Wednesday, March 29, 2017

RC Makonda ahojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge



RC Makonda ahojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.

Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexandra Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya Kudharau Bunge.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akipokelewa katika Viwanja vya Bunge na Mkuu wa Kitengo cha Babari, Elimu na Mawasiliano Ndg. Owen Mwandumbya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge. Picha na Deonisius Simba - Bunge


Friday, March 24, 2017

Malkia wa Tembo Afunguka Mahakamani



Malkia wa Tembo Afunguka Mahakamani
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Anayedaiwa kuwa Malkia wa Meno ya Tembo Yang Feng Clan (66), amesema kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania ni hapa kazi tu lakini mbona Mahakamani hamna hiyo kazi tu.

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi, Clan ameuliza hayo mahakamani Leo wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Kabla Clan hajasema kitu, Wakili wa Serikali Nassoro Katuga ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo Leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini wakili anayeendesha anamajukumu mengine kikazi.

Baada ya kusikia hayo, mshtakiwa Clan alinyoosha mkono ndipo Hakimu Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo akamruhusu kusema naye akalamika, " tumekuja màhakamani mara nyingi, leo mara ya nne hamna kitu, Rais Magufuli alisema hapa kazi tu, hapa court iko wapi hiyo kazi tu" amesema Mshtakiwa Clan kwa kutumia kiswahili chake chenye lafudhi ya kichina.

Hakimu Shahidi amewataka mawakili wa Serikali kuleta mashahidi na kuwaambia kuwa wanataka kesi zote ziishe kwa wakayi.Katika kesi hiyo Clan anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara Salvius Matembo (39) na Manase Philemon (39).

Wanadaiwa kujihisisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya bilioni 5.4.

Wanadaiwa kati ya Januari Mosi 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali bila kibali.Katika kipindi hicho wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 zenye thamani ya Sh5.4 bilioni bila leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machine 20 na 30, mwaka huu.


Sunday, February 26, 2017

Rais Magufuli Atoa Mkwala Mzito Kwa Wanaojenga Bomba la Mafuta Kutoka Tanga Hadi Uganda..


Rais Magufuli Atoa Mkwala Mzito Kwa Wanaojenga Bomba la Mafuta Kutoka Tanga Hadi Uganda..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amesema hatavumilia uzembe wa aina yoyote katika ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Hoima nchini Uganda bali anataka ujenzi wa bomba hilo ufanywe katika hali inayotarajiwa ili wananchi wa Uganda na Tanzania wanufaike nalo.

Dr.Magufuli ametoa onyo hilo Ikulu jijini Dar es salaam  mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda uliofanyika mbele yake na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta museveni ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Aidha Rais DKt.magufuli amemweleza mgeni wake Rais Museveni kuwa Tanzania imeanza kujenga reli kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Mwanza kwa kiwango cha kisasa yaani Standard Gauge ambapo itakapofika mkoani Mwanza atajenga bandari kavu maalum kwa ajili ya kuhudumia wafanyabiashara wa Uganda pekee.

Naye Rais Museveni amesema nchi ya Uganda inaitambua Tanzania kama rafiki wa kweli na kwamba atashirikiana na Rais Dr.Magufuli katika nyanja zote lengo kuu likiwa ni kuwafanya watanzania na waganda waweze kuishi maisha bora zaidi ya hivi sasa.

Baadhi ya nyanja ambazo Tanzania na Uganda wamekubaliana ni kuimarisha biashara miongoni mwao,kushirikiana katika usafiri wa anga,mawaziri wa mambo ya nje kukutana mara kwa mara na kujadiliana jinsi ya kuboresha uhusiano baina ya mataifa.

Friday, February 24, 2017

BAADHI YA VIONGOZI WAKILA KIAPO CHA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.



BAADHI YA VIONGOZI WAKILA KIAPO CHA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia kulia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto).
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa.


Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO.


Thursday, February 16, 2017

MAJALIWA ATETA NA MBUNGE WA SIMANJIRO



MAJALIWA ATETA NA MBUNGE WA SIMANJIRO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Simanjiro, James Ole Milya kwenye Ikulu Ndogo ya Orkesimet wilayani Simanjiro Februari 16, 2017. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia kwaya ya Wamasai wa Simanjiro wakati alipowasili kwenye uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjairo mjini Orkesimet Februari 16, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa zana za asili za kabila la wamasai wakati aliposimikwa kuwa Mzee wa Simanjiro na kupewa jina la Ole Majaliwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro mji Orkesimet Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mjini Orkesimet Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Monday, February 13, 2017

Utalii wa Tanzania Saudi Arabia


Utalii wa Tanzania Saudi Arabia
Baaadhi ya watu mbalimbali wakitembelea banda la Tanzania, nchini Saudi Arabia, katika maonyesho ya utalii ya '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).Maonyesho ya utalii nchini Saudi Arabia yaipaisha Tanzania

Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia mwishoni mwa juma hili ulishiriki katika maonyesho ya Safari na Utalii yajulikanayo kama '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).

Maonyesho ya TPF 2017 ambayo hufanyika kila mwaka kwa uandalizi Al Awsat Expo chini ya uhisani wa Mwana Mfalme HRH Prince Dr. Seif al Islam bin Saud bin Abdulaziz, yamefanyika kwa mafanikio huku ubalozi wa Tanzania ukifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa Tanzania.

Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba maonesho hayo yalikuwa maalumu kwa wafanya maamuzi na viongozi wa asasi za utalii (decision makers and leaders and tourisma leaders) nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, mwenye suti nyeusi akizungumza jambo na wageni waliotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho hayo.

Alisema kwamba kuwa banda la Tanzania lilifanikiwa kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, hifadhi za taifa, maeneo ya kihistoria ya Zanzibar, kilwa na Bagamoyo.
Mazungumzo yakiendelea yakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Watu wakipata maneno juu ya utalii wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Karibuni Tanzania.
"Tunashukuru kwa kiasi kikubwa kushiriki katika maonyesho haya sambamba na Tanzania kutangaza vivutio vya utalii wan chi yetu, tukiamini kuwa ni fursa adhimu kwa nchi yetu.

"Tunaendelea na juhudi za kutangaza nchi yetu ya Tanzania sambamba na kuwaonyesha watu wa Saudi Arabia juu ya umuhimu wa kutembelea nchini kwetu ili kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utalii," Alisema.

Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, miadi na majadiliano kuhusu kukuza utalii (promotion of tourism) yalifanyika baina ya washiriki wa Tanzania na mawakala wa utalii (tour operators) na wa usafiri (travel agents).