Showing posts with label VISA NA MKASA. Show all posts
Showing posts with label VISA NA MKASA. Show all posts

Monday, October 08, 2012

KAAZI KWELIKWELI AJIPAKA KINYESI MWILINI, ASIKAMATWE NA ASKARI.


Askari wa Jeshi la Polisi wakijihami na matambara pamoja na mifuko ya nailoni ili kumdhibiti mtuhumiwa aliyejipaka kinyesi mwili mzima na kutaka kuwakimbia askari kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Mtuhumiwa huyo ambaye jinalake halikupatikana maramoja alidaiwa kuwa ni mwizi wa simu lakini hakimu alimwachilia huru kutokana na kukosekana ushahidi hata hivyo askari waliendelea kumshikilia tena jambo ambalo lili muudhi na aliporudi mahabusu aliamua kujipaka kinyesi mwilini.
 Hapa wakimchomoa kwenye Chumba Cha Mahabusu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

 Akipandishwa kwenye gari la Polisi.

 Akiondoshwa kwenye eneo hilo.

Tuesday, October 02, 2012

BAADA YA SIMU ZA KICHINA KUFUNGIWA WANANCHI WA KENYA WAIDAI SERIKALI FIDIA





Stori kubwa Kenya ambayo hata kwenye leo  ni kuhusu mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya kuzizima kiteknolojia simu zote zilizofeki ambazo zimekua zikitumiwa na wakenya.

Mtangazaji wa Citizen Tv/Radio William Tuva ameripoti kwamba wakenya walionunua simu feki wapo kwenye wakati mgumu na itawabidi wanunue simu original kwa sasa ili kurudi tena kwenye mawasiliano.

Ameripoti pia kwamba inasemekana katika mtandao wa simu za mkononi wa Safaricom peke yake ni wateja laki sita ambao wameripotiwa simu zao kuzimwa kwa sababu ni feki.

Mbali na hilo  Tuva ameripoti pia kwamba Kenya imepoteza mabilioni ya shilingi kutokana na simu feki ambazo zimekua zikiingia sokoni kwa njia ambayo sio halali.

Baadhi ya wananchi ambao simu zao zimefungwa wamekaririwa wakisema waliamka asubuhi na kukuta simu zao hazifanyi kazi, kumbe tayari zimeshazimwa kiteknolojia na tume ya mawasiliano nchini humo ambapo kwa mujibu wa BBC n wateja milioni mbili na nusu ambao simu zao zimezimwa.


Mmoja wa watu hao amekaririwa akisema “usiku ninawekaga alamu nataka saa 11 niamke, sikusikia naamka tu naona nje kunapambazuka na simu yangu wamezima"

Sunday, September 30, 2012

Umasikini wa akili ndiyo uliyo mbaya kuliko yote ajiua kwa ujinga.



MKAZI wa Singida, Juma Hussein (18) amejiua kwa kunywa dawa ya kuulia wadudu baada ya kupotoshwa na wenzake kuwa ameathirika na Ukimwi kutokana na majibu ya vipimo vyake kuonesha kuwa ni hasi (yaani hajaathirika).

Hussein, ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Dkt. Assery Mchomvu anayeishi Tegeta, Dar es Salaam, alikumbwa na mauti hayo juzi mchana nyumbani kwa daktari huyo.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo, Dkt. Mchomvu alisema siku ya tukio alichelewa kwenda kazini kama ilivyo kawaida yake na wakati Hussein anamtayarishia kifungua kinywa, alimwuliza akitaka kujua inakuwaje mtu anapoambiwa kuwa ana ugonjwa wa zinaa, “Nilimjibu kuwa maana yake ni kwamba mtu huyo amefanya mapenzi bila kinga na atakuwa ameambukizwa magonjwa hatari ya zinaa, lakini tiba yake ni kuwahi hospitali kutibiwa,” alisema daktari huyo.

Alisema baada ya jibu hilo, mfanyakazi wake huyo alionekana kuridhika na kuendelea na kazi, na saa saba mchana akiwa kazini, alipigiwa simu na mfanyakazi wake mwingine wa bustani, Shafii, ambaye alimtaarifu kuwa Hussein amekunywa sumu.Alisema alishitushwa na taarifa hizo na kumtaka kijana wake huyo atoe taarifa kwa majirani ili wamsaidie kumpa huduma ya kwanza, lakini pia kumwahisha hospitali ya jirani Tegeta ili kuokoa maisha yake.

