Showing posts with label BANK-KCB. Show all posts
Showing posts with label BANK-KCB. Show all posts

Monday, September 24, 2012

Benki ya KCB Tanzania yasaidia vifaa vya mama na mtoto kwa hospitali za Temeke na Buguruni from MTAA KWA MTAA


 Matroni wa Haopitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, akitoa  ukaribisho kwa wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kupokea  msaada wa vifaa mbalimbali vya Hospitali ya Temeke na Buguruni
 Vilivyotolewa na Benki ya KCB Tanzania vikiwa na thaman ya shilingi  milioni 17,152,000.
 Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro,akisalimiana na wauguzi wa hospitali za Temeke na Buguruni wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali hizo wenye thamani ya shilingi milioni 17,152,000.
Wauguzi wa hospitali ya temeke wakifurahia msaada wa mashine ya  joto inayosaidia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya mda wake Njiti,  baada ya kukabidhiwa msaada na benki ya KCB.
Wafanyakazi wa benki ya KCB Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi wa  Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro, wakiwa katika picha ya  pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Temeke na Buguruni zote za  jijini Dar es Salaam, baada ya KCB kukabidhi Msaada wa vifaa  mbalimbali kwa hospitali hizo wenye thamani ya shilingi Milioni  17,152,000.
Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro,(kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke jijini  Dar es Salaam, DR.Amani Malima msaada wa Folding Screens  moja kati ya 3 zilizotolewa msaada na benki hiyo ikiwemo vitu  mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 11,152,000 ka ajili ya  hospitali hiyo. (Kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Temeke  James Magoti.
  Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura  Muro,(kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Buguruni  jijini Dar es Salaam, DR.Hawa Lesso msaada wa mashini ya joto  inayosaidia kutunzia motto aliyezaliwa kabla ya wakati wake (NJITI)  katika hafla iliyofanyika Hospitali ya Temeke, Benki ya KCB ilitoa  vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 17,152,000.  Wanaoshuhudia ni wauguzi wa ahaospitali ya Buguruni waliofika kupokea  msaada huo.
Mkurugenzi wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania Mama Zuhura Muro,(kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke jijini  Dar es Salaam, DR.Amani Malima,mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumulia
wakati wa hafla ya kukabidhiwa vitu mbalimbali kwa ajiri ya Hospitali  ya Temeke na Buguruni vyenye thamani ya shilingi Milioni  17.152.000.(katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Temeke James
 Magoti.
Benki ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto vyenye thamani ya shilingi 17,152,000/- kwa hospitali za Temeke na Buguruni zilizopo jijini Dar es Salaam Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Benki ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto vyenye thamani ya shilingi 17,152,000/- kwa hospitali za Temeke na Buguruni zilizopo jijini Dar es Salaam Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Mkurugenzi wa bodi ya benki hiyo Zuhura Muro alisema katika kuhadhimisha wiki ya jamii mwaka huu benki ya KCB imeamua kuelekeza misaada yake katika sekta ya afya “Wakati wa wiki ya jamii mwaka jana na juzi tulitoa madawati na vitabu kwa shule mbalimbali nchini. 

Mwaka huu tumechagua kusaidia sekta ya afya hasa kwa upande wa akinamama na watoto ili kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na uhaba wa vifaa muhimu hospitalini,” “Mkurugenzi huyo wa bodi alisema benki ya KCB inaatambua umuhimu wa afya ya mama na mtoto na ndiyo maana tumeona ni jambo zuri kuwekeza katika sekta ya afya. Nikiwa kama mama ninayo furaha kwa kuwa naamini msaada huu utaweza kuokoa maisha ya akina mama na watoto,” alieleza.

 Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke Amani Malima alisema kuwa hospitali yake imekuwa ikihudumia akina mama wengi kuliko uwezo wake kutokana ukosefu wa vifaa. “Tunapokea akina mama wengi wanaokuja kujifungua zaidi ya uwezo wetu. Wengine huwa wanazaliwa wakiwa bado hawajatimia na hulazimika kuwapa rufaa ya kwenda hospitali nyingine kama Muhimbili kutokana na kutokuwa na vifaa. Tunaishukuru benki ya KCB kwani msaada huu utasaidia kuboresha hali,” alisema.

