-->
Mabweni yakiwa yameteketea kwa moto pamoja na mali zilizokuwemo
MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza mabweni mawili ya wanafunzi zaidi ya 40 katika Shule ya Sekondari St Marys iliyopo kata ya limuli, Ifunda mkoani Iringa , inayomilikiwa na Kanisa la katoliki jimbo la Iringa.
Katika tukio hilo hakuna mwanafunzi aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo licha ya moto huo kuunguza magodoro, vitanda, nguo za wanafunzi pamoja na vifaa mbalimbali. Ajali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki saa mbili asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani na wengine nje ya bweni
Mwalimu mkuu wa shule hiyo matulinus Kipupwe anaeleza kuwa ajali hiyo ni ya mara ya pili ambapo nyingine iliwahi tokea mwezi wa saba mwaka huu na kuteketeza baadhi ya mali.
Kipupwe ameongeza kuwa ajali ya moto ilitokea mnamo tarehe 15 septemba muda wa saa mbili asubuhi na kuharibu mali ambazo zinagharimu kiasi cha shilingi milioni 80 na kutaka kuundwa kamati ambayo itashughulikia chanzo cha moto huo pamoja na wizi wa mali za shule.
Katika hatua nyingine, mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine ishengoma alipotembelea shule hiyo alishangazwa na matukio ya moto huo kujitokeza mara kwamara na kuwataka wananchi kuwafichua watu wanahusika na kuzuka kwa moto huo.
“Tunabahati hatuna mwanfunzi aliyepatwa na tatizo katika ajali hiyo lakini ni lazima tujiulize nini tatizo la kuwepo kwa tatizo hili mara kwa mara”alisema
Dkt Ishengoma ameutaka uongozi kufanya jitihada kwa muda wa siku kumi na kuhahakikisha wanafunzi wanarudi ili kuendelea na masomo yao.
Wakitoa maoni yao mbele mkuu wa mkoa Dkt Ishengoma wananchi ambao walielekeza hisia zao kutokana na kile kinachosemekana ajali hizi za moto katka shule hiyo zinahusishwa na masuala ya imani za kishirikina kwani walipomaliza zima moto huo uliwaka tena pasipo kufahamu aliyewasha.
Mmoja wa wananchi alieleza kuwa ana wasiwasi na ajali hizi za moto kwani msitu uko mbali sana na shule hiyo na kueleza labda kuna mbinu zinazotumika ambayo zinahusishwa na imani za kishirikina.
Naye diwani wa kata ya lumuli charles luteto ameeleza kuwa amekaa na wananchi wake na kuomba kufanyika uchunguzi kuhusu wakuu wa shule ambayo wamepita katika shule na kujaribu kufahamu kuhusu mahusiano yao pamoja na malipo yao au kutoridhika na kuwa na kinyongo toka kwa watu hao. Wananchi hao pia walisema yawezekana kuna mambo ya kiini macho yanayofanyika ambayo kwa hali ya kawaida hayawezi kubainika.
Chanzo cha moto huo hakijajulikana hivyo wameunda tume ili kufanya kazi hiyo na kutoa tathmini ya hasara iliyojitokeza kuwa ni zaidi ya shilingi mill 80 .
Kutokana na hali hiyo wanafunzi 376 wa shule hiyo wamelazimika kurudi nyumbani ili urekebishaji na ujenzi unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 80 ufanyike.
Huku zikiwa zimebaki siku chache kwa wanafunzi walio kidato cha nne kuingia katika mitihani yao ya taifa itakayoanza tarehe 8 oktoba mwaka huu.
Mabweni yakiwa yameteketea kwa moto pamoja na mali zilizokuwemo