Baada ya miaka 30 ya kuishi bila yandoa, Rais mpya wa Malawi, Profesa
Peter Mutharika, hatimaye amefunga pingu za maisha na mbunge wa zamani
wa Jimbo la Balaka, Gertrude Maseko.Kabla ya ndoa yao iliyofungwa jana
kwenye Kanisa la Mtakatifu Michaelna Malaika Wote jijini Blantyre,
Maseko aliwahi kuolewa, lakini ndoa yake ilivunjika miaka kumi
iliyopita; na mwaka jana mume wake huyo, ambaye pia alizaa naye mtoto
mmoja, anayesoma Chuo Kikuu, aliaga dunia.Aidha, kwa Rais Mutharika,
Profesa aliyebobea katika masuala ya sheria, aliwahi kumwoa
Christophine G. Mutharika, raia wa Visiwa vya Carribean. Alibahatika
kuzaa naye watoto watatu, Mahopela ambaye ni wa kiume na mabinti,
Monique na Moyenda, ambao wote ni wanasheria mahiri nchini Marekani
kwa sasa.Hata hivyo, Mutharika alimpoteza mkewe huyo kwa ugonjwa wa
kansa mwaka 1990, hivyo kumfanya asioe kwa muda mrefu, huku akijikita
zaidi katika kazi zake za uwakili kwa zaidi ya miaka 40 nchini
Marekani.Katika ndoa iliyoongozwa na Padri Rapson Chikwenzule, Rais
Mutharika hakuwa na mbwembwe nyingi kama mkuu wa nchi na alitarajiwa
kuendelea na sherehe katika shamba la familia ya Rais huyo lililopo
Ndata Wilaya ya Thloyo, Kusini mwa Malawi.Ukiondoa makundi ya marafiki
na wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya nchi, miongoni mwa
walioshuhudia wawili hao wakioanani mabinti wa Mutharika, ambao
walikanyaga ardhi ya Malawi kwa mara ya kwanza baada ya baba yao
kuutwaa urais wa Malawi Juni Mosi, mwaka huu.Kaka yao ambaye pia ni
profesa katika moja ya vyuo vikuu vya Marekani, hakuhudhuria na
hajawahi kukanyaga nchi ya Malawi.Hata hivyo, ujio wa watoto hao
umemaliza uvumi, uliokuwa umeenezwa wakati wa kampeni za urais, kwamba
Mutharika si mwanamume aliyekamilika na hajawahi kuwa na
watoto.Akizungumza siku moja kabla ya harusi hiyo, Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Harusi ya Rais Mutharika na Maseko, Saulos
Chilima ambaye ni Makamu wa Rais wa Malawi, alisema harusi ya `bosi'
wake ilitarajiwa kugharimu dola za Kimarekani 95,000 (Sh milioni
155).Alisisitiza kuwa fedha hizo si za Serikali, bali ni michango
kutoka kwa pande mbili za maharusi, hasa ndugu na marafiki."Kila kitu
kimekwenda sawa, nashukuru dhamira ya kutogusa fedha za Serikali
imetimia. Michango imetoka kwa ndugu na marafiki. Kuna watu waliotaka
kutumia mwanya wa harusi kujiweka karibu na Rais au wasaidizi wake,
hawa 'tuliwafungia vioo'. Hatukutaka baadaye waje kutusumbua wakitaka
kusaidia kufanikisha mambo yao kwa kigezocha ukaribu na Rais na hasa
kwa kushiriki kikamilifu katika harusi yake. Hilo tumesema hapana,
hatutaki rushwa na tutapambana kwa dhati na rushwa na wala rushwa,"
alisema Chilima.Mutharika (74) ambaye ni Rais wa Tano wa Malawi,
anakuwa Rais wa tatu kuoa akiwa madarakani. Wa kwanza kuoa akiwa
Ikulu, alikuwa Bakili Muluzi ambaye baada ya kuachana na Anne, alimwoa
Shanil Dzimbili.Baadaye, Bingu wa Mutharika, Rais wa Tatu ambaye ni
kaka wa Rais wa sasa, yeye alimwoa Callista Mutharika baada ya kufiwa
na mkewe, Ethel.Marais wengine waliowahi kuitawala Malawi ni Dk
Hastings Kamuzu Banda ambaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Malawi na Joyce
Banda, Rais wa Nne ambaye ameangushwa na Profesa Mutharika katika
uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, mwaka huu