Dkt. Mchomvu alisema kijana huyo, alipewa huduma ya kwanza ya kupewa maziwa na kukimbizwa hospitali ya Mico, Tegeta ambako walibaini kuwa alikunywa kemikali zisizofahamika na kujaribu kumsafisha tumbo, “Hata hivyo, kwa kuwa alikunywa kiasi kikubwa cha dawa ya kuulia wadudu ilishindikana kuokoa uhai wake na alifariki dunia,” Alisema waliporejea nyumbani, Shafii aliwaonesha kikopo cha dawa ya kuulia wadudu inayotumiwa kunyunyizia katika nyumba kikiwa kitupu ambapo walibaini pia kuwa marehemu alikunywa vikombe viwili vya dawa hiyo.

Aidha, alisema walipokagua chumbani kwa kijana huyo walikuta ujumbe aliouandika kwa ndugu, jamaa na marafiki zake, akiwaeleza kuwa wamwombee aendako kwani amepima ili kujua kama ameathirika na UKIMWI na kukutwa ameathirika, “Hata hivyo, cha kushangaza, pembeni ya ujumbe huo tulikuta cheti alichokwenda kupima ugonjwa huo ambacho kinaonesha kuwa ni negative (hajaathirika),” alisema.Alisema alipomhoji Shafii alisema juzi asubuhi alimsikia Hussein akiwapigia simu ndugu zake kijijini kuwataarifu kuwa amepima Ukimwi na kubainika kuwa hajaathirika, hata hivyo walipomhoji cheti kimeandikwa nini, aliwajibu ‘negative’, na kumwambia kuwa maana yake ni kwamba ameathirika.Alisema mwili wa marehemu unafanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Kairuki na baada ya hapo utasafirishwa kwa ajili ya maziko kijijini kwao Singida.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea tukio hilo akisema Hussein alikunywa dawa ya kuulia wadudu aina ya Nuvari 500 CC baada ya kupata hofu kuwa ameathirika na UKIMWI, “Nachukua fursa hii kuwaasa wananchi kuacha kuchukua uamuzi wa haraka hasa wa kukatisha maisha yao, kwani pamoja na kwamba ni dhambi kufanya hivyo, pia ni kinyume cha sheria,” Alisema endapo Hussein angekuwa na subira, angebaini ukweli kuwa neno ‘negative’ halimaanishi kuwa ameathirika na hata kama angeathirika, angeweza kuishi kwa muda mrefu kuliko uamuzi wake wa kukatisha ghafla maisha yake.Habari imeandikwa na Halima Mlacha via HabariLeo

Friday, September 28, 2012

WANYANG’ANYI WAUAJI WA WALINZI WANASWA NA JESHI LA POLISI MWANZA WAKIWA NA MTUTU WA KIENYEJI



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow akionyesha silaha hiyo iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na risasi sita za Short-gun inayohusishwa na matukio ya ujambazi ikiwa ni pamoja na tukio la kumuua mlinzi mmoja na kumjeruhi mwingine kwa kumpiga nondo kichwani maeneo ya Busweru kona Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.


Silaha hiyo iliyotengenezwa kienyeji kwa ukaribu zaidi.

Silaha hiyo iliyotengenezwa kienyeji, risasi zilizokamatwa na RB ya polisi.

JESHI la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wa tukio la ujambazi wakiwa na silaha moja ya kienyeji ikiwa na risasi sita za Short-gun na kukili kufanya uhalifu na kumuua mlinzi mmoja na kumjeruhi mwingine kwa kumpiga nondo kichwani maeneo ya Busweru kona Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow akizungumza ofisini kwake amesema kuwa  jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata majambazi hao wanaohusishwa na tukio lililotokea Septemba 6 mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku katika maeneo ya maduka mawili Busweru kona Kata ya Busweru Wilayani Ilemela ambapo watuhumiwa walimuua mlinzi mmoja Mwita Chariya(40) na kumjeruhi mwingine Mwita Wambura wote wakiwa wakazi wa Mabatini Wilayani Nyamagana.


Kamanda Barlow amesema kuwa baada ya tukio hilo jeshi la polisi liliunda kikosi kazi na kuanza msako wa kuwatafuta wahusika wa tukio hilo huku wakipokea ushirikiano wa raia wema kwa kutumia falsafa ya polisi jamii na ulinzi shirikishi ambapo mnamo Septemba 26 mwaka huu majira ya saa 7:30 walianda mtego na kufanikiwa kumkamata  moja kati ya watuhumiwa  Jonathan Fredrick mkazi wa Nyakato jijini Mwanza akiwa nyumbani kwake. 


Mtuhumiwa huyo baada ya kukamatwa aliwataja wenzake nalo jeshi la polisi likaweka mtego mwingine na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine wawili walio salia Mkubwa Rajab na Jonathan Athuman wote wakazi wa Mabatini.