Naye mganga mfawidhi wa hospitali ya Buguruni Dr Hawa Lesso aliishukuru benki ya KCB na kusema kuwa utasaidia kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla wakiwa hawajatimia (pre mature). Watoto wanaozaliwa kabla ya kutimia wakati mwingine hupoteza maisha kabla ya kuwapa rufaa ya kwenda hospitali nyingine kutokana na ukosefu wa vifaa. Tunaishuru benki ya KCB kwani imesikiliza kilio chetu, Tunaomba taasisi nyingine za kifedha kuiga mfanio wa benki ya KCB. 

 Vifaa vilivyotolewa kwa hospitali ya Temeke ni pamoja na mashine moja ya joto kwa watoto waliozaliwa bila kutimia (Incubator), Folding screens 10, seti ya mashine ya hewa 3 (Oxygen flow meter) na sare za wauguzi pea 10 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 11,252,00/- Hospitali ya Buguruni ilipokea mashine moja ya joto kwa watoto waliozaliwa bila kutimia yenye thamani ya shilingi 5,900,000/-

Friday, September 21, 2012

KCB Bank Yatoa Msaada Hospitali Za Amana Na Mwananyamala


 Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye akimkabidhi Mganga msaidizi wa Hospitali ya Amana  DK.Shaany Mwaruka  msaada wa Kitanda cha kusaidia wajawazito kujifunguria (Delivery beds)  wkati wa hafla iliyofanyika katika Hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.Jumla ya Vitanda Vitano  na Mashine moja ya kutunzia watoto  ambao wanezaliwa  kabla ya muda wake vyote vikiwa na Thamani ya shilingi milioni 15,5. Vilitolewa na benki ya KCB.Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Asha Mahita, kulia ni Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo na Matroni wa Hospitali ya Amana Sr.Agnes Mwega.
 Mkuu wa Idaraya ya Uhazini wa beki ya KCB Tanzania Sam Kimath akimkabidhi msaada wa Mashuka 116  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Asha Mahita, na Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam, jumla ya vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 15,640,000. Vilitolewa msaada na benki hiyo kwa ajiri ya kusaidia hospitali hiyo ya Amana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye.
 Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB Christina Manyeye, akimkakabidhi  Mganga msaidizi wa Hospitali ya Mwananyamala DR.chrispian Kayola  Mashine ya Kutunzia joto ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda,(babyWarrmer Machine) yenye thamani ya shilingi Milioni 7.8.iliyotolewa na Benki ya KCB Kwa ajili ya kusaidia jamii inayopata huduma katika hospitali hiyo.wanao shuhudia ni Diwani wa kata ya Ilala Edson Fungo na Mganga msaidizi wa Hospitali ya Amana DR.Shaany Mwaruka. Hafla hiyo ilifanyika katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo Mauzo na Huduma kwa wateja na Jamii  wa benki ya KCB  Tanzania ,Christina Manyeye, akiwa amemshika mmoja wa watoto wenye umri wa siku moja waliozaliwa katika wodi ya wazazi ya Amana jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea waodi hiyo, baada ya kutoa msaada wa Mashuka 116 na Mashine ya joto ya kutunzia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wake  ( Baby Warmer Mashine) Vitanda Vitano vya kujifungulia akina mama wajawazito vvyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 15.640.000.Vilivyotolewa na Benki ya KCB Tanzania.


