Diwani aliyesimama Bi. Twilumba Wapalila enzi za uhai wake akiendelea na majukumu yake kama mwakilishi wa wananchi.
Diwani wa kata ya Lupembe wilayani Njombe Bi Twilumba Wapalila, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam alikokuwa akipata matibabu katika hospitali ya Muhimbili.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika zilizopatikana kutoka kwa viongozi kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wamesema kuwa hii leo watalazimika kufupisha kikao kutokana na msiba huo.
Aidha Baadhi ya wajumbe hao licha ya kuonekana kuwa na simanzi lakini pia wamebainisha kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Msiba huu ni wa pili kwa tarafa ya Lupembe na wa tatu kwa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe kufuatia siku chache zilizopita aliyekuwa diwani wa kata ya mfiliga kufariki ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutokea kwa msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama Hicho Marehemu Adam Msigwa.