Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Friday, November 21, 2014

KASHFA YA IPTL & ESCROW; NIMROD MKONO(MB) ANUSURIKA KUUAWA KWA SUMU LONDON UINGEREZA.



Nimrod Mkono amekoswakoswa kuuawa nchini Uingereza alikokuwa amekwenda kikazi. Aliwekewa sumu ambayo ilipaswa iharibu kabisa figo zake ndani ya saa 72. Uongozi wa bunge umethibitisha na ripoti ya madaktari wa London inaonesha hivyo.

Mkono mwenyewe anasema alionywa kuwa usalama wake uko mashakani na akatakiwa asifikie katika hoteli ambayo ujumbe wa viongozi wa Tanzania utafikia.

Mkoni anasema alipofika London aliamua kwenda katika nyumba take binafsi, lakini baadaye alianza kutoka jasho, kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu kwa saa 6.

Ikumbukwe kuwa Mkono na kampuni yake ya Mkono & Advocates ndiyo iliyokuwa inatetea upande wa TANESCO na Serikali katika kesi dhidi ya IPTL.

Inasemekana Mkono anatafutwa kuuawa kwa sababu inaonekana ana taarifa nyingi mno kuhusu sakata la IPTL na ESCROW, na serikali inamtuhumu kuwa yeye ndiye aliyevujisha nyaraka zote hadi umma wa watanzania kugundua kuwa zaidi ya bilioni 321 mali ya umma zimeibiwa katika sakata hilo.

Chanzo: Gazeti la Citizen la leo 21 Nov 2014.


MY TAKE:
Inawezekana kabisa serikali yetu inahusika au inawafahamu wauaji waliotumwa (iliowatuma) kummaliza Mkono. Kwa sababu serikali inaogopa kuanguka, "Ni bora punda afe mzigo ufike".

Pole sana mhe. Nimrod Mkono, Mungu akupe nguvu na akuponyeshe!

J. Mtatiro,
DSM @#IPTL #And #ESCROW #BRING #Back #Our #Money.

Wednesday, July 02, 2014

KAMA ULIKUWA HUJUI BASI HUU NDIO UTAJIRI WA EDWARD LOWASSA



KAMA ULIKUWA HUJUI BASI HUU NDIO UTAJIRI WA EDWARD LOWASSA


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema madai kwamba yeye ni tajiri hayana ukweli wowote. Amesema yeye ni mfugaji na anamiliki ng'ombe zaidi ya 800 katika Jimbo la Monduli, mkoani Arusha.

Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake wiki iliyopita mjini Dodoma.

"Haya madai hayana hata chembe ya ukweli hata kidogo, isipokuwa mimi nadhani wananitakia mema kwa sababu ukiona jumba zuri wanasema la Lowassa, gari nzuri la Lowassa, kitu chochote kizuri wanasema cha Lowassa," alisema na kuongeza:
"Wamesema uongo mwingi sana, mimi nasema tu nilichopata nimepata na sina utajiri kiasi hicho, lakini si mbadhirifu wa haki zangu ninazopata kama mshahara na haki nyingine."
Alipotakiwa kutaja mali anazomiliki, Lowassa alisema: "Mimi ni mfugaji, nina ng'ombe zaidi ya 800 jimboni kwangu Monduli."
Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli, alisema madai kwamba anamiliki utajiri uliopindukia yalianza kabla hajajiuzulu uwaziri mkuu na ilielezwa kuwa "maduka fulani" ni yake.
Alibainisha kuwa hata kampuni ya Alphatel ambayo wanamiliki kwenye familia yake iliwahi kuhusishwa na jengo kubwa lililojengwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia wilayani Kinondoni, Dar es Salaam likiitwa Alpha.
"Ikaonekana ni jengo langu, kule Mbezi kuna rafiki yangu mmoja walienda watu wakasema hii nyumba ya Lowassa. Yule bwana alitoka na bastola akawakimbiza. Mimi sina nyumba maeneo hayo," alisema Lowassa.


Chanzo: Mwananchi.


