Showing posts with label Ajali. Show all posts
Showing posts with label Ajali. Show all posts

Wednesday, July 02, 2014

AJALI MBAYA MAENEO YA BUNJU A JIONI LIVE!!


AJALI MBAYA MAENEO YA BUNJU A JIONI LIVE!!
UZEMBE WA MADEREVA NDIYO CHNZO CHA AJARI TANZANIA AJARI HII IMETOKEA BUNJU A DAR-SALAAM. DEREVA WA LORI ALITAKA KULIPITA GARI DOGO  LILILOKUWA MBELE YAKE WAKATI HUO HUO KARI DOGO HILO LILIKUWA LINA PINDA KONA HIKI NDICHO KILICHOTOEA. BAATI MZURI AKUKUTOKEA KIFO KATIKA AJARI HII.


MH. PINDA ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA



MH. PINDA ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama asali kutoka Ilagala, Kigoma wakati alipotembelea banda la Asali kwenye maonyesho ya Biashara ya Kiataifa yanayoendelea kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es salaam Jumlai 2, 2014. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Bishara, Dr.Abdallah Kigoda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama asali kutoka Ilagala, Kigoma wakati alipotembelea banda la Asali kwenye maonyesho ya Biashara ya Kiataifa yanayoendelea kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es salaam Julai 2, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Friday, November 02, 2012

BREAKING NEWSSS WATOTO WAWILI WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI IMEZU INYALA MBEYA WAGONGWA NA ROLI NA KUFARIKI PAPO HAPO



Miili  ya wanafunzi wa shule ya msingi imezu ikichukuliwa na wanausalama watoto hao walikuwa wakivuka barabara akielekea shuleni ndipo roli hilo lilipowagonga na kukimbia huku miili ya watoto hao ikiwa imetawanyika vipandevipande ajali hiyo imetokea mida ya saa moja na nusu asubuhi
Watoto hao wamegongwa katika barabara kuu itokayo Zambia kwenda dsm maeneo ya imezu inyara wilaya ya mbeya vijijini
Waanchi kwa hasira wameamua kufunga barabara hiyo wakimtaka mkuu wa mkoa mbeya aje afike eneo la tukio  wamweleze kero zao za barabara hiyo kwani sasa inawamaliza wanakijiji hao kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo
Vijana wameshaanza kuweka mawe barabarani kuzuia magari yasipite na ukizingatia hii ndiyo barabara kuu ya magari yaendayo Malawi na zambia na mikoa ya jirani


Habari kamili tutawaletea baadae mpaka tunaondoka eneo la tukio mkuu wa mkoa Mbeya bado hajafika eneo la tukio 
na habari zisizo rasmi dereva aliyewagonga watoto hao kajisalimisha katika kituo cha polisi inyala

