Thursday, January 08, 2015

Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara wajiajiri kupitia mfuko wa mendeleo ya Vijana



Vijana Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara wajiajiri kupitia mfuko wa mendeleo ya Vijana
Kikosi kazimaalum kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wa kiongea na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ,Bw. Rashid Mohamed walimpotembelea leo ofisini kwake kwa ajili ya kufuatilia na kufanya tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-mikindani.
Wajumbe wa kikundi cha AMKENI kutoka Halmashauri ya manispaa ya Mtwara mikindani wakiwa katika majadiliano na wajumbe wa kikosi kazi maalum kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipowatembea leo ili kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa kwa kikundi hicho ilikujua nichangamoto gani wamekutana nazo ilikuboresha zaidi Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ,Bw.Yohana Ngao akiwa katika majadiliano na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini Bw.Oscar Ng'itu ilikujua maoni na changamoto wanazopata wana vikundi waliopata mkopo kupitia mfuko wamaendeleo yaVijana katika eneo lake.
4875:Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mtwara Vijijini Bw. Musa Said akimkaribisha ofisini kwake kiongozi wa kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Afisa uchumi mwandamizi Bw.Ngao Yohana walipotembelea wilaya iyo ilikufanya tathmini na ufuatiliaji wa mfuko wa Maendeleo ya Vijana.