Showing posts with label Tangazo.. Show all posts
Showing posts with label Tangazo.. Show all posts

Sunday, June 08, 2014

WASANII 20 WALIOMO KATIKA TUZO ZA KORA WIKI HII - DIAMOND NDANI!


WASANII 20 WALIOMO KATIKA TUZO ZA KORA WIKI HII - DIAMOND NDANI!



Monday, May 12, 2014

NANI KUIBUKA NA MILIONI 20 KATIKA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014?






Wafuatao ni washiriki wa mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambao sasa wapo kijijini Maisha Plus wakiwania zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tzshs. Milioni 20.

MS 01: Elinuru M. Pallangyo - Arusha
MS 02: Dorothy D. Pallangyo - Arusha
MS 03: Leah D. Mnyambugwe - Dodoma
MS 06: Martina G. Chitete - Iringa
MS 08: Grace G. Mahumbuka - Kagera
MS 10: Zinaida J. Kijeri - Kigoma
MS 11: Upendo M. Msuya - Kilimanjaro
MS 12: Neema U. Kivugo - Manyara
MS 15: Elizabeth Simon - Morogoro
MS 16: Joyce N. Hassan - Mtwara
MS 17: Bahati Muriga - Mwanza
MS 18: Thereza Kitinga - Mwanza
MS 20: Santina Mapile - Njombe
MS 21: Mary A. Ndasi - Rukwa
MS 22: Fredina M. Said - Shinyanga
MS 23: Esther Kulwa - Simiyu
MS 24: Mary J. Mwanga - Singida
MS 25: Doricus M. Shumbi - Singida
MS 27: Kuruthum R. Mwengele - Tanga

Kumpigia kura mshiriki umpendae, andika namba yake mfano MS 00 kisha tuma kwenda +255689666662 au mtandaoni kupitia: http://voting.maishaplus.tv/index.php/voting/mamashujaa

Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake. INALIPA.



Thursday, November 08, 2012

TAMKO LA MKUU WA MKOA WA DODOMA KWA WATOA HUDUMA ZA USAFIRI




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehama Nchimbi (pichani) amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Makampuni ya usafirishaji abiria (mabasi) yanayoendelea kufanya shughuli ya kupakia na kushusha abiria kwenye maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma yasiyoruhusiwa na Mamlaka zinazohusika na badala yake kuagiza shughuli hizo zifanyike katika stendi ya muda iliyopo uwanja wa Maonesho ya Nane Nane Nzuguni.
Dr. Nchimbi amesema kuwa agizo hili linayahusu makampuni yale ambayo hayana vituo rasmi vinavyotambuliwa na kuruhusiwa kisheria na Mamlaka husika (H/M Dodoma) kuendesha shughuli hizo na badala yake shughuli hizo zinatakiwa kufanyika katika Stendi ya Muda iliyopo viwanja vya Nzuguni.
Katika hatua nyingine Dr. Nchimbi amepiga marufuku tabia ya Magari Makubwa ya mizigo kuweka vituo na kuegesha katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma yasiyo rasmi kufanya shughuli hiyo na yasiyoruhusiwa kisheria na Mamlaka husika na badala yake amewataka madereva wa magari hayo kuegesha katika eneo maalumu lililopo kizota lililoandaliwa na Manispaa ya Dodoma na CDA kwa ajili ya shughuli hiyo.

Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ambapo alisema amewaagiza Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya Uendelezaji Makao Makuu (CDA), Polisi – usalama barabarani, wenye makampuni ya usafirishaji na wadau wengine wote wanaohusika kusimamia na kutekeleza agizo hili.
Dr. Nchimbi alibainisha kuwa kwa sasa Mkoa wetu wa Dodoma kupitia Halmashauri ya Manispaa Dodoma na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu – CDA umebahatika kuingia klwenye mpango wa uboreshaji Majiji ambapo Mkoa wa Dodoma umepatiwa zaidi ya shilingi bilioni 30 ili kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara na vituo vya mabasi ya Mikoa na daladala.
Hivi sasa mradi wa uboreshaji kituo cha mabasi ya mikoani unaendelea na Mkataba unamtaka mkandarasi kumaliza kazi hiyo ifikapo mwezi Mei, 2013 lakini kwa kutambua umuhimu wa kituo hiko mkandarasi ameahidi kumaliza kazi hiyo ifikapo Aprili, 2013. Kutokana na ukarabati huo Mamlaka husika (Manispaa Dodoma) imehamishia shughuli zote zilizokuwa zikifanyika kituoni hapo kituo cha Muda Nzuguni na kupiga marufuku shughuli hizo kufanyika katikati ya mji agizo ambalo baadhi ya makampuni yanakiuka.
Kwa upande mwingine Dr. Nchimbi ameeleza kuwa madereva wa magari makubwa ya mizigo wanakiuka kuegesha magari yao eneo la kizota lililotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo badala yake wanaegesha kandokando ya baadhi ya barabara, kwenye mitaa mbalimbali, kwenye vituo vya kuuzia mafuta na kwenye maeneo yakuoshea magari ambapo baadhi yake siyo vituo rasmi.
Dr. Nchimbi amesema tabia hiyo inachangia uharibifu wa miundombinu, uchafuzi wa mazingira, haizingatii taratibu nzuri za mipangomiji na inapoteza mapato kwa mamlaka husika na hivyo inarudisha nyuma juhudi za wadau wengine wa maendeleo na hasa uongozi wa Mkoa wa Dodoma wa kuufanya Mji wa Dodoma kupata hadhi ya kuwa Jiji.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
DODOMA

Wednesday, November 07, 2012

INVITATION TO TCCIA TRAINING PROGRAMME ON





''TECHNOLOGICAL TRANSFER IN BUILDING INNOVATIVE ECONOMIES''
(2 DAYS TRAINING) Nov. 29th - 30th, 2012).
Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) in collaboration with Promoting International Collaboration (PIC-Israel) is hereby inviting the business community to attend the Advanced International training programme  in  collaborating on Entrepreneurship  which is expected to be held in Dar es Salaam on 29th - 30th November 2012.

The training programme aims at enabling SMEs entrepreneurs, Government Officials, Ministerial departments and Agencies Officials to obtain international opportunity, to familiarise with one another and lay the groundwork for collaborative activities in promoting entrepreneurship competence. The program shall help SME's to be more creative, efficient and self-confident in market innovation through information and communication technology applications (ICT).
Participants are requested to contribute TZS 100,000/- which will cover for two days conference facilities. (Venue, stationeries, breakfast, Snacks & lunch) and TCCIA is coordinating the training. Costs of transport and accommodation while in Dar Es Salaam will be borne by the participants.

We shall be delighted to receive confirmation of your participation by 10thNovember 2012.

For further information on the Training Program and any other inquiries please contact Ms. Anna Msonsa Email: anna.msonsa@tccia.com or Mr. Revocatus Kimario, Email: revocatus.kimario@tccia.comMobile:  0752374772

Thursday, November 01, 2012

Libeneke Jipya la Mihangaiko

Jiunge nasi kwenye Libeneke jipya la www.mihangaiko.com kwa kukuza biashara yako, kuangalia nafasi za ajira mbalimbali zinazotangazwa, kwako msanii huu ndio wakati wa kukuza biashara yako, pia kuna mambo mbalimbali tembelea www.mihangaiko.com

Pia kwako mdau mwenye habari mbalimbali waweza jumika nasi, ikiwa una blog yako wataka kuitangaza basi ni nafasi pekee ya kufanya hivyo. 

Wote Mnakaribishwa.

Kumbuka www.mihangaiko.com ni chaguo lako.

Sunday, October 21, 2012

Tahadhali kwa wanaotangaziwa kuuzwa kwa viwanja Ufukweni ! Kimbiji



Wanunuzi kabla hamjanunua viwanja hivyo tafadhalini sana kwanza wasiliana na ofisi ya serikali ya kijiji au ofisi ya katibu mtendaji Kimbiji,hili ujue uhalali wa umiliki wa muuzaji,pia mnashauriwa kuwasiliana na uongozi wa kijiji kimbiji,Diwani simu namba 0713768082, Mwenyekiti simu 0713846688 viongozi wa kijiji wanayajua vema maeneo na wamiliki halali wa maeneo haya.

