Utabakia Stevie? Hodgson ana matumaini ya kutompoteza Gerrard
ROY Hodgson atajaribu kumshawishi Steven Gerrard ili aendelee kucheza soka la kimataifa mpaka 2016.
Nyota huyo amebaki njia panda juu ya hatima ya soka lake la kimataifa kutokana na matokeo mabaya ya kombe la dunia, lakini bado anahitajika na klabu yake ya Liverpool itakayoshiriki michuano ya UEFA msimu ujao.
Japokuwa Gerrard, 34, ameshindwa kutamba kombe la dunia, thamani yake na uzoefu wake unahitaji katika kikosi cha England na Hodgson anatamani kuona anaendelea kucheza licha ya vijana wengu kuchipukia kwasasa.
Frank Lampard anajiandaa kustaafu soka la kimataifa, kwahiyo Gerrard atabaki mchezaji pekee mkongwe na England haitaki kumpoteza kwasababu anawaunganisha vijana katika kikosi hicho.
Hata hivyo, Gerrard ataifikiria klabu yake ambayo ina mechi ngumu msimu ujao baada ya kufuzu UEFA.
Gerrard amesema atafanya maamuzi baada ya kuzungumza na marafiki, familia na kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers baada ya kombe la dunia.
Mawazo Rodgers yatakuwa muhimu zaidi na inaonekana kocha wa Liverpool na madaktari wa timu watapenda kumpa mapumziko Gerrard baada ya kombe la dunia.
Hata kama mwenyekiti wa FA , Greg Dyke amemhakikishia kazi Hodgson mpaka 2016 licha ya kuchemsha kombe la dunia, mechi ya mwisho dhidi ya Costa Rica itakuwa muhimu sana na kama England itapoteza, kocha huyo atakuwa katika mazingira mabaya.
Gerrard akiwatazama wachezaji wa Uruguay walipokuwa wanashangilia bao la pili na la ushindi.