MAGUFULI AVUNA WANACHAMA WAPYA 376 KATIKA VIJIJI VITATU




MAGUFULI AVUNA WANACHAMA WAPYA 376 KATIKA VIJIJI VITATU
Mbunge wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioamua kujiunga na chama hicho mara baada ya Mbunge huyo kufanya Mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Nyabugela, kata ya Mganza katika Wilaya ya Chato leo.
Mbunge wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kihutubia mamia ya wakazi wa kata ya Mganza katika Wilaya ya Chato leo.
Wananchi wa Kata ya Mganza wakimfurahia Mbunge wa Jimbo lao la Chato Mheshimiwa Dkt. John Magufuli wakati akiwahutubia na kuwasisitiza wafanye kazi kwa bidii ili waweze kujiletea Maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwapokea wanachama wapya zaidi ya 100 walioamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya mbunge huyo kumaliza hotuba yake.
Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mganza wakila kiapo mbele ya Mbunge wao Mheshimiwa Dkt.John Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama hivi leo.

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli amezidi kuongeza idadi ya wanachama wapya katika Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya mkutano wake wa siku moja kuzoa wanachama wapya 376.

Hali hiyo imekua pigo kubwa kwa vyama vingine vya siasa kwasababu katika muda mfupi wa mikutano ya Mbunge huyo idadi ya wanachama waliotoka katika vyama vya upinzani imezidi kuongezeka.
Katika mikutano hiyo iliyofanyika katika vijiji vya Nyisanzi, Kasenda na Muganza. Dkt. Magufuli alieleza jinsi alivyotekeleza ahadi mbalimbali zilizomo kwenye za Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kutatua kero mbalimbali za wanachi.

"Mlinichagua kwa kura nyingi sana hapa na mimi lazima nionyeshe mfano katika kuwatumikia na naahidi vitu vyote nilivyoahidi nimetekeleza kwa sehemu kubwa kuanzia kwenye shule, huduma za afya, barabara, maji na umeme" alisema Dkt. Magufuli
Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli aliwaasa vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha kudanganywa na wanasiasa uchwara.

"Nawaambia hakuna kitu cha bure, wala hakuna mtu atakayewaletea kitu chochote kama hamtajishughulisha, mfanye kazi muache maneno ya kukaa vijiweni" alisema Dkt Magufuli 
Akizungumza huku akishangiliwa na umati wa watu, Dkt. Magufuli aliwataka wakazi wa Muganza kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa za kiuchumi zinazoanza kufunguka katika kata hiyo.

"Hapa Muganza ndipo linajengwa lango kuu la watalii kuelekea hifadhi ya Taifa ya Rubondo, hivyo ni bora mkajianda mapema na fursa hii, mkikaa bila kufanya kazi fursa hizi zitawapita tu" alisema Dk. Magufuli
Aidha, Mbunge huyo wa Chato pia alisema watanzania wanatakiwa kudumisha Amani iliyopo isije kupotea kwani gharama yake ni kubwa.

Waziri Magufuli alitolea mfano wa nchi za Misri, Libya na Iraq jinsi zilivyokuwa na Amani hapo zamani lakini sasa hivi hali yake ni mbaya watu wanauana kila muda.

"Wakataeni wanasiasa wanaohubiri siasa chafu za kuvuruga Amani, na eti kudai hadi kieleweke vinginevyo damu itamwagika, akija mtu kama huyo mwambieni amwage damu yake kwanza, msimkubali kwani atawapoteza" alisisitiza Dkt. Magufuli.

Katika hatua nyingine Waziri Magufuli amewaahidi wakazi wa Muganza kuwa Serikali itamalizia kipande cha barabara kisichozidi kilomita tatu katika kata hiyo, kwani ni ahadi ya Mhe. Rais na tayari Wizara ya Ujenzi kwenye bajeti yake ya mwaka huu wa fedha 2014/15 imetenga kiasi cha sh. 50.mil kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mwanzo ya ujenzi wa barabara hiyo.

"Serikali ya CCM imeahidi na itatekeleza ahadi yake, tumejenga barabara kila kona ya nchi hatuwezi kushindwa kumalizia kipande hichi kidogo, alisema Dkt. Magufuli .

Pia katika mikutano hiyo waziri Magufuli alitoa michango mbalimbali katika shule na vituo vya afya.


Monday, June 30, 2014

President Jonathan condemn attacks on churches near Chibok...




President Jonathan condemn attacks on churches near Chibok...
Find the State House press release below..
President Goodluck Ebele Jonathan has received with dismay and consternation reports of yesterday's attacks by Boko Haram on churches in  villages near Chibok, Borno State.

The President deplores the renewed targeting by Boko Haram of adherents of a particular religion and urges all lovers of peace and unity to wholly condemn the resurgence of efforts by agents of global terrorism to disunite and destabilize Nigeria by callously instigating violence among religious groups in the country.