Watuhumiwa hao licha ya kukiri kufanya matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo hilo la kuua mlinzi waliwaonyesha mahala walipoficha silaha hiyo iliyotengenezwa kienyeji.  

Thursday, September 27, 2012

BILIONEA WA HONGKONG AJITOLEA KUMWAGA DOLA MILIONI 65 KWA MWANAUME ATAKAYEMUOA BINTI YAKE MSAGAJI.


Ghafla isivyo tarajiwa, bilionea mmoja nchini Hong Kong amejitolea kumwaga dola milioni kwa 64 sawa na Paundi milioni 40 ambapo kwa hela zetu za madafu ni bilioni 120, na milioni 400 kwa mwanaume yeyote atakayejitokeza kumuoa binti yake mwenye tabia za kisagaji.
Tajiri huyo mfanyabiashara yuko tayari kutoa mkwanja huo wa hatari kwa mtu atakayemchukua binti huyo ila awe mwerevu, msomi na asiwe ni kwa nia za kujitafutia kipato.
Papaa huyo wa China Cecil Chao Sze-tsung amefikia hatua hiyo kufuatia taarifa kumfikia kuwa binti yake huyo Chao ana mahusiano ya kimapenzi na Sean Yeung  uliodumu kwa muda wa miaka saba (7) nchini Ufaransa.
Binti huyo Chao ambaye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Manchester na pia Mkurugenzi wa Makampuni na Biashara za Baba yake, Anaendesha Kampuni ya walimbwende ya Monde Talent na pia Afisa Uhusiano wa kampuni kubwa nchini Hong Kong.
Hata hivyo Bilionea Cecil Chao amesema hamlazimishi binti yake kuolewa ila atakayejitokeza atakula bingo.

Sean Yeung akiwa na mpenzi wake.
Baba na Mwana.

YALIYOJIRI KATIKA SHOO YA EVANS BUKUKU’S COMEDY CLUB @ NYUMBANI LOUNGE.




Mchekeshaji mahiri Evans Bukuku akiwavunja mbavu wadau waliohudhuria onyesho lake lililofanyika Nyumbani Lounge.
Mmoja wa wachekeshaji wa Evans Bukuku Comed Club ‘Ray’ akiwaburudisha wadau na ‘The Language of Laughter’.
Msanii Enika akitoa burudani ya muziki kwa watu waliohudhuria onyesho hilo.
Wadau wakiwa taabani kwa vicheko wakati wa onyesho hilo.

Friday, September 21, 2012

MOTO UNAODHANIWA KUNATOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA WATEKETEZA MABWENI MAWILI IRINGA



-->
MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza mabweni mawili ya wanafunzi zaidi ya 40 katika Shule ya Sekondari St Marys  iliyopo kata ya limuli, Ifunda  mkoani Iringa , inayomilikiwa na Kanisa la katoliki jimbo la Iringa.

Katika tukio hilo hakuna mwanafunzi aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo licha ya moto huo kuunguza magodoro, vitanda, nguo za wanafunzi pamoja na vifaa mbalimbali. Ajali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki  saa mbili asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani na wengine nje ya bweni

Mwalimu mkuu wa shule hiyo matulinus Kipupwe   anaeleza kuwa ajali hiyo ni ya mara ya pili ambapo nyingine iliwahi tokea mwezi wa saba mwaka huu na kuteketeza baadhi ya mali.
Kipupwe ameongeza kuwa ajali ya moto ilitokea mnamo tarehe 15 septemba muda wa saa mbili asubuhi na kuharibu mali ambazo zinagharimu kiasi cha shilingi milioni 80 na kutaka kuundwa kamati ambayo itashughulikia chanzo cha moto huo pamoja na wizi wa mali za shule.
Katika hatua nyingine, mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine ishengoma  alipotembelea shule hiyo alishangazwa na matukio ya moto huo kujitokeza mara kwamara na kuwataka wananchi kuwafichua watu wanahusika na kuzuka kwa moto huo.
“Tunabahati hatuna mwanfunzi aliyepatwa na tatizo katika ajali hiyo lakini ni lazima tujiulize nini tatizo la kuwepo kwa tatizo hili mara kwa mara”alisema
Dkt Ishengoma ameutaka uongozi kufanya jitihada kwa muda wa siku kumi na kuhahakikisha wanafunzi wanarudi ili kuendelea na masomo yao.
Wakitoa maoni yao mbele mkuu wa mkoa Dkt Ishengoma wananchi  ambao walielekeza hisia zao kutokana na kile kinachosemekana ajali hizi za moto katka shule hiyo zinahusishwa na masuala ya imani za kishirikina kwani walipomaliza zima moto huo uliwaka tena pasipo kufahamu aliyewasha.
Mmoja wa wananchi alieleza kuwa ana wasiwasi na ajali hizi za moto kwani msitu uko mbali sana na shule hiyo na kueleza labda kuna mbinu zinazotumika ambayo zinahusishwa na imani za kishirikina.

