Kuku bora
Lakini hata mizinga ya kisasa kama hii kutoka SIDO mkoani Dodoma imekuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wengi wa kijiji cha Ilindi. Medani Ibiga (35) akiwa na wanakikundi wenzake wa Kilimo Nyuki - Rose Sudayi na Ellen Sangula.

Ng'ombe hawa wa Medani Ibiga wametokana na ufugaji wa nyuki. Jamaa ana mizinga 175 ya nyuki na mwaka huu tu amevuna lita 281!

Ujamaa ni ushirika mkubwa kwa Wagogo iwe kiangazi au masika. Hapa wakazi hawa wa Nghambi wakimenya karanga kwa ajili ya mbegu. Dodoma inasifika kwa kilimo cha karanga ingawa alizeti na ufuta ni mazao yanayokuja kasi kwa sasa.