President Jonathan shares the view of the most learned Islamic leaders and scholars that no true Muslim will resort to the mindless killing of innocent people at any time, especially not during the holy month of Ramadan, to redress any perceived grievance.

The President believes, therefore, that Sunday's attacks on churches and other similar atrocities by Boko Haram are conclusive proof, if any is still needed, that its leaders and members are  thoroughly misguided persons who are only using religion as a cover for their reprehensible crimes against their countrymen and women.

President Jonathan urges all Nigerians, irrespective of their religious beliefs, to resist this new attempt to undermine the nation's firm and collective resolve to unite in full support of its armed forces and security agencies against the vicious perpetrators of brutal attacks on innocent citizens.

The President assures all Nigerians once again that the Federal Government and national security agencies will continue to intensify ongoing efforts to end Boko Haram's senseless attacks until the terrorists are routed and totally defeated.  

He commiserates with the families and churches that lost loved ones, members and places of worship during Sunday's attacks.


REUBEN ABATI
Special Adviser to the President

(Media & Publicity)
June 30, 2014

Msajili wa vyama vya Siasa Jaji F. Mutungi amzuia Mbowe kugombea uenyekiti tena


Msajili wa vyama vya Siasa Jaji F. Mutungi amzuia Mbowe kugombea uenyekiti tena


Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.

Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.

Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa chama hicho. Mutungi alisema baada 


ya kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.

"Mjadala kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao vya chini," alisema Dk Slaa.

Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: "Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba"

Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.Alisema kama chama hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi kuitambua ibara hiyo.Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa kazi.

"Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema," alisema katika barua hiyo 


Naibu Katibu Mkuu CUF Bara aliyechukua nafasi ya Julius Mtatiro anusurika katika ajali



Naibu Katibu Mkuu CUF Bara aliyechukua nafasi ya Julius Mtatiro anusurika katika ajali

Naibu Katibu m kuu mpya wa CUF pia Mbunge wa viti Maalum Magdalena Sakaya akimshukuru Mungu baada ya kunusurika katika ajali na Lori kwenye makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere Dar


 
Picha na Robert Okanda 


ZITTO KABWE: FEDHA ZA IPTL NI MALI YA UMMA!




ZITTO KABWE: FEDHA ZA IPTL NI MALI YA UMMA!
Kwa mara nyingine serikali kupitia viongozi na watendaji wake akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika 'Tegeta Escrow Account' si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma. Akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Limited (IPTL).

