Showing posts with label Kikwete. Show all posts
Showing posts with label Kikwete. Show all posts

Saturday, November 17, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGA MKUTANO WA MAJAJI JIJINI ARUSHA


Rais Jakaya Kikwete akikufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha Novemba 16, 2012.Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Nhe. Magesa Mulongo Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Sheria Mhe Mathias Chikawe, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi Mhe Fakih Jundu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala ya Waheshimiwa majaji toka kwa muwakilishi wao, Jaji Dkt Fauz Twalib, wakati wa kufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha Novemba 16, 2012.
Rais Jakaya Kikwete akikufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha Novemba 16, 2012.
Waheshimiwa majaji wakimsikilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha Novemba 16, 2012.



Wednesday, November 07, 2012

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI



Rais wa Marekani,Barack Obama akiwahutubia wananchi wa Marekani mara baada ya kutangazwa ni mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo,dhidi ya Mpinzani wake,Mitt Romney.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza furaha na shangwe yake kufuatia ushindi wa jana, Jumanne, Novemba 6, 2012 wa Rais Barack Obama wa Marekani katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.

 Katika salamu zake za pongezi kwa kiongozi huyo wa Marekani ambaye amechaguliwa tena na wananchi wa nchi hiyo kwa kipindi cha pili, Rais Kikwete amesema mapema leo, Jumatano, Novemba 7, 2012:

“Nimepokea kwa furaha na shangwe habari za kuchaguliwa tena kwako kuwa Rais wa Marekani kwa kipindi cha pili. Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kukutumia wewe na kupitia kwako Chama cha Democratic pongezi nyingi kwa ushindi wako wa maana sana.”

Ameongeza Rais kikwete katika salamu zake hizo: “Kuchaguliwa kwako tena kuendelea kuongoza nchi yako muhimu na wananchi wake, ni ishara ya wazi ya uaminifu na imani ambayo wananchi wa Marekani wanayo katika uongozi wako wa mfano.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua tena uongozi wa nchi hiyo katika kipindi chako kipya, napenda kukuhakikishia msimamo wangu binafsi na ule wa Serikali yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa na wewe na Serikali yako ya kutukuka, ili kuendeleza uhusiano bora ulioko kati ya nchi zetu mbili ndugu.”

Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
 Ikulu. 
Dar es Salaam. 
7 Novemba, 2012

Saturday, November 03, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA TAASISI SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDERA ARUSHA



 Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila. 
  Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, hatimiliki ya Ardhi ya chuo hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa chuo hicho iliyofanyika leo Novemba 02, 2012 jijini Arusha. Kuliani ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
 Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

JK Kutembelea Manyoni Mkoani Singida jumatatu ya November 5,2012.




Na Rodrick Ray

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwasili wilayani Manyoni, mkoani Singida Jumatatu ya Novemba 5, mwaka huu kwa ziara siku moja. 
 
Mkuu wa wilaya ya Manyoni, Fatma Toufiq ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo uliofanyika mjini Manyoni. 
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya huyo wakati wa ziara hiyo rais Kikwete atazindua na atafungua barabara ya Manyoni –Isuna ambayo imeshaanza kutumika,atazindua rasmi barabara ya Manyoni –Itigi-Chaya ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami. 
 
Bi Toufiq amesema kutokana na ujio huo wa rais hivyo kila mmoja atachukua nafasi yake kuhakikisha anahamasisha wananchi wake kufika kwa wingi kwenye maeneo hayo kwa sababu hiyo ni miongoni mwa kazi kubwa ambazo serikali imafanya. 
Pamoja na mambo mengine yaliyofanywa na serikali, lakini mkuu wa wilaya huyo amezitaja baadhi kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara itakayofunguliwa jumatatu na kiongozi huyo mkubwa wa kitaifa. 
Hata hivyo, Bi Toufiq amesema pamoja na kazi ya uzinduzi na ufunguzi,vile vile Rais atakuwa na mikutano ya hadhara kwenye maeneo ya Itigi na Manyoni

Sunday, October 28, 2012

IKULU:Taswira Mbalimbali Za Rais Jakaya Kikwete Alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 kuanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Vunjo-TLP Augustine Lyatonga Mre ma Muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 tayari kuanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali na wananchi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 tayari kuanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ngoma baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 tayari kuanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na wananchi baada ya kuwasili wilayani same Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 kwa ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same.
Sehemu ya viongozi mbalimbali  wakiwakatika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 kumlaki Rais Jakaya Kikwete ambae ameanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi  wilayani same Kilimanjaro leo Oktoba 28, 2012 kwa ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same.Picha na IKULU

Saturday, October 20, 2012

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI LEO

-->


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Jordan Rugimbana leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.

