Showing posts with label Chukua Hatua. Show all posts
Showing posts with label Chukua Hatua. Show all posts

Saturday, June 11, 2011

CUF yafuta maandamano ya Juni 12, 2011!

Jana niliwapwni dondoo ya maandamano ya CUF, sasa leo kuna jipya kuhusiana na mandamano.

Chonde chonde usiandamane,maana mwenyekiti kasema, unataka kujua kasemaje? Endelea mwenyewe hapo


M/kiti Taifa wa chama cha CUF Mhe. Ibrahim Lipumba ametangaza kufuta maandamano yaliyopangwa na chama hicho kufanyika kesho.... Amesema uamuzi huo umekuja baada ya kuombwa na Mhe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda! Hivyo kesho hakutakuwa na maandamano hayo hadi siku yatakapotangazwa tena...
Chanzo: TBC 1
--

Friday, June 10, 2011

AZMA YA KUTOSITISHA MAAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI YANAYOFANYWA NA POLISI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

AZMA YA KUTOSITISHA MAAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI YANAYOFANYWA NA
POLISI

Imetolewa na Julius MtatiroNaibu Katibu Mkuu-Chama Cha Wananchi CUF –
Tanzania Bara10/6/2011Chama Cha wananchi CUF kinasisitiza kuwa
maandamano ya kupinga vitendo vya kinyama vya mauaji vinavyofanywa na
jeshi la polisi dhidi ya wananchi wasioikuwa na hatia nchini
yatakayofanyika tarehe 12/6/2011 yako palepale licha ya jeshi la
polisi kupinga kwa sababu zisizokuwa na mashiko wala mantiki ya
kikatiba.Kwa nini tutaandamana1. Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za
Binadamu la mwaka 1945, (The UN declaration of Human Rights of 1945)
ambalo Tanzania ikiwa ni mjumbe rasmi wa Umoja wa Mataifa
imeridhia,linatoa haki ya kuandamana ikiwa watu au chama kinataka
kuonesha hisia zake kwa jamii husika ni muhimu kwa watanzania wote.2.
Katiba yetu ya jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, ambayo tayari ina
viraka zaidi 14 inatoa haki kwa Raia wa Tanzania vikundi au taasisi
kutoa mawazo au hisia zao ibara ya 20 kifungu 13. CUF ni chama chama
siasa chenye kauli mbiu HAKI SAWA KWA WOTE, hivyo basi kitendo
walichofanya Polisi cha kufyatua risasi ni cha kinyama kilichokatisha
haki ya kuishi ya mtanzania mwenzetu huko wilayani Urambo Mkoa wa
Tabora, CUF, tutaandamana ili kupinga kitindo hicho na vitendo kama
hivyo. Tutaandamana ili polisi wote waliohusika katika mauaji ya
wananchi wasio na hatia wafikishwe mahakamani na wachukuliwe hatua za
kisheria.4. Moja ya malengo ya kuanzishwa kwa chama cha wananchi (CUF)
ni pamoja na kuwaunganisha watanzania, kukataa aina yoyote ya uonevu,
ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi, na uadhalilishaji wa kisiasa au wa
kiuchumi. Hivyo basi CUF kama chama chenye usajili wa kudumu nchini,
kilichosajiliwa kutokana na malengo yake, kinacho haki na wajibu wa
kuungana na wananchi kupinga unyanyasaji na uonevu unaofanywa na jeshi
la polisi nchini.5.Kifungu cha 43(1) cha sheria za Polisi na Polisi
Wasaidizi sura ya 322 kama ilivyoandikwa upya mwaka 2002 kinaeleza
kuwa waandamanaji wanapaswa kutoa taarifa ya maandamano kwa ofisa wa
Polisi masaa 48 kabla ya maandamano. Aidha kifungu cha 43 (3)
kinaeleza kuwa Ofisa wa polisi hawezi kukataza maandamano chini ya
kifungu cha 43(2); isipokuwa iwapo atajiridhisha kuwa mkusanyiko huo
utasababisha uvunjifu wa amani au kuathiri usalama wa nchi au kuvunja
utulivu wa nchi au kutumika kwa malengo yasiyo halali. Kwa manti hiyo
kukataza maandamano bila Polisi kusema maandamano ya CUF yatavuruga
vipi amani ni uzembe wa dhahiri na kamwe chama hakiwezi kusitisha
maandamano kwa kutekeleza uzembe.6.Hoja ya Kova kwamba maandamanao ya
CUF kesi za Urambo na Nyamongo zimeshafikishwa mahakamani kwa hatua za
kisheria haina mashiko ya kwani kesi zote hizo si za mauaji bali ni
kesi kukuasanyika kinyume na sheria.HIVYO CUF TUTAANDAMANA NA KUJARIBU
KUTUZUIA NI KUVUNJA AMANI YA NCHI.NGUVU ZA POLISI KUTUZUIA ZITUMIKE
KUTULINDA.

