Showing posts with label Kumbukumbu. Show all posts
Showing posts with label Kumbukumbu. Show all posts

Friday, July 04, 2014

Mazishi ya Mwanahabari Nguli nchini, Mzee Nkwabi Ng’wanakilala



Mazishi ya Mwanahabari Nguli nchini, Mzee Nkwabi Ng'wanakilala
Mwanahabari wa Reuters nchini Bw. Fumbuka Ng'wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake, Lugendo  (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, Marehemu Mwl. Nkwabi Ng'wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwa ajili mazishi. 
Mwl. Ng'wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. PICHA ZOTE/JOHN BADI
Mzee Nkwabi Ng'wanakilala enzi za uhai wake.
Ndugu, jamaa na waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng'wanakilala kutoka kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba.
Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani Kibamba.
Mkurugenzi Msaidizi  wa Idara ya Habari MAELEZO  BW. Raphael Hokororo  (kati) akiwa na wadau wa habari waliokuwepo mazishini


Thursday, July 03, 2014

JK aomboleza kifo cha Nkwabi Ng’wanakilala


JK aomboleza kifo cha Nkwabi Ng'wanakilala
Nkwabi-Ng'wanakilala
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha mwandishi wa habari mkongwe na mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Bwana Nkwabi Ng'wanakilala.
Bwana Ng'wanakilala ambaye alifariki dunia mwishoni mwa wiki kwenye Hospitali ya Rufani ya Bugando mjini Mwanza kwa matatizo ya figo na tumbo, alizikwa  Jumatatu, Julai Mosi, 2014, nyumbani kwake Kibamba, Dar es Salaam.
Katika salamu ambazo amemtumia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais Kikwete amesema: "Kifo hiki kimelinyang'anya taifa letu mmoja wa wanataaluma wa habari mahiri sana na mtumishi hodari wa umma ambaye alithibitisha sifa hizo katika nafasi zote alizozishikilia. Tasnia ya habari imepoteza kiongozi hodari."
Ameongeza Rais Kikwete: "Alithibitisha sifa hizo kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Idara ya Habari, kwenye Ukurugenzi wa Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD) na kwenye Ukurugenzi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA). 

Aidha, marehemu alithibitisha vipaji vyake siyo kwenye uandishi wa habari tu bali hata kwenye uandishi wa vitabu, utafiti na uhadhiri, shughuli ambayo ameifanya hadi mauti yalipomfika."
"Naungana na wanafamilia, wanajumuia ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustine na wanataaluma wa tasnia yote ya habari nchini kuomboleza kifo cha Bwana Ng'wanakilala. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema roho ya Marehemu Nkwabi Ng'wanakilala. Amina."


Sunday, June 29, 2014

Kumbukumbu



Kumbukumbu
Tarehe kama ya leo ya maka 2013 mpendwa wetu Anna Ntamubano Gwitaba uliitwa na Bwana maana yeye alikupenda zaidi na tayari amekuandalia taji zuri kwa ajili ya Ufalme wake .
Wewe ulikuwa moja ya maua mazuri yaliyopandwa katika bustani ya Bwana na wakati ulipochanua na kuvutia Bwana alikuchuma na kukuweka mahali pazuri mno. 
Daima unakumbukwa na familia yako wakiwemo watoto wako (Adam, Irene, Edgar na Kelvin) na baba yao, mama yako mpendwa (Bibi Naomi), dada zako, kaka zako, watoto wote uliowalea, wajukuu, mawifi, mashemeji, wajomba, mashangazi, wakwe, marafiki, wafanyakazi wenzako na majirani wote. 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, 
Jina lake lihimidiwe
AMINA


Thursday, November 15, 2012

Kumbukumbu




Askofu Stephen Mwakasyuka (1933-2008)

Leo tarehe 15/11/2012 imetimu miaka minne tangu tulipoondokewa na Baba yetu mpendwa Askofu Stepen Mwakasyuka. Wakati anaondoka tuliumia mno na wengine kujiona kuwa na hatia ya kushindwa kufanya kila lililowezekana kuokoa maisha yake.