Kwa bahati mbaya sana viongozi wa serikali wamekuwa wakiendelea kurudia kuueneza huo uongo kwamba fedha hizo si mali ya umma. Inasikitisha pia kwamba vyombo vya habari vimekuwa navyo vikibeba na kusambaza huo uongo bila kuhoji na kuchunguza. Inashangaza sana pia asasi za kiraia nazo zimekaa kimya. Inatisha na kushangaa tena kuona wapinzani wakimwachia suala hili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, pekee wakati mapambano dhidi ya rushwa ni ajenda kuu ya wapinzani. Kafulila amekuwa akiendelea kuhoji suala hilo bungeni peke yake bila kupata kuungwa mkono na kupewa msaada wa aina yoyote kutoka kwa wenzake wa kambi ya upinzani bungeni.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza kuwapo kwa ukaguzi maalumu kwenye akaunti hiyo ya Tegeta escrow account iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo fedha za umma. PAC haina sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo. Agizo hilo la POAC lilitokana na sababu kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za Tanesco.
Akaunti ya 'Tegeta escrow' ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa TANESCO. Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL. Kwa uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu ya escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.
Hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Disemba 2012 za Tanesco zinaonyesha wazi kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja. Fedha za kampuni ni suala la kisheria kama inavyobainishwa katika sheria ya kampuni ya mwaka 2002.
Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100? Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma? Je ni baada ya baadhi ya watendaji wa serikali kula njama za kuzichukua fedha hizo kwa kushirikiana na 'mwekezaji' aliyechafuka kwa ufisadi duniani?
Serikali inadanganya waziwazi kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma. Umma una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika lile sakata la ufisadi maarufu wa EPA unaofanana kwa kila hali na huu wa sasa wa 'Tegeta Escrow'.
Hoja nyingine ni kwamba, Mbunge Kafulila alisema kwamba Jaji Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania hakutoa uamuzi wa kuchukuliwa fedha kutoka akaunti ya 'Tegeta Escrow'. Nimepitia kwa makini hukumu ya Jaji Utamwa na kubaini kwamba hakuna popote alipotaja akaunti ya 'Escrow'. Hata hivyo, nilipopitia muhstasari wa kikao kati ya TANESCO, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini, ndipo kwa mara ya kwanza nikakuta wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za 'Tegeta Escrow' zipewe kampuni ya PAP (inamilikiwa kwa asilimia 50 na Harbinder Singh na 50% na Simba Trust iliyosajiliwa Australia). Hiki ndicho kikao kilichofanya maamuzi ya kuiba na kugawana wenyewe fedha hizo (Hukumu ya Jaji Utamwa na muhstasari wa kikao vinaambatanishwa).
Wote waliohudhuria kikao hicho kilichojipa mamlaka ya kutafsiri hukumu ya Mahakama Kuu, wanapaswa kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria zilizopo. Inawezekana vipi uamuzi wa mahakama ukatafsiriwa na kikao cha Wizara? Muhstasari wa kikao hicho ndio uliowasilishwa Benki Kuu (BoT) kuhalalisha madai kwamba fedha hizo lazima zitolewa kutoka akaunti ya Escrow.
Fedha zinazohusiana na akaunti ya Escrow ni Dola za Marekani milioni 250, katia ya hizo Dola milioni 122 zilizokuwa BoT zimeshatolewa na kiasi kilichosalia Dola milioni 128 zitalipwa na Tanesco kutokana na fedha zake kwa madai ya kushindwa kulipa kwa wakati. Fedha zilizolipwa ni zile ambazo zimetoka Wizara ya Nishati na Madini ambayo kisheria ndio walipaswa kulipia gharama za uzalishaji umeme (capacity charge) fedha zilizotoka kwa walipa kodi.
Ikumbukwe kwamba uhamishaji wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda PAP umeambatana na nyaraka za kughushi kutokana na kutokuwepo kabisa kwa uthibitisho wa cheti halisi cha hisa (share certificate) kutoka kampuni ya Mechmar kwenda kampuni ya Piperlink. Nyaraka za TRA zinaonyesha kwamba hisa hizo (70%) ziliuzwa kwa Shilingi za Kitanzania milioni sita (6) tu. Na bado hakuna ushahidi kuonyesha kwamba uhamishaji huo wa hisa ulipata baraka za mamlaka husika kama inavyotakiwa na sheria za nchi.
Wakati huyo anayejiita mmiliki mpya wa IPTL aliposaini mkataba wa kuchukua fedha kutoka akaunti ya Escrow zilizokuwapo BoT, hakuwa mmiliki halali kisheria kwani kodi ililipwa siku moja baada ya wao kupokea fedha kutoka BoT. Sheria inataka kutolewa kwa cheti na Kamishna wa TRA kama uthibitisho kwamba kodi yote imelipwa ipasavyo (Sheria ya Fedha ya 2012 kifungu cha 29).
Ni nani wamiliki wengine wa kampuni ya PAP? Uchunguzi ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini.
Inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh aliyechukua fedha za Escrow, anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na ya kampuni ya Simba Trust. Kitalu hicho cha mafuta kinaitwa 'Mnazi Bay North', jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara.
Tunatarajia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua ukweli wa sakata hili na TAKUKURU itawafikisha mahakamani wahusika bila kujali nyadhifa zao serikalini.
Kauli ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kwamba kuna watu waliokula rushwa na kwamba nyaraka zinazotajwa ni karatasi za kuuzia vitumbua, ni kauli zenye kuonyesha kutapatapa kwa watendaji serikalini. Hakuna hata mahali pamoja ambapo nimemtaja mtu kuwa ni mwizi zaidi ya kuwasilisha hoja zinazohitaji majibu mwafaka na si matusi, vitisho na tuhuma za kuzusha. Nyaraka za TRA haziwezi kuwa za kufungua maandazi kama ambavyo hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu haiwezi kuwa karatasi za kufungia maandazi na badala yake ni nyaraka halali zinazohitaji maelezo kutoka kwa viongozi na watendaji wa serikali badala ya kuropoka na kuporomosha matusi.
Hali kadhalika, Bunge lina kila sababu kupitia sheria yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kulinda hadhi yake kutoka kwa watendaji kama Maswi ambao wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge. Maswi na wengine kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi kupayuka ovyo bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama TAKUKURU na polisi ili wachunguze na kuchukua hatua kama ambavyo vinawachunguza wao.
Kauli ya Maswi kwamba "wanaume" hawazungumzi ndani ya Bunge si tu udhalilishaji wa chombo hicho bali pia inaashiria ugonjwa wa mfumo dume uliotawala miongoni mwa viongozi wetu kwa maana kwamba wanaume ndio wenye hadhi, uwezo na heshima na wanawake ni dhaifu na wasiostahili heshima. Tufumbue macho tuone na tuondoe hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo yetu ya kisiasa. Tuwe wazalendo ili tuweze kusimamia utaifa.


