Rais wa Jamhuri ya                Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete                anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa                barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika tarehe 1 Oktoba                2014. 
        Ufunguzi wa barabara ya                Mwenge-Tegeta wenye urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika                kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda                ya Kawe. 
        Upanuzi wa barabara ya                Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya                Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la                Dar es Salaam.
        Taarifa hii imetolewa                na;
        Kitengo cha Mawasiliano                Serikalini(GCU)
        Wizara ya Ujenzi 
        