Tukiwa bado katika kipindi cha uchungu mkubwa, wakaondoka waliokuwa wakitufariji wakiwemo akina John Samwel Mwakasungura, Tulinagwe Mbangula, Jimmy David Ngonya, Kyomba Mwaipopo, na hivi karibuni Jimmy Mwabwagilo, Ashery Mwasandube, Amon Mwakatobe na Spendi Mwalisatile. Katika hili tumejifunza na kuamini kuwa ni kweli hapa duniani sote tu wapitaji.

Sisi tuliobaki katika Familia akina Ezeline, Phoebe, Florence, Jossey, Tungibwaga, Mponjoli, Atuganile, Frida, Salome, Gwakisa, Christian na Lazaro, tunazidi kuliwazwa na kufarijiwa na Hazina tuliyonayo ya Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wapendwa waliopo, tukiamini kwamba iko siku sote tutaja onana Paradiso.

Wafilipi 4:6

Tuesday, October 16, 2012

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu,  Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16, kushiriki katika shughu za msiba huo na kutoa heshima za mwisho wakati wa shughuli ya  kuaga mwili wa marehemu huyo aliyeuawa hivi karibuni jijini Mwanza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo  ya msiba wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16, kushiriki katika shughu za msiba huo na kutoa heshima za mwisho wakati wa shughuli ya  kuaga mwili wa marehemu huyo aliyeuawa hivi karibuni jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16, kushiriki katika shughu za msiba huo na kutoa heshima za mwisho wakati wa shughuli ya  kuaga mwili wa marehemu huyo aliyeuawa hivi karibuni jijini Mwanza. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Marehemu Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Barlow (52)Kuaagwa Jumanne(Leo)saa tano asubuhi katika kanisa la Katoliki lililoko Ukonga, jijini Dar es salaam.


Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Marehemu Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Barlow (52)
-- 
Mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Marehemu Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Barlow (52) ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, utaagwa Jumanne saa tano asubuhi katika kanisa la Katoliki lililoko Ukonga, jijini Dar es salaam.

 Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya maandalizi ya mazishi na kuthibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Advera Senso, Mwili Marehemu utawasili siku ya Jumatatu jioni ukitokea mwanza.

 Siku ya Jumanne mwili wa marehemu utafikishwa nyumbani kwake Ukonga kabla ya kupelekwa katika kanisa la Katoliki Ukonga kwa shughuli za ibada na kutoa heshima za mwisho.

 Aliendelea kusema kuwa viongozi mbalimbali wa Serikali, Maofisa wa waandamizi wa Polisi, Askari na wananchi watatoa heshima zao za mwisho  katika kanisa la hilo.

 Aliongeza kuwa baada ya ibada na shughuli ya kuaga kukamilika, mwili wa marehemu utasafilishwa kuelekea nyumbani kwao kilema, Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatano mchana kwa taratibu zote za kidini na baadae kuhitimishwa kwa kufuata taratibu za kijeshi.

 Marehemu kamanda Barlow alizaliwa katika kijiji cha Kyou Wilaya ya Moshi vijijini, Mkoani Kilimanjaro mwaka 1960, baada ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 1974 katika shule ya msingi Lombetha, alijiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Maua Seminary na baadae kujiunga kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondary Milambo na kuhitiku mwaka 1981.

 Baaada ya kumaliza elimu ya sekondari, marehemu kamanda Barlow alilitumikia taifa katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Operesheni Imarisha katika kikosi cha Mafinga  JKT, Mkoani Iringa.

 Mwaka 1982, Marehemu alijiunga na Chuo cha mafunzo cha Polisi Moshi (CCP) kwa ajili ya kusomea mafunzo ya awali ya sheria ya Uhamiaji na baadae kupangiwa kufanya kazi mpakani mkoani Mtwara akiwa kama Mkuu wa kituo cha Uhamiaji.
 Marehemu kamanda Barlow aliajiriwa  na Jeshi la Polisi baada ya kumaliza shahada ya kwanza ya utawala  kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam  kwa kuomba kazi katika Idara ya Polisi mwaka 1987 katika ngazi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi.

 Kutokana na uadilifu wake katika kazi, Marehemu aliweza kuaminiwa na viongozi wake na kupandishwa vyeo mbalimbali mpaka kufikia ngazi ya Cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi, cheo ambacho kilimuwezesha kupewa madaraka ya kuwa Kamanda wa Polisi Mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora na Mwanza.