Sunday, June 29, 2014

Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi CUF wakutana


Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi CUF wakutana
 Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi CUF wakiwa katika picha ya pamoja katika makao makuu ya chama hicho Buguruni jiji i Dar es Salaam
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu Maalim Seif wakisalimiana na wajumbe baada ya picha ya pamoja


Wednesday, May 14, 2014

NJEMBA ALA KICHAPO KITAKATIFU KATIKA MKUTANO WA UKAWA



Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Moro.
NJEMBA mmoja amepokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jioni hii baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge Rose Kamli wakati wa kampeni jimboni Kalenga, mkoani Iringa.

Wednesday, November 07, 2012

HABARI KAMILI KUHUSU KUSHITAKIWA KWA RAIS KIKWETE





Na: Julius Magodi, Dodoma

SUALA la kuwapo kwa majaji wasiokuwa na sifa nchini limeingia katika sura mpya baada ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kusema atawasilisha hoja ya kumshtaki Rais Jakaya Kikwete kama atashindwa kuwaondoa kazini ifikapo Kikao cha Bunge lijalo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.

Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Rais Kikwete ambaye ana mamlaka ya kuteua majaji, ameshindwa kuwaondoa kazini majaji hao wasiokuwa na sifa. Lissu alisema atawasilisha hoja yake hiyo kwa kutumia Kanuni ya Bunge sehemu ya 11, Ibara ya 121, 122, 123, 124, 125 na 126 na pia kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 146 A. Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki Rais kwa madhumuni ya kumwondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 46 A ya Katiba ikiwa inadaiwa kwamba Rais; ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma. Lissu alisema atakusanya saini za wabunge kuunga mkono hoja yake ambayo ni asilimia 20 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. 

Wabunge wote kikatiba ni 357. Julai 13, mwaka huu wakati akitoa maoni ya Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Katiba na Sheria bungeni, Lissu alisema uteuzi wa majaji umegubikwa na ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. 

Alisema baadhi ya majaji walioteuliwa hawana sifa, uwezo na kwamba hawakufaa kufanya kazi hiyo. Kauli hiyo ilisababisha Bunge kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Hassan Ngwilizi kumhoji ili athibitishe kauli yake.

Alisema wakati akihojiwa na kamati hiyo, pamoja na nyaraka nyingine, aliwasilisha nakala ya ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa mwaka 2008 na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuchunguza uteuzi wa majaji nchini. Alisema ripoti ya kikosi kazi hicho kilibaini kuwapo majaji ambao hawana sifa ya kufanya kazi hiyo, lakini Rais Kikwete ameshindwa kuwaondoa kazini.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alisema hali ya mahakama ni mbaya, kwani kuna majaji wawili ambao waliwahi kukamatwa kwa rushwa wakiwa mawakili, lakini wakateuliwa kufanya kazi hiyo. Alisema baadhi ya majaji hawana uwezo hata wa kuandika hukumu kutokana na kutojua vyema lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo inayotumika katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.

Mbunge huyo alimtaja Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ambaye ameteuliwa akisema hana hata shahada ya kwanza ya sheria kinyume cha taratibu.“Kwa mfano, yupo Jaji wa Mahakama ya Rufani (jina tunalo), ambaye hana hata shahada ya sheria anaweza vipi kuwa jaji?,” alihoji Lissu. Alisema jaji huyo hivi sasa anasoma shahada ya sheria katika chuo kikuu kimoja hapa nchini. 

Lissu alisema ili mtu aweze kuchaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu lazima awe na elimu ya shahada ya kwanza ya sheria, awe ametumikia miaka 10 mahakamani na anayechaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani lazima awe ametumikia miaka 15 mahakamani. 