Na Mwandishi Wetu
 
Benki ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa vifaa  kwa wodi ya akina mama wajawazito vyenye thamani ya shilingi milioni 15,640,000 kwa hospitali  ya  Amana katika uzinduzi wake wa   wiki ya jamii
Akizungumza katika hafla fupi ya mabidhiano ya vifaa hivyo hivyo yaliyofanyika hospitalini hapo,  Mkuu wa kitengo cha masoko na jamii wa benki ya KCB Christine Manyenye  alisema  Msaada huo uanalenga kupunguza vifo vya aikina mama na watoto Manyenye  alisema kuwa, Benki ya KCB inatambua umuhimu wa  afya ya mama na motto na ndiyo maana iliona ni jambo zuri kuelekeza msaada huo muhimu kwakundi hilo Kila mwaka huwa tunaadhimisha wiki ya jamii kwa kutoa misaada kwa jamii. Kwa kawaida tunaangalia sehemu yenye kuhitaji sana msaada na kutoa mchango  sehemu hiyo. Kwa mfano tumegundua kuwa hospitali zetu haswa hizi zinazohudumia watu wenye kipato cha chini zina matatizo mengi na ndiyo maana leo tumekuja kutoa mchango hapa Amana,Alisema  "Ni matumaini yetu kuwa, vifaa hivi vilivyotolewa na Benki ya KCB vitachangia kwa kiasi kuboresha utoaji huduma kwa akina mama na watoto na hivyo kujenga taifa lenye afya na nguvu," aliongeza.
Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo  Docta Shani Mwaruka aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa utasidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kutokana na kupatiwa vifaa Hali za hospitali zetu hizi za serikali siyo nzuri sana kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, hakika tuahitaji msaada ili tuweze kutoa huduma bora na ndiyo maana tunatoa shukrani za pekee kwa benki ya KCB," alisema Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashine ya joto kwa watoto wachanga waliozaliwa bila kutimia 1, vitanga vya kujifungulia 5, vifaa vya kusaidia wakati wa akina mama kujifungua 10, mashuka 116, drums 20 na Cord clamp 100

MWANANYAMALA
 
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, jana imepokea msaada wa mashine ya joto kwa watoto waiozaliwa bila kutimia (baby warmer )  yenye thamani ya shilingi 7,850,000 kutoka katika Benki ya KCB Tanzania Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo Christine Manyenye  alisema msaada huo umetolewa baada ya kubaini uwezo mdogo wa hospitali za umma kuhudumia watoto wanaozaliwa bila kutima (pre mature) kutokana njha ukosefu wa vifaa , Kabla ya kufukia uamuzi wa kutoa msaada huu tulichunguza na kugundua kuwa huduma kwa watoto walizaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa bado si nzuri kutokana na ukosefu wa vifaa. Tuliona ni jambo zuri kueleza msaada wetu kwa kundi hili" alisema Manyeye alisema kuwa benki ya KCB imekuwa ikielekeza zaidi misaada yake kwenye makundi yenye mahitaji  makubwa na yenye uchache wa rasilimali za kutatua matatizo yake .
Mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali hiyo  Mwananyamala Docta Chrispian Kayolai aliishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema kuwa utasidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kwa watoto wanauzaliwa kabla ya muda wao Tunachangamoto nyingi ambazo tunakutana nazo wakati wa kutoa huduma na haswa kwa ajili ya vitendea kazi. Msaaada huu tulioupokea leo utasaidia sana kuboresha huduma na tuna kila sabau ya kuishukuru sana benki ya KCB," alisema Kwa mujibu wa Manyenye, katika kuadhimisha wiki ya jamii hospitali za KCM Moshi, Mwembeladu Zanzibar, Morogoro na Mount Meru ya Arusha itanufaika na misaada itakayogharimu shilingi milioni 79,040,000/-

Friday, August 17, 2012

Lowassa Awataka Viongozi Wa Morogoro Kushughulikia Tatizo La Uchomaji Moto Misitu

  Mh.Lowassa akiangalia madawati yaliyokabidhiwa kwa shule hiyo na benki ya KCB hivi karibuni.
Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi ujirani katika eneo la wafungaji wa jamii ya wamasai kata ya mkundi wilaya ya Morogoro alikokwenda kukagua na kukabidhi harambe za wafugaji hao kwa ajili ya ujenzi wa shule yao hiyo Waziri mkuu mstaafu mh Edward Lowassa ameuomba uongozi wa mkoa wa Morogoro kulishughulikia tatizo la uchomaji moto misitu.
 Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akikabidhiwa kibuyu na mama wa kimasai kata ya Mkundi wilaya ya Morogoro.