Wenu watiifu

Tuesday, October 16, 2012

Dkt Ali Mohammed Shein Afanya Mabadiliko Katika Baraza La Mapinduzi




 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohammed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi.

 Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imesema katika mabadiliko hayo, Rais Dkt Shein amemteua Shawana Bukheti Hassan kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Rais Dkt Shein amefuta uteuzi wa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi,Mansoor Yussuf Himid. 

Katika uteuzi mwengine Dkt Shein amewateua Mtumwa Kheir Mbarak kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili na Mohammed Said Mohamed kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Katika hatua nyengine, Rais Dkt Shein amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makatibu Wakuu katika Wizara za Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati.

 Dkt. Juma Malik Akili ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano akichukua nafasi ya Dkt. Vuai Idd Lila atapangiwa kazi nyengine. Ali Khalil Mirza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati. 

Kabla ya uteuzi huo, Mirza alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Mwalimu Ali Mwalimu atapangiwa kazi nyengine. Taarifa ya Ikulu imesema pia Rais Dkt Shein amemteua Tahir M. Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Msanif Haji Mussa atapangiwa kazi nyengine. 

Uteuzi mwengine ni Mustafa Aboud Jumbe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Tahir M Abdulla ambaye amehamishiwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. 

Rais Dkt Shein ameteua CDR Julius Nalim Maziku kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kapteni Juma Abdulla Juma ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar hivi karibuni. 

Uteuzi mwengine ni Juma Ameir Hafidh ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais(Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo) ambaye amechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Abdi Khamis Faki aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar. 

Aidha, aliyepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ambaye anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Ali Khalil Mirza aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati. 

 Pia Rais Dk Shein amemteua Mussa Haji Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu uchumi Zanzibar. Uteuzi huo wote unaanza Oktoba 15 mwaka 2012. 

         Imetolewa na: Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzíbar leo tarehe 15/10/2012

Saturday, October 13, 2012

BAADHI YA WAUMINI WA KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA META WAMEFUNGA MILANGO YA KANISA HILO NA KUSABABISHA KUTOFANYIKA KWA IBAADA YA ASUBUHI YA UMOJA WA AKINA MAMA KWA KISINGIZIO CHA KUTOMTAKA MCHUNGAJI WA KANISA.



MOJA WA WAUMINI WA KANISA HILO ANAZIDI KUPIGILIA MISUMARI KANISA LISIFUNGULIWE


HILI NDILO KANISA LA MORAVIAN META

AKINA MAMA WA KIPANGA WAKIMBA NYIMBO ZA KUTOMTAKA MCHUNGAJI WAO


MAKAMU  MWENYEKITI ZAKARIA SICHONE, MCHUNGAJI WA USHIRIKA HUO NA MZEE WA KANISA HUYO 
NYUMA WAKIKATAA KUZUNGUMZIA SWALA HILO



Sakata hilo limetokea asubuhi ya jumatano ambapo waumini wa kanisa hilo walifika kwa lengo la kutaka kufanya ibaada ya umoja wa akina mama na kukuta milango imefungwa na makufuli mengine na kubandika  matangazo ya katika milango hiyo yaliyosomeka

 MLANGO UMEFUNGWA KWASABABU MCHUNGAJI HANA AMANI NA WAKKRISTO TAFADHALI USIFUNGUE MPAKA UONGOZI WA JUU UTAKAPO FIKA BY UTAWALA.

Mwandishi wa habari hii alikutana na makamu wa mwenyekiti ZAKARIA SICHONE,Mwenyekiti wa wilaya ya Meya mjini mch swila na mchungaji wa kanisa hilo Ambao walifika kanisani hapo kwa kusudi la kusikiliza tuhuma hizo hawakuwa tayari kuzungumzia mgogolo huo


Wednesday, October 03, 2012

RASHID MATUMLA KUVAANA NA MKENYA, MTWARA



Tamasha la kimataifa la ngumi litakalofanyika mkoani Mtwara katika ukumbi wa MAKONDE BEACH RESOLT .