Mbali ya kueleza hayo, Lissu alisema kwamba alitoa pia katika kamati hiyo, ushahidi unaoonyesha kuwa kuna jaji mmoja wa Mahakama Kuu ambaye hawezi hata kuandika sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka... 

“Kama jaji hawezi kuandika hata sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka, tunaweza vipi kuwa na mahakama inayotenda haki?”Alisema kuna jaji mwingine ambaye ameongezewa mkataba wa kufanya kazi mara ya tatu kitu ambacho ni kinyume cha sheria. 

Alisema kwa mujibu wa Tume ya Mahakama, hakuna jaji ambaye anaweza kufanya kazi kwa mkataba kwa vipindi vitatu. Mbunge huyo alisema mbali ya madudu hayo katika sekta ya mahakama, hivi sasa kuna jaji maarufu ambaye ameghushi umri wa kuzaliwa ili aweze kuendelea kufanya kazi hiyo. 

Alisema jaji huyo amezaliwa Septemba 4, 1949 lakini amebadilisha umri wake kuwa amezaliwa Septemba 4, 1952 ili aweze kufanya kazi hiyo hadi mwaka 2017. Mbunge huyo alisema kazi hiyo ya kughushi umri wa jaji huyo imefanywa kwa kunyofoa nyaraka za kumbukumbu zake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Alimtaka jaji huyo kuzirejesha mara moja nyaraka hizo vinginevyo katika Bunge lijalo atamtaja kwa jina hadharani. Alipotakiwa kueleza kwa nini asimtaje sasa alisema akifanya hivyo anaweza kutingisha nchi. Kama Lissu atachukua hatua hiyo, itakuwa ni mara ya pili kwa mbunge kuwasilisha bungeni hoja ya kutaka kumwajibisha kiongozi wa juu serikalini. 

Mara ya kwanza alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe katika Bunge lililopita alipokusanya saini za wabunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitaka awajibishe baadhi ya mawaziri waliokuwa wametajwa kuhusika katika matumizi mabaya ya madaraka katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). 

Hata hivyo, Rais Kikwete alifanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la Mawaziri hivyo kuzima hoja hiyo ya Zitto.

CHANZO:http://www.mwananchi.co.tz/habari

Wednesday, October 31, 2012

Wananchi Kuchangia Katiba Kwa SMS



Wananchi sasa kutuma maoni kuhusu Katiba Mpya kwa 'sms' Jumatano, Oktoba 31, 2012 Na Mwandishi Wetu Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza namba nne (04) za simu za mkononi ambazo wananchi kwa sasa wanaweza kuzitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ('sms') kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Kwa mujibu wa taarifa ya Tume hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo (Jumatano, Oktoba 31, 2012) namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao kwa njia ya 'sms' ni 0715 (Tigo) /0767 (Vodacom) / 0787 (Airtel) / 0774 (Zantel) – 08 15 08. "Kwa kuzingatia kuwa Watanzania wengi waliopo mijini na vijijini wanamiliki simu za mkononi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaamini kuwa njia hii ni fursa nyingine muhimu kwa Watanzania kuweza kuwasilisha maoni yao kwa Tume," imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid. Ili kutuma maoni, Bw. Assaa amesema, mwananchi anapaswa kufungua ukurasa wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) katika simu yake na kuandika maoni yake pamoja na jina lake kamili, jinsia, mahali anapoishi, umri, elimu na kazi na kutuma kwenda kwenye namba yoyote kati ya zilizotolewa. Kwa mujibu wa Bw. Assaa, baada ya kutumwa, maoni hayo yatakwenda kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambapo yatafanyiwa kazi pamoja na maoni yanayokusanywa kwa njia nyingine. Uanzishwaji wa njia hii ya ujumbe mfupi wa maandishi unalenga kuwapa fursa nyingine wananchi kutoa maoni yao. Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inapokea maoni ya wananchi kupitia mikutano ya ana kwa ana; barua pepe (maoni@katiba.go.tz); njia za posta (S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar); ukurasa wa 'facebook' (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na tovuti (http://www.katiba.go.tz/). Katika taarifa yake hiyo, Tume imewaomba wananchi kutumia namba hizo kutuma maoni yao binafsi kuhusu Katiba Mpya bila kushawishiwa na watu, makundi, vyama au taasisi yoyote na kufafanua kuwa Tume inatarajia kuanza kupokea maoni ya makundi, vyama na taasisi mara baada ya kumaliza kukusanya maoni binafsi ya wananchi katika awamu ya nne na ya mwisho itakayomalizika mwezi Desemba, 2012.



