Friday, March 24, 2017

Malkia wa Tembo Afunguka Mahakamani



Malkia wa Tembo Afunguka Mahakamani
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Anayedaiwa kuwa Malkia wa Meno ya Tembo Yang Feng Clan (66), amesema kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania ni hapa kazi tu lakini mbona Mahakamani hamna hiyo kazi tu.

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi, Clan ameuliza hayo mahakamani Leo wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Kabla Clan hajasema kitu, Wakili wa Serikali Nassoro Katuga ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo Leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini wakili anayeendesha anamajukumu mengine kikazi.

Baada ya kusikia hayo, mshtakiwa Clan alinyoosha mkono ndipo Hakimu Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo akamruhusu kusema naye akalamika, " tumekuja màhakamani mara nyingi, leo mara ya nne hamna kitu, Rais Magufuli alisema hapa kazi tu, hapa court iko wapi hiyo kazi tu" amesema Mshtakiwa Clan kwa kutumia kiswahili chake chenye lafudhi ya kichina.

Hakimu Shahidi amewataka mawakili wa Serikali kuleta mashahidi na kuwaambia kuwa wanataka kesi zote ziishe kwa wakayi.Katika kesi hiyo Clan anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara Salvius Matembo (39) na Manase Philemon (39).

Wanadaiwa kujihisisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya bilioni 5.4.

Wanadaiwa kati ya Januari Mosi 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali bila kibali.Katika kipindi hicho wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 zenye thamani ya Sh5.4 bilioni bila leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machine 20 na 30, mwaka huu.