Friday, October 19, 2012

State House:Tanzania, Oman to enhance Political and Economic Ties






 Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation exchanges legal instruments with Sultan bin Salim Al Habsi, Secretary General of the Oman Ministry of Financial Affairs.  The Agreements signed were for Promotion and Protection of Investment.  Witnessing the ceremony is H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete.

 Mr. George Yambesi, Permanent Secretary, President's Office (Civil Service) exchanges signed legal instruments with Dr. Hamed bin Mohamed Al Dhawyan, Oman's Under Secretary at the Ministry of Heritage and Culture.  The Agreement based on Cooperation in Records and Archives. 


 Zanzibar's Minister for Labour, Cooperatives and Economic Empowerment, Haroun Ali Suleiman and Oman Minister for Higher Education, Dr. Rawiyah Al Busaidi exchanging legal instruments on Memorandum of Understanding on Cooperation in higher Education between Oman and Zanzibar.  Witnessing the ceremony is H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania.


Mr. Aloyce Joseph Mwamanga, President of Tanzania Chamber of Commerce, Agriculture and Industry signs Agreement on Forming joint Business Council between Tanzania and Oman.  Witnessing the ocassion is Mr. Khalil Abdullah Al Konji (right- seated), Oman's President of Chamber of Commerce and Industry.All photos by Freddy Maro-State House 
--

Tanzania and the Sultanate of Oman yesterday signed various agreements aimed at enhancing political and economic ties between the two countries.  The Agreements were signed during the second day of President Jakaya Mrisho Kikwete's State Visit to the Sultanate of Oman following the invitation of His Majesty Sultan Qaboos bin Said Al Said.

The Agreements were signed yesterday during the joint Tanzania-Oman business forum held at Al Bustan Hotel in Muscat, Oman.  They are: Agreement on Promotion and Protection of Investment, Memorandum of Understanding on Cooperation in higher Education between Oman and Zanzibar, Agreement on Cooperation in Records and Archives and the Agreement on Forming joint Business Council between Oman and Tanzania.

Thursday, October 18, 2012

WA JENGO LA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman katika mtaa wa balozi jijini Muscat Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, (watatu kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh na (kulia) ni Afisa Mwandamizi Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bwana Abdallah Kilima.
 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe,watatu kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Ali Ahmed Saleh, (wanne kulia aliyeshika karai) ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Abdallah Kilima na (kulia anayeshuhudia) ni Afisa katika Ubalozi huo, Bw. Saidi Mussa.Picha na Freddy Maro-IKULU.

Wednesday, October 17, 2012

Rais Jakaya Kikwete:Tanzania na Oman zina mahusiano ya Kidamu na kindugu ambayo ni maalum sana yanayopaswa kudumishwa, kuthaminiwa na kuenziwa kwa dhati.


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya Sultani jijini Muscat jana jioni.Picha na Freddy Maro-IKULU
--
 Tanzania na Oman zina mahusiano ya Kidamu na kindugu ambayo ni  maalum sana yanayopaswa kudumishwa, kuthaminiwa na kuenziwa kwa dhati.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemuambia Mfalme Qaboos Bin Said katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika katika nyumba ya kifalme ya Al -Alam mara baada ya kuwasili katika Taifa la Kifalme la Oman jana  tarehe 15.Octoba, kuanza ziara ya kiserikali ya siku 4.
 
"Tanzania na Oman zina mashirikiano maalum kuliko nchi nyingine yeyote duniani  kwa sababu ya undugu wa damu uliopo baina ya watanzania na wa Oman, hivyo hii ni ziara  maalum sana  katika nchi zetu." Rais amemuambia Mfalme.
 
Mfalme Qaboos amekubaliana na Rais Kikwete na kumueleza kuwa ni muhimu mahusiano haya yakadumishwa zaidi kwa njia ya uwekezaji katika nyanja mbalimbali, hasa katika Viwanda.
Rais Kikwete amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula maalum cha usiku ambapo Rais na ujumbe wake wamehudhuria.
 
Katika ujumbe wake Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof Sospeter Muhongo, Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Dr. Abdallah Kigoda, Waziri wa Kazi, Ushirika  na Uwezeshaji , Zanzibar Mhe. Haroun  Ali Suleiman na Naibu Waziri Fedha wa Tanzania Mhe. Janet Mbene.
 
