Sunday, May 11, 2014

MOURINHO: ACHANA NA SUAREZ, MCHEZAJI BORA NI EDIN DZEKO …anafunga, anasaidia, hajirushi

 

The questionable one: Jose Mourinho has cast doubt over Liverpool's Luis Suarez's PFA and FWA awards

BOSS wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kwake yeye mchezaji bora msimu huu ni Edin Dzeko wa Manchseter City na sio Luis Suarez.

Kocha huyo anasema ni vizuri mchezaji bora akatoka kwenye timu itakayotwaa ubingwa ambapo akadai kama bingwa atakuwa Liverpool basi Steven Gerrard ndiye angestahili kuwa mchezaji bora. "Kama ni City (ambao wanahitaji pointi moja tu) Dzeko ndiye bora," alisema Mourinho.

Hivi karibuni, Suarez alitwaa tuzo mbili za uchezaji bora. Moja ikiwa ni ile ya kuchaguliwa na wachezaji wenzake wa kulipwa nay a pili ni kutoka kwa waandishi wa michezo.

Accolades: Suarez (right) won Player of the Year while Chelsea's Eden Hazard won the Young Player's award

Mourinho aliwahi kumtaja Suarez kama 'mfalme wa penalti' akimfananisha na bingwa wa kucheza sarakasi kwenye bwawa la kuogelea, kwamba ukimgusa kwenye box basi imekula kwako. Ni lazima ajirushe.

Kocha huyo anasema mchezaji bora hapatikani kwa kufunga tu, bali kwa magoli anayochangia, uungwana wake, anavyojiheshimu uwanjani na asiyejirusha.

"Dzeko alikuwa chaguo la tatu City, alifichwa, lakini alipohitajika katika wakati mgumu akaonyesha tofauti.

"Nadhani amefunga magoli 16 sambamba na kuchangia mengine kadhaa. Magoli 16 kutoka kwa mshambuliaji chaguo la tatu si jambo la kawaida," alifafanua Mourinho.

Kocha huyo anasema Suarez ni mchezaji mzuri na kwamba wanaochagua hawachagui kutoka miongoni mwa wachezaji wasio bora, lakini utukutu wake uwanjani na kujirusha kwake, kuna mpunguzia sifa ya kuwa mchezaji bora.