Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano.
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi akimueleza Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mikakati ya ofisi hiyo ya kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika vitengo cha mawasiliano.
Afisa Habari wa Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Kassim Nyaki (kulia) akieleza kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mafanikio ya kitengo cha mawasiliano cha ofisi hiyo katika kutoa taarifa kwa umma ambapo alisema hadi sasa tovuti yao ina zaidi ya watu Elfu 8 wanaotembelea kwa siku.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia mwenye Kaunda Suti) akiwaeleza baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma. Katikati ni Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila.
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kujionea utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano serikalini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa ofisi hiyo Bw. Gerard Mwanilwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia) akisisitiza kwa Maafisa Habari wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu utoaji wa taarifa kwa umma kwa wakati. Kushoto ni Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bi. Evelyne Thomas. Picha na Fatma Salum-MAELEZO