea kunufaika na uhusiano mwema ulipo baina yake na Taifa la China.



Tanzania yaendelea kunufaika na uhusiano mwema ulipo baina yake na Taifa la China.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkk. Mary Nagu akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
 : Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing akigonga glasi ya mvinyo wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
 Picha ya Keki kwa ajili ya hafla ya maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu  na Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing wakikata Keki  wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing (katikati) akiteta jambo na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kuadhimisha miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Afisa anayeshughulikia masuala ya Menejimenti na Programu wa Aga Khana Development Network Bw. Navroz Lakhani
 Msanii wa Jamhuri ya Watu wa China akicheza mchezo wa Wushu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wageni wakisoma vitabu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni wakifuatilia michezo mbalimbali kutoka kwa wasanii wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM.
========  ========  =======
Tanzania yaendelea kunufaika na uhusiano mwema ulipo baina yake na Taifa la China.

Na; Daud Manongi,    WHVUM.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 China imetoa msaada wa zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1.943 kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ushirikiano wa kibiashara  dola bilioni 3.7 na uwekezaji dola bilioni 2.5 na jumla ya makampuni 500 yamewekeza nchini Tanzania.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Nci ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya miaka 65 ya toka kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.

Dkt Nagu amesema kuwa msaada huo utasaidia katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwema Bandari ya Bagamoyo, mradi wa EPZ, usambazaji wa umeme ukanda wa Kaskazini – Mashariki, Elimu kwa njia ya mtandao,Serikali Mtandao kwa ajili ya Zanzibar na Umeme wa upepo katika mkoa wa Singida. Aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua njia za uchumi na kusababisha Tanzania kuwa na uchumi imara na endelevu.

"Najisikia faraja kusema kuwama pamoja na mafanikia chanya tunayopata Tanzania bado ina miradi mingi ambayo inahitaji msaada wa kifedha na kitaalam kutoka kwa Jamhuri ya Watu wa China na ni imani kuwa wataendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha miradi hiyo" Alisema Dkt. Nagu.

Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini Balozi Lui Youqing amesema kuwa nchi yake itaendelea kuisaidi Tanzania kwa kuwa kumekuwa na mahusiano mazuri nay a muda mrefu baina ya nchi hizi mbili.

Balozi Youqing ameongeza kuwa Tanzania inavutia wakezaji kwa kuwa na mazingira salama ya kisiasa na kijamii ambapo anashawishika kuunganisha wawekezaji wa China kushirikiana na wawekezaji wengine katika kupunguza umasikini na kuleta maendeleo akitolea mfano ushirikiano katika sekta ya majengo.

"Tanzania ni nchi kubwa yenye maono na inayovutia zaidi kimataifa kutokana na uimara wake katika Nyanja za siasa na uchumi jamii, imekuwa na ushawishi wa hali ya juu katika anga za kikanda na kimataifa, hali inafanya wawekezaji kutoka sehemu kama EU, US, Japana na kwingineko waongeze uwekezaji, ata mimi binafsi nashawishika kuwashawishi wawekezaji wa China kuwekeza zaidi katika nchi hii" Alisema Balozi Youqing.

China inasherehekea miaka 65 toke kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1949, wkati huo huo ni miaka 50 sasa tokea Taifa kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia kati yake na Tanzania uhusiano ambao umeasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Zedong.
Mwisho.