Tamasha hilo litasimamiwa na ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA - TPBO, na maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na bondia Patrick Amote kutoka Kenya anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 23-10-2012 tayari kuanza safari ya kuelekea mkoani Mtwara tarehe 24 -10 -2012.

Thursday, September 27, 2012

UTEUZI WA POSTA MASTA MKUU WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Deos Khamis Hubert Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania.
 Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Septemba 26, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo,kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 21 Septemba, 2012.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
26 Septemba, 2012

Saturday, September 22, 2012

TANGAZO LA SEMINA KWA WAKAZI WA DODOMA




SEMINA YA KINABII KWA WACHUNGAJI NA WAUMINI WOTE WAISHIO DODOMA
MHUBIRI: BOB WATSON TOKA USA NA TIMU YAKE.
TAREHE: 8/11 MPAKA 10/11/2012 
MUDA: SAA NNE ASUBUHI MPAKA12 JIONI KILA SIKU
MAHALI: KATIKA KANISA LA HEMA LA UPAKO LILILOPO; MAILI MBILI,  HADO
WAANDALIZI; MCHUGAJI ISAYA GWAE AKISHIRIKIANA NA JUMUIYA YA WACHUNGAJI DODOMA.
WOTE MNAKARIBISHWA. 

ASANTENI

Wednesday, September 19, 2012

SEXIEST COMMERCIAL VIDEO EVER – XENERGY.


 

This sexy Xenergy commercial is still the most viewed of all videos about an energy drink on youtube. When it comes to brand and business promotions, some businesses play hard ball, they hit the nail right on the head. This advert is tight, you just check it out http://www.xyience.com/index.cfm?fa=products.beverages 

Friday, September 14, 2012

TAHADHARI DHIDI YA MVUA ZA OKTOBA 2012–DISEMBA, 2012



 
Kufuatia Utabiri wa Hali ya Hewa uliofanywa kwa pamoja na Mamlaka za Hali ya Hewa kwa nchi za Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, Mamlaka ya Hali ya Hewa - Tanzania imetoa taarifa kuhusu uwezekano wa nchi kupata mvua nyingi iliyo juu ya wastani. Hali hii ya kuwa na mvua nyingi inatabiriwa kuikumba nchi kwa kipindi cha Oktoba, 2012 hadi Disemba, 2012 na huenda ikaendelea zaidi.
 Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga). Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Septemba, 2012 katika mkoa wa Kagera na kaskazini mwa Kigoma na kuendelea kusambaa katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita na Simiyu katika wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2012. Kwa ujumla mvua hizo zinatarajiwa kuwa juu ya wastani katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Viktoria.
Ukanda wa Pwani ya Kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza ya mwezi wa Oktoba, 2012. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.
Nyanda za juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).  Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Oktoba, 2012 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.
Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa).
Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Oktoba, 2012 katika mkoa wa Kigoma na wiki ya pili ya mwezi Novemba katika mikoa ya Tabora, Rukwa na Katavi. Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika mikoa ya Rukwa na Kigoma. Aidha maeneo mengi ya mikoa ya Katavi na Tabora mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani.
Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma). Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Novemba na zinatarajiwa kuwa za juu
ya wastani.
Nyanda za juu Kusini Magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro): Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Novemba 2012 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika mkoa wa Njombe na kusini mwa mikoa ya Mbeya na Morogoro. Maeneo ya kaskazini mwa mikoa ya Mbeya na Iringa, mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani.
Maeneo ya Kusini na Pwani ya Kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara): Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba, 2012 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.

