Wednesday, April 20, 2011

Tafakuri yangu ya leo ni "Kila unajionae amesimama angalia usianguke"

Tafakuri Ya Leo.

Kuna wakati sisi binadamu huwa tunajisahu sana kana kwamba tutaishi milele hapa dunani. Tunasahau kuwa ipo siku tutaondoka duniani na kupoteza historia yeto kama upepo.

Wakati mwingine tunatumia ubabe wetu katika maamuzi yetu na kudidimiza wengine ili matakwa yetu yaweze kukubaliwa hata kama ni mabaya. Tunajitahidi kufunika hata yale mema ya wenzetu kwa sababu tu tunataka tuonekane sie ndio wema.
Tafakuri yangu ya leo ni "Kila unajionae amesimama angalia usianguke"

Ni dhahili umewahi kuusikia huo usemi na leo sio mara yako ya kwanza kuusikia huo msemo. Tunapokuwa tumepewa baadhi ya vitu, fahari, utajiri, madaraka ni dhahili kuwa ni mambo ya dhamana tu hayo. Nakuuliza kuna mtu alizaliwa kuwa na madaraka? Au kuna mtu alizaliwa na utajiri?

Mbona unanikodolea jicho sana kwenye hii tafakuri yangu kama umepigwa na butwaa? Tafadhali elewa kuwa wewe umepewa kila kitu kwa dhamana. Swali langu ni kuwa unatumiaje hayo madaraka yako? Huo utajiri wako? Hivyo vitu vyako? Na mengineyo? Unajua ninachomaanisha maana hata dhamira yako inakusuta kwa jinsi unavyotumia madaraka yako vibaya, unawanyanyasa wenzako kwa sababu ya cheo chako. Unawaona kama ni uchafu mbele yako. Why? Kwani haujui aliekupa wewe ndio
alieninyima mie? Kwani haujui unaweza kunyang'anywa hicho cheo chako? Wako wapi akina Hosni Mubaraka? Wapi Ben ALi? Wapi akina Mabutu na wengine kama hao? Je walipewa heshima gani na jamaii baada ya kuondoka kwenye madaraka yao? Ni lazima ujue kuwa kila kitu hapa duniani ni cha muda tu. Naomba niishie hapa huku ukiendelea kutafakari na Tafakuri yetu ya Kila ajionnae amasimama angalia asianguke maana mwisho wake ni mbaya sana.

Asomae na afahamu,

Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia gemmstore@gmail.com

Asante nakutakia siku njema.