Picha habari na Mbeya yetu

Monday, October 15, 2012

Watu wanne wapoteza Maisha ajalini Bahi, Dodoma


Na. Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Abiria wanne waliokuwa wakisafiri katika Daladala (Hiace) iliyokuwa inatokea Dodoma kuelekea kijiji cha Mkanda wilayani Manyoni Mkoa Singida wamepoteza Maisha katika tukio la ajali na kuwaacha abiria wengine kumi na nane wakiwa majeruhi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kuwa ilitokea siku ya Jumapili tarehe 14/10/2012 majira ya saa kumi jioni (16:00hrs) katika Kijiji cha Uhelela Kata ya Bahi Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma katika barabara kuu ya Dodoma/Singida.
Bw. Zelothe Stephen alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T.518 AVQ aina ya SCANIA likiwa na tela lenye namba za usajili T.780 AVK lililokuwa linaendeshwa na Dereva TUTU ACKSON mwenye umri wa miaka 23, Mkazi wa Chaduru, na gari namba T. 803 AHX aina ya TOYOTA HIACE lililokuwa likiendeshwa na DANIEL JACKSON mwenye umri wa miaka 46, mkazi wa Dodoma.
Aliwataja waliopoteza Maisha katika ajali hiyo kuwa ni abiria wanne waliokuwa wakisafiri na Hiace hiyo ambao ni MASHAKA ELIA mwenye umri wa miaka (27) ambaye ni kondakta, mkazi wa Chang’ombe Mkoani Dodoma, MOSI MAUNDAA mwenye umri wa miaka (55) mkazi wa wilaya ya manyoni, EZEKIELI MASALITO mwenye umri wa miaka kati ya (40-45) mkazi wa Makanda wilaya ya Manyoni na DASTAN KIPINGU mwenye umri wa miaka (35) ambaye hakufahamika ni mkazi wa wapi.
Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dododma alisema Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Bahi ikisubiri kuletwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa Uchunguzi zaidi wa Daktari, wakati majeruhi wengine kumi na tano (15) wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.
“Katika ajali hiyo Abiria kumi na nane (18) walijeruhiwa akiwemo Dereva wa Daladala hiyo, ambapo kati yao wanaume waliojeruhiwa ni 15 akiwemo mtoto mdogo mmoja na wanawake watatu (3).” Alifafanua Kamanda Zelothe
Bw. Zelothe aliwataja waliotibiwa na kuruhusiwa kuwa ni ESTER FUNGA mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, aliyejeruhiwa katika mkono wa kushoto na usoni, CHRISTINA DANIEL mwenye umri wa miaka (25) mhudumu wa hoteli, mkazi wa Ipagala, ambaye ameumia mkono wa kulia na mguu wa kulia na GREYSON OMARY mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni ambaye ameumia kichwani.
Aidha Kamanda Zelothe alitaja orodha ya majina ya waliojeruhiwa kuwa ni
DANIEL JACKSON @ NZOYA mwenye umri wa miaka (46) Dereva wa Toyota Hiace, mkazi wa Bahi road Dodoma, ANTONY CHAKA mwenye umri wa miaka (23) mkazi wa Makanda Manyoni, JOSEPH CHRISOPHER mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa Makanda, VENANCE MIRAJI mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, MASONGA BURUGE mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, PROTAS MWALUKO mwenye umri wa miaka (70) mkazi wa Makanda wilayani Manyoni na PEASON MAGUMILA mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Kibaigwa wilayani Kongwa.
Wengine ni TIMITA MADATILO mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Makanda wilayani Manyoni, MATONYA MWENDAUHEMBA mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa wilaya ya Bahi, MASHAKA ELIA mwenye umri wa miaka (27) mkazi wa Chang’ombe Dodoma, TITUS MTWEVE mwenye umri wa miaka (32) mwalimu wa shule ya sekondari Manyoni, JUMA SHABANI mwenye umri wa miaka (35) mkazi wa Makanda wilyani Manyoni, SOPHIA LEMA mwenye umri wa miaka (52) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, RAMADHANI ABDALLAH mwenye umri wa miaka (38) mkazi wa wilyani Manyoni na mwanaume ambaye hajafahamika jina mwenye umri kati ya (35-40) ambaye hali yake ni mbaya.
Bw. Zelothe Stephen alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori hilo ambaye aliigonga kwa nyuma gari hilo la abiria iliyokuwa mbele yake na kuitoa nje ya barabara na kusababisha ajali hiyo, Dereva wa Lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam likielekea Kigoma amekamatwa na utaratibu wa kumfikisha mahakamani unaandaliwa.

Friday, October 12, 2012

KIKOSI CHA ZIMAMOTO MBEYA WASIFIWA KUWAHI KWENYE TUKIO LA MOTO SOKO LA UYOLE by Mbeya YetuKIKOSI CHA ZIMAMOTO MBEYA WASIFIWA KUWAHI KWENYE TUKIO LA MOTO SOKO LA UYOLE



MOTO MKUBWA ULIOSABABISHWA NA HITILAFU YA UMEME UMEUNGUZA MADUKA MATATU KATIKA SOKO LA UYOLE MBEYA USIKU WA  TAREHE 10/10 


WAKAZI WA UYOLE WAMEWASHUKURU KIKOSI CHA ZIMAMOTO KWA KUWAHI ENEO LA TUKIO NA KUWAHI ZIMA MOTO HUO MAANA BILA KUWAHI KIKOSO HICHO SOKO LOTE LINGETEKETEA KWA MOTO