Katika Ziara hii, Rais amefuatana na wafanyibiashara kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambapo leo tarehe 16 Octoba,2012 atakuwa na kikao na wafanyabiashara wa Tanzania na Oman na hatimaye kutia saini makubaliano ya kibiashara na kiuchumi baina ya nchi mbili hizi.
 
Mbali na kufanya mkutano na wafanyibiashara, leo Rais  atatembelea makumbusho ya jeshi na jioni  atakutana tena na Mfalme kwa ajili ya chakula binafsi cha usiku.
Mwisho.
 
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Muscat – Oman.
16 Oktoba, 2012



Monday, October 15, 2012

RAIS KIKWETE SAFARINI OMAN KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) anaanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne katika Taifa la Kifalme la Oman, ikiwa ni ziara ya kwanza ya Kiserikali kufanywa na Rais wa Tanzania katika nchi hiyo.
Rais Kikwete na ujumbe wake ameondoka mjini Dar es Salaam asubuhi ya leo, Jumatatu, Oktoba 15, 2012, kwenda Oman kuanza ziara hiyo inayofanyika kwa mwaliko wa Kiongozi wa Ufalme wa Oman, Mfalme Qaboos bin Said, ambaye atakuwa mwenyeji wake kwa siku zote nne.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat, Rais Kikwete anatarajiwa kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yousef  bin Abdullah bin Alawi ambaye ataandamana naye hadi Jumba la Muscat Gate ambako Rais atapokelewa na Mfalme Qaboos. Kutoka hapo wataandamana hadi Kasri ya Kifalme ya Al Alam ambako atapokelewa rasmi kwa heshima zote za Kiserikali.
Shughuli kubwa ya jioni ya leo ya Mheshimiwa Rais itakuwa ni kufanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Serikali za Tanzania na Ufalme wa Oman na pia kuhudhuria dhifa rasmi ambayo Mfalme Qaboos atamwandalia mgeni wake kwenye Kasri ya Al Alam.
Kesho, Jumanne, Oktoba 16, 2012, Rais Kikwete atatembelea Jumba la Makumbusho la Majeshi ya Ulinzi ya Oman, atafungua Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman, atashuhudia utiaji saini makubaliano ya mikataba miwili kati ya nchi hizo mbili, ukiwamo ule wa kuundwa kwa Baraza la Biashara la Tanzania na Oman na ule wa Kuendeleza na Kulinda Uwekezaji katika nchi hizo mbili.
Jioni, Rais Kikwete atatunukiwa nishani ya juu kabisa ambayo Ufalme wa Oman hutoa kwa viongozi wa nchi za nje ya First Order Medal kwenye Chakula Maalum cha Usiku kitakachoandaliwa na Mfalme Qaboos kwa heshima ya Rais Kikwete.
Rais Kikwete na ujumbe wake pia utakutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi Oman katika mkutano utakaofanyika kwenye Hoteli ya Kifalme ya Al Bustan.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Mheshimiwa Kikwete kutembelea Oman. Aliitembelea nchi hiyo mara ya kwanza mwaka 1998, wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Oktoba, 2012

Sunday, October 14, 2012

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Ireland hapa nchini by Foreign Affairs New


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Fionnuala Gilsenan, Balozi mpya wa Ireland hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.

Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Mhe. Balozi Gilsenan, Bibi Grace Shangali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anayeshuhudia pembeni mwa Bibi Shangali ni Bi. Felista Rugambwa, Afisa Mambo ya Nje.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Gilsenan mara baada ya kupokea hati za utambulisho za Balozi huyo.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Gilsenan mara baada ya kupokea hati za utambulisho za Balozi huyo. Pembeni mwa Balozi ni Bw. Nicholas Michael, Afisa katika Ubalozi wa Ireland hapa nchini.

Mhe. Balozi Gilsenan akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais.

Mhe. Balozi Gilsenan akisikiliza na kufurahia wimbo wa Taifa lake ulipokuwa ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais. Wengine katika picha kulia kwa Balozi ni Bw. Shaaban Gurumo, Mnikulu na Bw. Japhet Mwaisupule, Kaimu Mkuu wa Itifaki.

Mhe. Balozi Gilsenan akisalimiana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi, Inspekta Billy Kachalle mara baada ya kumaliza kupiga nyimbo za mataifa ya Tanzania na Ireland kwa heshima ya Balozi huyo.