Naye diwani wa kata ya lumuli charles luteto ameeleza kuwa amekaa na wananchi wake na kuomba kufanyika uchunguzi kuhusu wakuu wa shule ambayo wamepita katika shule na kujaribu kufahamu kuhusu mahusiano yao pamoja na malipo yao au kutoridhika na kuwa na kinyongo toka kwa watu hao. Wananchi hao pia walisema yawezekana kuna mambo ya kiini macho yanayofanyika ambayo kwa hali ya kawaida hayawezi kubainika.
Chanzo cha moto huo hakijajulikana hivyo wameunda tume ili kufanya kazi hiyo na kutoa tathmini ya hasara iliyojitokeza kuwa ni zaidi ya shilingi mill 80 .
Kutokana na hali hiyo wanafunzi 376 wa shule hiyo wamelazimika kurudi nyumbani ili urekebishaji na ujenzi unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 80 ufanyike.
Huku zikiwa zimebaki siku chache kwa wanafunzi walio kidato cha nne kuingia katika mitihani yao ya taifa itakayoanza tarehe 8 oktoba mwaka huu.


Mabweni yakiwa yameteketea kwa moto pamoja na mali zilizokuwemo

Friday, September 14, 2012

MUINGEREZA AKAMATWA UGANDA KWA USHOGA



 
David Cecil katika mahakama ya Makindye

Msanii moja toka Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa madia ya kuandaa na kuonyesha mchezo wa kuigiza kuhusu ushuga.
Mtayarishi David Cecil wa Uingereza alifikishwa katika mahakama moja mjini Kampala na kushitakiwa kwa madia ya kukaidi na kupuuza amri ya serikali. Polisi wanasema kuwa Muingereza huyo alionyesha mchezo huo wa kuigiza licha ya kwamba Uganda ilipiga marufuku kwa muda onyesho hilo.
Mahakama hiyo iliambiwa kuwa Bwana Cecil alionyesha mchezo huo kwa jina "The river and the mountain" katika ukumbi wa Tilapia Cultural Center taraehe 17 Agosti na pia katika ukumbi mwengine wa Mish Mash Cultural Center tarehe 26 Agosti mjini Kampala.
Mahakama hiyo ya Kampala ilikataa kuamuachilia Muingereza huyo kwa dhamana na badala yake kuagiza awekwe katika gereza la Luzira hadi siku ya jumatatu ,Septemba 17 ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea.
CHANZO: BBC Swahili.

Sunday, September 09, 2012

FLY 540 YAWAWEKA ABIRIA MPAKA USIKU WA MANANE MWALIMU air port


 

 

 
Haya sasa... hata tulipokwenda hotelini bado hapakueleweka kimeo nako..mwendo kukesha

Tuesday, August 07, 2012

Calif. woman tries to steal newborn in tote bag

GARDEN GROVE, Calif. (AP) — A woman disguised in scrubs was caught trying to steal a newborn girl from a Southern California hospital in a tote bag after sensors attached to the baby alerted employees, Garden Grove police said. Grisel Ramirez, 48, was arrested Monday at Garden Grove Medical Center after a hospital staffer stopped her from leaving with the baby, Lt. Jeff Nightengale said during a news conference. "At this point we don't have a solid reason why she stole the baby," Nightengale said.

Ramirez is accused of posing as a nurse who came into the room of the baby's mother and told her to take a shower before a doctor came to examine her, Nightengale said.
Once the baby's mother was out of the room, Ramirez allegedly put the newborn in a purple tie-dyed tote bag and tried to carry her out of the ward.
"An alarm went off when the baby crossed an imaginary line" in the hospital that set off a sensor, Nightengale said.

Many hospital wards have security systems where patients, such as newborns or those with Alzheimer's disease, are tagged with an electronic sensor — usually in a bracelet or anklet — that sets off an alarm when the patient leaves a certain perimeter.

Authorities would not say what kind of system the Garden Grove hospital uses.
Nightengale added that the baby was only in the bag for a short period of time. The baby wasn't harmed and is back in the care of her mother Nightengale credits an alert employee and hospital policies for stopping Ramirez and saving the baby. "The hospital staff reacted as they should," said Nightengale. Authorities are working with other law enforcement agencies to figure out whether Ramirez has made a similar attempt in the past, Nightengale said. Nightengale said Ramirez has no history of mental illness.

Source:AP