Akizungumza mapema leo kwenye kijiji cha Kiegea mjini Morogoro,Mh.Lowassa  ametoa wito huo alipokuwa akikabidhi michango ya harambee ya wafugaji wa jamii ya  Wamasai,kusaidia ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo.Mh Lowassa alialikwa kufanya kazi hiyo akiwa ni kiongozi wa jamii ya wamasai nchini.

Mh.Lowassa pia aligusia suala la baadhi ya wanchi kuwa na tabia ya kuchoma moto misitu hovyo hasa mkoa wa Morogoro,hali inayopelekea uharibifu mkubwa wa Mazingira,Lowassa amebainisha kuwa kila anapopita mkoani morogoro amekuwa akishuhudia misitu ikichomwa moto,hali iliyokuwa ikimhudhunisha sana.

''Nimekuwa nikishuhudia maeneo kadhaa ya misitu yakichomwa moto,kwa hivyo ndugu zanguni naomba tuachane na tabia hii pamoja na kuwa kilimo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku,lakini kwa njia hii tutaufanya mkoa huu wa Morogoro ugeuke jangwa'' alionya Lowassa na kuongeza kuwa iwapo mwanamuziki maarufu wa mkoa huo, Marehemu Mbaraka Mwinshehe angefufuka angesikitika sana.

''Mara nyingi nikikutana na hali hii,huwa naukumbuka wimbo wa Mbaraka Mwinshehe unaosema kuwa Morogoro maji yatiririka milimani, kama akifufuka atalia'' alisema Lowassa na kuuomba uongozi wa mkoa kushirikiana kwa pamoja kutafuta suluhisho la tatizo hilo ambalo limekuwa likikithiri siku hadi siku.''Mh DC wa Morogoro nawaombeni mtafute suluhisho la tatizo hili, tusipoangalia mkoa huu utakuwa jangwa''alisema.

Aidha Mh.Lowassa amesema kuwa suala la elimu ni muhimu zaidi kabla ya kilimo kwanza,akaongeza kuwa Elimu kabla baadaye kilimo kwanza.Mh Lowassa pia ametoa changamoto kwa wananchi wa kata mpya ya mkundi ya jamii hiyo ya wafugaji kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ya kata.

''Ni aibu kata hii kutokuwa na shule ya sekondari wakati kila kata nchini ina shule ya sekondari ,ambako hivi sasa angalau kuna usawa kwa watoto kugusa elimu ya sekondari'' alisema na kuongeza kuwa atakuwa tayari kuja kwenye kata hiyo Januari mwakani kuongoza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa sekondari.Mh.Lowassa ndiye aliyeongoza operesheni ya ujenzi wa shule za kata kote nchini wakati alipokuwa waziri mkuu.

''Niko tayari kuja January kuongoza harambe ya kuchangisha fedha, ni aibu kwakweli sijafurahishwa na hali yenu hapa mnatakiwa nyinyi wenyewe msimame kidete kujiletea maendeleo, njooni Monduli mjifunze jinsi wafugaji wenzenu walivyoweza kutumia mifugo yao kujenga shule na nyumba za waalimu'' alisema Lowassa.

Mh.Lowassa amemtaka kila mfugaji kutoa ng'ombe au mbuzi mmoja kwa ajili ya kuchangia elimu kwenye kata yao na kumuomba mkuu wa wilaya kutumia sheria zilizopo kumkamata na kumtia ndani yeyote atakayekaidi wito huo.

Mh Lowassa alichangia mabati 500 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ya msingi ya Ujirani yenye wanafunzi 414 ,lakini yenye upungufu mkubwa wa Waalimu, wawili tu mmoja wa kuajiriwa na mwingine wa kujitolea.

Katika harambee ya wananchi wa eneo hilo walichanga ng'ombe watano kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo, idadi ambayo mh Lowassa aliipinga,akidai kuwa ni Wanachi hao wana idadi kubwa ya mifugo hivyo walipaswa  kujitolea zaidi.