Kwa kuzingatia hali hii Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa tayari imetoa taarifa/elimu kwa umma kupitia kipindi cha“Tuambie” cha TBC 1 na kuelekeza taasisi na wadau mbalimbali kuchukua hatua za tahadhari. Mfumo wetu wa kukabiliana na maafa una Kamati za Maafa kwenye ngazi ya mkoa, wilaya hadi kijiji ambazo zina majukumu ya kusimamia masuala ya maafa katika maeneo yao. Kamati zilizoanishwa hapo juu pamoja na wadau wote mnakumbushwa kujiandaa kukabiliana na maafa endapo yatatokea. Katika jitihada za kujiandaa mnakumbushwa kuzingatia yafuatayo:-
1.   Kutekeleza mipango mbadala katika maeneo mliyobaini kuwa yana uwezekano mkubwa wa kukumbwa na mafuriko; kama vile kuhamisha wananchi maeneo ya mabonde kwenda sehemu salama na kurejesha mawasiliano endapo yataharibika.
2.   Kupatikana dawa muhimu za magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na madawa ya kusafisha maji ya kunywa (Water Guard Tablets).
3.   Kupatikana kwa dawa muhimu za mifugo kwani magonjwa miguu na midomo (FMD) na homa ya bonde la ufa (RVF) yana uwezekano mkubwa wa kutokea.
4.   Upatikanaji wa chakula cha kutosha. Aidha wananchi wahimizwe kuweka akiba ya chakula cha kutosha.
5.   Kutenga fedha za kukabiliana na maafa endapo yatatokea.
6.   Elimu kwa Umma itolewe kwa kuhusisha vyombo vyote vya mawasiliano na uongozi wa Vijiji na Mitaa.
7.   Kuchukua hatua za ziada kwa maeneo ambayo yana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na mmomonyoko wa ardhi.
8.   Kuainisha mitaro inayoweza kuingiza maji katika migodi ya wachimbaji wadogowadogo, na kuchukua tahadhari zinazostahili.
9.   Kuhakikisha kuwa mifereji na mitaro ya maji machafu  kwa maeneo ya Jiji/miji iko safi na wazi wakati wote kupitisha maji.
10.               Kuchimba au kukamilisha uchimbaji wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua.
11.  Maofisa Ugani - Kilimo kutoa ushauri kwa wakati kuhusu mazao ya kupanda na pia wafugaji kutumia nafasi kuvuna malisho ya kutosha yatakayotumika kipindi cha kiangazi .
12.  Kila ngazi kujiweka tayari kukabiliana na mafuriko ni muhimu kuunda timu za wataalam wa kukabiliana na athari zitakazotokea, majina yao yaainishwe na waelekezwe cha kufanya pindi hali ikiwa hivyo.
Ni matumaini yangu kuwa tukishirikiana katika kukabiliana na mvua nyingi pamoja na majanga yanayoambatana na mvua hizi, tunayo nafasi kubwa ya kujihakikishia usalama wa nchi yetu kutokana na majanga ya asili.

Nashukuru kwa ushirikiano wenu.
IMETOLEWA NA KATIBU MKUU, OFISI YA WAZIRI MKUU

Thursday, September 13, 2012

Vodacom Na Precision Air Waendesha Bahati Nasibu



 
 Meneja Mawasiliano wa shirika la ndege la Precision Annette Nkini  (wa pili toka kushoto), kimsisitiza jambo Sarah Nadhan Mwanjelele baada ya kumkabidhi tiketi ya kwenda Afrika Kusini aliyoipokea kwa niaba ya mume wake Lusako Mwanjejele aliyoshinda katika  bahati nasibu ya kampeni ya MOYO iliyoendeshwa  na wafanyakazi wa Idara ya Masoko ya Vodacom na Precision Air mapema mwaka huu,wanaoshuhudia kushoto ni Elizabeth Mtegwa na kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
 
 Meneja Mawasiliano wa shirika la ndege la Precision Annette Nkini (wa pili toka kushoto),akimkabidhi Sarah Nadhan Mwanjelele,tiketi ya kwenda Afrika Kusini aliyoipokea kwa niaba ya mume wake Lusako Mwanjejele aliyoshinda katika  bahati nasibu ya kampeni ya MOYO iliyoendeshwa  na wafanyakazi wa Idara ya Masoko ya Vodacom na Precision Air mapema mwaka huu kwa ajili ya matibabu ya wakina mama walioadhirika kwa ugonjwa wa fistula,wanaoshuhudia kushoto ni Elizabeth Mtegwa na kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.
 