 Kabla ya kufikia ngazi aliyokuwanayo, marehemu aliwahi kuaminiwa na kushika nyazifa mbalimbali akiwa kama Mkuu wa Upelelezi Wilaya (OC-CID), Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) na Mkuu Upelelezi Mkoa (RCO) na hatimaye kupata wadhifa wa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa. Marehemu Kamanda Barlow hadi umauti unamkuta alikua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na atakumbukwa kwa juhuda kwa juhudi zake za kupambana na kudhibiti uhalifu.



Na 
Tamimu Adam- Jeshi la Polisi


Monday, October 15, 2012

KAMANDA BARLOW AAGWA NYAMAGANA LEO


 Afande George Msangi akiongoza ratiba za kumuaga aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Ballow aliyeuawa usiku wa kuamkia jumamosi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na Hotel ya Tai Five.
 Msafara wa magari ya kuleta mwili wa marehemu Liberatus Ballow yakiingia katika uwanja wa Nyamagana ili viongozi na wananchi mbalimbali wapate kuuaga mwili huo.

                                       Magari yakiingia kwa uwanja wa Nyamagana..
 Maaskari walioteuliwa kubeba mwili wa marehemu Liberatus Ballow wakiwa wamejipanga vyema ili mwili uweze kutolewa ndani ya gari ili uwekwe sehemu nzuri ambayo kila mtu anaweza kuuaga vizuri.
                                     Hapa wakiushusha kutoka ndani ya gari ili waweze kuubeba.
            Safari ya kuelekea sehemu maalum iliyopangwa kwa ajili ya mwili wa marehemu ilianza hiviii..
                                          Maaskari wakiwa sawa kutekeleza jukumu lao..
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Everest Ndikillo akienda kuuaga mwili wa marehemu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow katika uwanja wa Nyamagana leo.
 Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakisimama kwa dakika chache kuupa heshima mwili wa marehemu kamanda Liberatus Ballow.
             Baadhi ya Maafisa ya Jeshi la Polisi wakionekana katika flash ya Blogu yako ya Fpluss Blog.
                Afisa Usalama wa Taifa Meja Jacob Mutashi mwenye suti nyeusi kulia akionekana pichani.
                     Mwili wa Marehemu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow.
 Mwandishi Peter Fabian kutoka gazeti la Mtanzania akiweka picha vizuri ya marehemu kamanda Liberatus Ballow.
 Saluti kutoka kwa Maafisa wa Polisi walizamu kwa Marehemu Kamanda wa Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow wakitoa heshima za mwisho.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga akiweka saini katika daftari la maombolezo katika msiba wa marehemu kamanda Liberatus Ballow katika uwanja wa Nyamagana.
 Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Kaminishina Richard Manumba akisalimia na Mkuu wa Wilaya ya Magu Bi. Jackline Wana huku Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Bi. Rosemary Mwanyika akiwa mbele mwenye suti nyeusi.
 Ibada ya ya kumuaga mwili wa marehemu kamanda Liberatus Ballow kama ilivyoongoza na Watumishi wa Kanisa la Roman Katoliki maana kamanda alikuwa muumini wa kanisa hilo.
 Wakuu wa wilaya mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza na baadhi ya viongozi wa serikali, vyama vya kisiasa wakionekana katika picha wakiwa na majonzi makubwa kumpoteza kamanda Liberatus Ballow.
 Wananchi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Mwanza na nje ya Mkoa wa Mwanza wakionekana katika tukio la kuuaga mwili wa Kamanda Liberatus Ballow.
 Wanafamilia wa marehemu kamanda Liberatus Ballow wakiwa na majonzi makubwa sana katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao Liberatus Ballow.
 Maafisa wa Majeshi aina mbalimbali kutoka Tanzania wakionekana katika hafla la kuuaga mwili wa marehemu kamanda Liberatus Ballow.
            Mabanda ambayo watu wamekaa kwa utulivu wakiuaga mwili wa kamanda Liberatus Ballow.
Umati mkubwa watu wakiwa katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Ballow.