BAADHI YA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA UYOLE WAKIOKOA MALIZAO SISIUNGUE NA MOTO

NAIBU MEYA WA JIJI LA MBEYA MH, FUNGO MOJA WA VIONGOZI WALIOTEMBELEA ENEO HILO LA SOKO

WAKAZI WA UYOLE WAKIANGALIA MABAKI YA BIDHAA MBALIMBALI ZILIZOUNGUA KATIKA MADUKA YA SOKO HILO LA UYOLE





Monday, October 08, 2012

BODA BODA YAUA DEREVA NA ABIRIA WAKE PAPO HAPO ENEO LA MAKONGO JIJINI DAR LEO from MTAA KWA MTAA



Dereva wa Bodaboda na abiria wake, ambao hawakuweza kufahamika majina yao kwa haraka, wakiwa wamelazwa pembeni mwa barabara ya Bagamoyo eneo la Makongo, baada ya kugongwa na gari aina ya Starlet yenye namba za usajiri T 838 BKB, wakati wakiwa katika Pikipiki yao yenye namba za usajiri T 491 BFY, na kufariki dunia papo hapo. Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi, Pichani ni raia akijaribu kutambua mwili wa marehemu katika ajali hiyo. Picha na Sufiani Mafoto Blog.

Saturday, October 06, 2012

Just In: Kuna ajali imetokea Eneo la Mafiati Mbeya muda huu, kati ya Pick Up na Hiace . Watu watatu wanusurika Kifo!



 Hivi ndivyo Daladala ilivyo gongwa na pick up

 Kioo cha daladala kikiwa kimebomoka bomoka baada ya ajali
 Hili Ndilo Gari aina ya Pick up ambalo ndilo limesababisha ajali hiyo
 Baadhi ya watu wakiwa wanakuja kushuhudia tukio

 Watu wakiwa wameongezeka kushuhudia tukio


**********************************
Ajali hii imetokea muda huu maeneo ya Mafiati Jijini Mbeya ambapo imesababishwa na Gari aina ya Pick up ambayo ilikuwa katika Mwendo kasi sana na kushindwa kuhimili mwendo kasi wake kisha Kugonga Hiace ambayo ilikuwa imetoka Iyunga kuelekea Mwanjelwa. Katika ajali hii watu watatu wamejeruhiwa.

PICHA ZOTE NA : www.mbeyayetu.blogspot.com

Friday, October 05, 2012

Breaking News> Ajali mbaya yatokea Mwanza leo.



                                             Gari iliyosababisha ajali mwonekano wa mbele.
                                                             Hapa zikiwa zimegongana.
                                                          Mwonekano wa mbele...
                                               Wananchi wakishuhudia ajali ilivyotokea.
 Ilikuwa hali mbaya sana eneo la national ambapo kama unanyowaona watu wanaangalia ndivyo ilikuwa na kusababisha msongamano wa magari sana.
                              Wasamaria wema nao huwa hawakosi kufika kwenye tukio.
                                   Toyota hiace aliyogongwa kwa nyuma ikionekana kwenye picha.
 Mmiliki wa Toyota Hiace bwana John Atanas akiongea na redio Living water fm live kuelezea tukio lilivyotokea.

Wednesday, October 03, 2012

Moto Wateketeza Nyumba Morogoro



Wakazi wa mtaa wa Mto, Manispaa ya Morogoro wakimzuia Aziz Salh ambaye ni mmiliki wa nyumba iliyoungua jana mjini humo, alipotaka kuingia ndani ili kuokoa mali zake wakati moto ukiendelea jana machana.
Nyumba ya mkazi wa Manispaa ya Morogoro ilipokuwa ikiungua huku wakazi wakiangalia. 

Picha na Juma Mtanda

UP DATE AJALI MBALIZI MBEYA...WATU KUMI WAFARIKI KUFIKIA SASA

We found an exclusive and fun way to meet new people online: Twoo.com.


MBUNGE VITI MAALAM MBEYA DR.MARY MWANJELWA AKIWA HOSPITlLI YA FISI BAADA YA KUPATA AJALI

HILI NDILO GARI ALILOKUWEMO MBUNGE MARY MWANJELWA LIMETEKETEA LOTE KWA MOTO



PICHA NA MBEYA YETU NA KALULUNGA BLOG