Wednesday, August 22, 2012

Bibi Winfrida Beatrice Korosso ateuliwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria



 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
         
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Winfrida Beatrice Korosso kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Agosti 22, 2012 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Agosti 14, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Korosso alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mkurugenzi wa Mashtaka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Agosti, 2012