Saturday, December 06, 2014

Wadau Amini Mture Robert Kisanga na Maria Deborah Kimalando wameremeta jioni hii



Wadau Amini Mture Robert Kisanga na Maria Deborah Kimalando wameremeta jioni hii
 Mdau Amini Mture Robert Kisanga na mai waifu wake Maria Deborah Kimalando wakiingia nyumbani Oysterbay jijini Dar es salaam jioni hii tayari kwa mnuso wa nguvu  baada ya kumeremeta katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM chapel)
Mdau Amini Mture Robert Kisanga na mai waifu wake Maria Deborah Kimalando wakikaribishwa kimila kwa kunywa Mbege mlangoni wakati wakingia nyumbani Oyster bay jijini Dar es salaam tayari kwa mnuso wa nguvu
Maharusi wakikata keki

Ni wakati wa Ndafu ambapo maharusi na mpambe wao na Jaji Robert Kisanga na Mama Kisanga wanajiandaa kulisha watoto wao 

Jaji Robert Kisanga na Mama Kisanga wakilishwa ndafu na mtoto wao Amini