Saturday, April 04, 2015

FAMILIA KUTAMBUA MIILI YA WALIOUAWA KENYA


FAMILIA KUTAMBUA MIILI YA WALIOUAWA KENYA
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa
Familia za wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu kazkazini mashariki mwa Kenya zimeenda katika eneo la mkasa ili kuitambua miili ya waliouawa.


Zaidi ya watu 140 waliuawa katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Al shabaab mjini Garissa siku ya alhamisi ambapo wapiganaji hao waliwatenganisha wanafunzi hao kwa misingi ya kidini kabla ya kuwaua wanafunzi wa kikristo.
Wakati huohuo mamlaka nchini Kenya imetoa mabasi ili kuwasafirisha wanafunzi walionusurika hadi makwao,huku miili ya waliofariki ikisafirishwa hadi mjini Nairobi.
Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamoud,amesema kuwa Somalia na Kenya lazima ziimarishe ushirikiano wao dhidi ya Ugaidi baada ya shambulizi hilo.