 Meneja Mawasiliano wa shirika la ndege la Precision Annette Nkini (wa kwanza toka kushoto),akijadiliana na Sarah Nadhan Mwanjelele watatu toka kushoto kuhusu zawadi ya tiketi ya kwenda Afrika Kusini aliyoipokea kwa niaba ya mume wake Lusako Mwanjejele aliyoshinda katika  bahati nasibu ya kampeni ya MOYO iliyoendeshwa  na wafanyakazi wa Idara ya Masoko ya Vodacom na Precision Air mapema mwaka huu kwa ajili ya matibabu ya wakina mama walioadhirika kwa ugonjwa wa fistula,wanaoshuhudia wa pili toka kushoto ni Elizabeth Mtegwa, kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.
 
Baadhi ya washindi wa tiketi ya kwenda Afrika Kusini waliyoshinda katika  bahati nasibu ya kampeni ya MOYO iliyoendeshwa  na wafanyakazi wa Idara ya Masoko ya Vodacom na Precision Air mapema mwaka huu,wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Masoko wa shirika la ndege la Precision Linda Chiza wapili toka kushoto,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.

Wednesday, September 12, 2012

National and International Consultants Wanted


UN Women is building a roosters of international consultants in entrepreneurship and enterprise development, and national consultants fromKenya, Uganda, Tanzania, Ethiopia, Sudan and Southern Sudan with proven success in the following areas to support program design:

1.       Agriculture production, processing and marketing
2.       Entrepreneurship and enterprise development
3.       Value chain systems development
4.       Small and Medium Enterprises development and appropriate technology
5.       Industrial development
6.       Business management
7.       Development Economics and economic literacy

They are kindly seeking your assistance in circulating the link below and/ or collaborating with local UNDP at Country level to post the adverts on local networks or circulate with registry to reach wider pool of local applicants.


Short Course Announcement



 

                        UNIVERSITY OF DODOMA


DEPARTMENT OF STATISTICS SHORT COURSE ANNOUNCEMENT ON DATA PROCESSING AND ANALYSIS  (To be conducted in Dar es Salaam) 

The Department of Statistics, School of Mathematical Sciences is announcing a short course on “DATA PROCESSING AND ANALYSIS” that will be conducted on September 27 and 28 from 14: 00 – 18:00; September 29 - 30 from 09:30 – 17:00.

The training will cover: overview of data; data management using SPSS; data cleaning (missing values, outliers and normality); descriptive data analysis and interpretation. Participants are required to come with their laptops.

Objective of the training 

The objective of the training is to improve skills of researchers into different statistical techniques applied during data processing and analysis and hence practical interpretation of the result.
Target Group: Any interested person. 
Participation Fee: Tshs 250, 000/= (The amount paid will cover tuition fee, training materials, and certificate of attendance only). 
Mode of payment: All payments should be done through; Account Name: College of Natural and Mathematical Sciences; Account no: 0150221567000 – CRDB
Venue: National Institute of Transport (NIT) Payment deadline: September 21, 2012.

Mode of Registration: Send an email indicating your name after making payment using contact below. Come with bank deposit slip.
Contact person:
Josephat Peter

Training Coordinator
Mobiles: 0787288998 or 0718453773
E-mail: statistics.data.udom@gmail.com

Thursday, August 23, 2012

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YABADILI UTARATIBU WAKUTEUA WAJUMBE WA BODI



 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.

Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
Makumbusho ya Taifa
Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)

Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara,www.mnrt.go.tz 

Wednesday, August 22, 2012

Bibi Winfrida Beatrice Korosso ateuliwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria



 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
         
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Winfrida Beatrice Korosso kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Agosti 22, 2012 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Agosti 14, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Korosso alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mkurugenzi wa Mashtaka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Agosti, 2012