Friday, June 10, 2011

AZMA YA KUTOSITISHA MAAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI YANAYOFANYWA NA POLISI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

AZMA YA KUTOSITISHA MAAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI YANAYOFANYWA NA
POLISI

Imetolewa na Julius MtatiroNaibu Katibu Mkuu-Chama Cha Wananchi CUF –
Tanzania Bara10/6/2011Chama Cha wananchi CUF kinasisitiza kuwa
maandamano ya kupinga vitendo vya kinyama vya mauaji vinavyofanywa na
jeshi la polisi dhidi ya wananchi wasioikuwa na hatia nchini
yatakayofanyika tarehe 12/6/2011 yako palepale licha ya jeshi la
polisi kupinga kwa sababu zisizokuwa na mashiko wala mantiki ya
kikatiba.Kwa nini tutaandamana1. Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za
Binadamu la mwaka 1945, (The UN declaration of Human Rights of 1945)
ambalo Tanzania ikiwa ni mjumbe rasmi wa Umoja wa Mataifa
imeridhia,linatoa haki ya kuandamana ikiwa watu au chama kinataka
kuonesha hisia zake kwa jamii husika ni muhimu kwa watanzania wote.2.
Katiba yetu ya jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, ambayo tayari ina
viraka zaidi 14 inatoa haki kwa Raia wa Tanzania vikundi au taasisi
kutoa mawazo au hisia zao ibara ya 20 kifungu 13. CUF ni chama chama
siasa chenye kauli mbiu HAKI SAWA KWA WOTE, hivyo basi kitendo
walichofanya Polisi cha kufyatua risasi ni cha kinyama kilichokatisha
haki ya kuishi ya mtanzania mwenzetu huko wilayani Urambo Mkoa wa
Tabora, CUF, tutaandamana ili kupinga kitindo hicho na vitendo kama
hivyo. Tutaandamana ili polisi wote waliohusika katika mauaji ya
wananchi wasio na hatia wafikishwe mahakamani na wachukuliwe hatua za
kisheria.4. Moja ya malengo ya kuanzishwa kwa chama cha wananchi (CUF)
ni pamoja na kuwaunganisha watanzania, kukataa aina yoyote ya uonevu,
ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi, na uadhalilishaji wa kisiasa au wa
kiuchumi. Hivyo basi CUF kama chama chenye usajili wa kudumu nchini,
kilichosajiliwa kutokana na malengo yake, kinacho haki na wajibu wa
kuungana na wananchi kupinga unyanyasaji na uonevu unaofanywa na jeshi
la polisi nchini.5.Kifungu cha 43(1) cha sheria za Polisi na Polisi
Wasaidizi sura ya 322 kama ilivyoandikwa upya mwaka 2002 kinaeleza
kuwa waandamanaji wanapaswa kutoa taarifa ya maandamano kwa ofisa wa
Polisi masaa 48 kabla ya maandamano. Aidha kifungu cha 43 (3)
kinaeleza kuwa Ofisa wa polisi hawezi kukataza maandamano chini ya
kifungu cha 43(2); isipokuwa iwapo atajiridhisha kuwa mkusanyiko huo
utasababisha uvunjifu wa amani au kuathiri usalama wa nchi au kuvunja
utulivu wa nchi au kutumika kwa malengo yasiyo halali. Kwa manti hiyo
kukataza maandamano bila Polisi kusema maandamano ya CUF yatavuruga
vipi amani ni uzembe wa dhahiri na kamwe chama hakiwezi kusitisha
maandamano kwa kutekeleza uzembe.6.Hoja ya Kova kwamba maandamanao ya
CUF kesi za Urambo na Nyamongo zimeshafikishwa mahakamani kwa hatua za
kisheria haina mashiko ya kwani kesi zote hizo si za mauaji bali ni
kesi kukuasanyika kinyume na sheria.HIVYO CUF TUTAANDAMANA NA KUJARIBU
KUTUZUIA NI KUVUNJA AMANI YA NCHI.NGUVU ZA POLISI KUTUZUIA ZITUMIKE
KUTULINDA.

WOTE TUNAWAALIKA KATIKA MAANDAMANO.

HAKI SAWA KWA WOTE.
Julius Mtatiro,
10/06/2011