WOTE TUNAWAALIKA KATIKA MAANDAMANO.

HAKI SAWA KWA WOTE.
Julius Mtatiro,
10/06/2011

Soma Uongo wa kutisha Wa Serikali Yako JUU ya Badget!!



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA

Simu Na. 026 2322761-5
Fax Na. (255) 026 2324218
E-Mail: poctz@parliment.go.tz

(Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (Kiongozi wa Upinzani)
Unapojibu tafadhali taja:



OFISI YA BUNGE
S.L.P. 941 DODOMA




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
9 Juni, 2011
"Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa"
Kutokana na Hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkullo (Mb), aliyoitoa jana bungeni Dodoma tarehe 08/06/2011, kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kambi ya Upinzani tumeshtushwa na upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa na serikali kwa lengo la kuwajengea matumaini hewa wananchi kuwa watapata nafuu ya maisha kupitia bajeti hiyo wakati hali halisi haipo hivyo.

Yafuatayo ni baadhi tu ya maeneo ya waziwazi ambayo serikali ya CCM kupitia kwa Waziri wake Mhe. Mkulo iliamua kuupotosha umma wa Watanzania kwa makusudi kama ifuatavyo;

1. Wakati Waziri akitaja kuwa kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo ni kumaliza tatizo la Umeme na hivyo kutamka kwamba ametenga shilingi 537 Bilioni, , upembuzi uliofanywa na Kambi yetu ya Upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa jumla ya kiasi cha shilingi 402,402,071,000 milioni kwa mujibu wa fungu la 58. Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya Matumizi kawaida shilingi 76,953,934,000 milioni na kwa upande wa bajeti ya Maendeleo zimetengwa shilingi 325,448,137,000. Shilingi Bilioni 325 zilizotengwa katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza. Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaonekana katika Bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme.

2. Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa. Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.

3. Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012 itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu "kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija (uk.53)", ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 13 % ya bajeti yote ya serikali kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama "Personnel allowances (non discretionary na In-kind"). Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa.

4. Wakati Waziri akisema kuwa ili kuthibiti matumizi watapunguza posho mbalimbali, kwenye hotuba yake uk.66, waziri amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato SURA 332 na anasema kwenye (i) "kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali" . Hii inaonyesha dhahiri kuwa kauli ya Kufuta au kupunguza posho ilitolewa na Serikali ili kupumbaza wananchi lakini haina udhati.

5. Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imewaongezea mzigo mkubwa sana wananchi na haswa wajasiriamali wadogo na vijana ambao wamejiajiri ama kuajiriwa kwenye biashara ya usafiri na usafirishaji. Tunasema hivyo, kwa sababu serikali katika bajeti vyake rasmi vya bajeti imeamua kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati mtu akiwa anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee), kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000. Lakini Waziri Mkulo katika Hotuba yake aliyoitoa jana ukurasa 74, alitamka kuwa wataongeza kiwango cha faini hadi kufikia shilingi 50,000. Ni dhahiri kuwa kauli ya waziri ya kusema faini itafikia 50,000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300,000, hivyo alilenga kuuhadaa umma na kuupotosha.

6. Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya Bajeti kulipa Madeni na Kulipana Posho (Asilimia 27 – 14% kulipa madeni na 13% kulipa Posho mbalimbali).

7. Kambi ya Upinzani itawasilisha Bungeni Bajeti Mbadala siku ya Jumatano tarehe 15.6.2011, saa tano asubuhi ambayo itakuwa inajali masilahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza Uchumi wa Vijijini (rural growth) na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta Posho mbalimbali.

Imetolewa leo, Mjini Dodoma, na



Zitto Zuberi Kabwe
Waziri Kivuli wa Fedha
Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni
--

Wednesday, April 27, 2011

CAG aibua uozo wa ajira Tanapa

CAG aibua uozo wa ajira Tanapa

James Magai
WATUMISHI 181 wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), wameajiriwa kinyume cha taratibu za ajira.

Ajira hizo zisizofuata taratibu ndani ya shirika hilo, zimebanika wakati wa ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.

Kwa mujibu wa Utouh, Tanapa ni mfano wa mashirika mbalimbali ya   umma yanayotoa ajira za watumishi kwenye sekta mbalimbali kinyume cha taratibu.

Utouh anabainisha kwenye uchambuzi wa usimamizi wa raslimali watu katika mashirika mbalimbali ya umma, kuna mashirika ambayo ajira za kazi zilifanywa bila kufuata taratibu za uwazi.

Anabainisha taratibu hizo zinazokiukwa na mashirika hayo wakati wa ajira kuwa, ni kutangaza nafasi zilizo wazi, jambo ambalo linawanyima watu wengi nafasi ya kushindana.