Wednesday, October 17, 2012

DIALLO MWENYEKITI MPYA CCM MWANZA, MABINA KUKATA RUFAA KUPINGA MATOKEO .....!!!



Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, na mbunge wa zamani wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Anthony Mwandu Diallo, ameibuka mshindi kwa kura 611 katika wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, kisha kumgalagaza aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Clement Gregory Mabina aliyepata kura 328.

Pichani Wadau wa uchaguzi wa mkutano mkuu wa mkoa wa mwanza wakijipanga kabla ya uchaguzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 Wajumbe kupitia utaratibu uliowekwa walijipanga kwenye mistari kwenda kupiga kura kuchagua viongozi nafasi mbalimbali.

 Huu ndio utaratibu wa zoezi la kupiga kura katika Mkutano mkuu wa mkoa wa Mwanza.

 Kisha unatumbukiza hapa kwenye vyombo hivi vya wazi...

 Zoezi gumu la uhesabu kura ukafuata....

 Wajumbe wakaserebuka kusubiri matokeo ingawa simu zilizuiwa kuingia kwenye chumba cha kuhesabu kura.. lakini wapi...!!  Habari zilipenya, mara tetesi kwa upande wa magharibi wakiwa wamenuna kumaanisha kuwa imekula kwao, nao mashariki wakifunguka kwa matabasamu kumaanisha yaliyomo yamo, ukiuliza aku tunafurahia muziki...tehe-te...

 Dj Chris kutoka Semira mobile Sound ndiye aliyekuwa akimwaga burudani kwa wajumbe kuvuta subira kungoja matokeo rasmi kutangazwa....kulikuwa hakuna pombe lakini watu walilewa.

 Wakati huo wajumbe wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano huona habari nyinginezo duniani kupitia www.gsengo.blogspot.com

Mbali na Diallo, wagombea wengine wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, waliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi ni pamoja na Zebedayo Athumani (kura 4), Hussein Mashimba (kura15), Joseph Langula Yared (kura 30), na Mabina ambaye alipata (kura 328) wote kati ya kura zote 988 halali zilizopigwa.


Wakati wa kutoa shukurani mwenyekiti aliyekuwa akitetea kiti hicho na kuangushwa Mh. Clement Mabina mbali na kupinga matokeo hayo waziwazi akidai kuwa atakwenda kukata rufaa,  ilidaiwa kuwepo kwa mchezo mchafu ambapo mmoja wa wagombea alidaiwa kutoa rushwa ya sh. 50,000 kwa kila mjumbe, kati ya wajumbe wanaokadiriwa kufikia 988, na kwamba inadaiwa kigogo huyo alitumia zaidi ya sh. Milioni 56 kwa lengo la kutafuta ushindi wa nafasi uenyekiti.


Maneno hayo yaliifanya meza kuu kuwa na tafakuri za kina huku minong'ono ya hapa na pale ikitawala... sssssSSSSSsssss!!!... sikiliza kesho Amlifaya na Millard Ayo.

Diallo akitoa neno la shukurani...

Msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisimama na kusema kuwa mkutano huo ni halali na umefuata taratibu zote hivyo kama Mabina anadai kuwa si halali kwa vigezo alivyotaja basi akate rufaa na tume ya uchunguzi haito bagua kukagua mgombea anayelalamikiwa tu! bali itakaguwa wagombea wote wa nafasi ya U-enyekiti mkoa.

Viongozi ambao pia ni wajumbe wa mkutano huo toka kada mbalimbali wakifuatilia hitimisho la mkutano huo ndani ya dimba la CCM Kirumba MZ.

Mwenyekiti mpya Dr. Anthony Diallo akizungumza na waandishi wa habari.

Uchaguzi huo ulifanikiwa pia kuwachagua wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza, ambapo waliochaguliwa na wilaya wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Mwamba Makune na Christine Mwalu Jilala (Misungwi), Joseph Langula Yared na Marco Mabihya (Sengerema), Stella Aya, Raban Mageje (Magu).


Wengine ni Angelina Mabula, Dede Swila (Ilemela), Sikitu Sanziyote na Charles Marwa Nyamasiriri (Nyamagana), George Nyamaha na Benadethar (Ukerewe), huku wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza wilaya Kwimba waliochaguliwa ni Bujiku Philip Sakila na Dominic Kadaraja.