“Mfano mzuri ulibainika Tanapa ambapo menejimenti ilitangaza nafasi 19 za kazi kuwa uwazi, lakini kufikia mwisho mwa zoezi la uajiri, wafanyakazi 32 zaidi waliajiriwa;
“Uchambuzi zaidi ulibaini kuwa wafanyakazi walioajiriwa na Tanapa mwaka huu wa ukaguzi bila nafasi zake kutangazwa ni 181” anasema Utouh.

Licha ya ukiukaji taratibu za ajira katika mashirika ya umma, CAG amebainisha ukiukaji mkubwa wa sheria na haki za wafanyakazi.Miongoni mwa kasoro hizo za ukiukaji sheria na haki za wafanyakazi uliobainishwa, ni kuchelewa kulipa mishahara na malipo ya mishahara chini ya kima cha chini

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, uchambuzi wa usimamizi wa raslimali watu juu ya suala la ulipaji mishahara, baadhi ya mashirika ya umma hayatoi umuhimu wa kutosha kuhusu haki ya wafanyakazi kulipwa mishahara.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya mashirika yamekuwa hawalipwi mishahara yao kwa wakati, huku mengine yakiwalipa wafanyakazi wao chini ya kima cha chini cha mshahara.

Shirika lingine ambalo halikuwalipa wafanyakazi wake mishahara, ni Tamko Kibaha ukaguzi huo umebaini kuwa wafanyakazi saba wa zamani, hawakulipwa mishahara yao ya jumla ya Sh2.6 millioni.

Pia, Nyanza Glass Works Limited na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), kuwa yanawalipa wafanyakazi wake mishahara chini ya kima cha chini cha mishahara.

Source:http://www.mwananchi.co.tz/biashara/-/11398-cag-aibu-uozo-wa-ajira-tanapa

Wednesday, April 20, 2011

Tafakuri yangu ya leo ni "Kila unajionae amesimama angalia usianguke"

Tafakuri Ya Leo.

Kuna wakati sisi binadamu huwa tunajisahu sana kana kwamba tutaishi milele hapa dunani. Tunasahau kuwa ipo siku tutaondoka duniani na kupoteza historia yeto kama upepo.

Wakati mwingine tunatumia ubabe wetu katika maamuzi yetu na kudidimiza wengine ili matakwa yetu yaweze kukubaliwa hata kama ni mabaya. Tunajitahidi kufunika hata yale mema ya wenzetu kwa sababu tu tunataka tuonekane sie ndio wema.
Tafakuri yangu ya leo ni "Kila unajionae amesimama angalia usianguke"

Ni dhahili umewahi kuusikia huo usemi na leo sio mara yako ya kwanza kuusikia huo msemo. Tunapokuwa tumepewa baadhi ya vitu, fahari, utajiri, madaraka ni dhahili kuwa ni mambo ya dhamana tu hayo. Nakuuliza kuna mtu alizaliwa kuwa na madaraka? Au kuna mtu alizaliwa na utajiri?

Mbona unanikodolea jicho sana kwenye hii tafakuri yangu kama umepigwa na butwaa? Tafadhali elewa kuwa wewe umepewa kila kitu kwa dhamana. Swali langu ni kuwa unatumiaje hayo madaraka yako? Huo utajiri wako? Hivyo vitu vyako? Na mengineyo? Unajua ninachomaanisha maana hata dhamira yako inakusuta kwa jinsi unavyotumia madaraka yako vibaya, unawanyanyasa wenzako kwa sababu ya cheo chako. Unawaona kama ni uchafu mbele yako. Why? Kwani haujui aliekupa wewe ndio
alieninyima mie? Kwani haujui unaweza kunyang'anywa hicho cheo chako? Wako wapi akina Hosni Mubaraka? Wapi Ben ALi? Wapi akina Mabutu na wengine kama hao? Je walipewa heshima gani na jamaii baada ya kuondoka kwenye madaraka yao? Ni lazima ujue kuwa kila kitu hapa duniani ni cha muda tu. Naomba niishie hapa huku ukiendelea kutafakari na Tafakuri yetu ya Kila ajionnae amasimama angalia asianguke maana mwisho wake ni mbaya sana.

Asomae na afahamu,

Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia gemmstore@gmail.com

Asante nakutakia siku njema.

Tuesday, September 21, 2010

Maisha ya Kitanzania

Hapo sio zizi la ng'ombe wala kuku. Hiyo ni sehemu ambayo binadamu anaweka ubavu wake pia anaishi na jamaa zake.

Nchi imejaaliwa kuwa na viongozi walio na busara za utafuta madaraka tu. Ewe Diwani unafikiria nini juu ya wananchi wako? Kama sio kupiga picha kama hizo na kupeleka sehemu ili upate msaada baadaye unajua unakopeleka hiyo misaada.

Mwaka 2010 Watanzania tuamke tena tusichague bora viongozi bali Viongozi Bora. Tumeongozwa miaka zaidi ya 40 na chama fulani hivi lakini maisha ya Mtanzania bado duni......


Chukua Hatua....