Tuesday, September 30, 2014

Hizi Ni Sababu Kuu Tano Kwanini Lowassa Anafaa Kuwa Rais 2015



Hizi Ni Sababu Kuu Tano Kwanini Lowassa Anafaa Kuwa Rais 2015
Maisha ya watanzania yamekua magumu mno,sasa sukari ipo juu ikiwa ardhi na mabonde kama ruvu mtibwa na kageara tunayo, umeme usio wa uhakika wakati gesi ya mtwara na RUBADA, madawa hakuna hospitalini, viongozi wanatuziba masikio kwa vizungumkuti vya ESCROW huku madawati hakuna shuleni, vitendo vya kihalifu vimejaa kila kona watu wakisaka ridhiki kwa nguvu, tumaini la katiba mpya ni kizunguzungu kiasi kutuacha wakiwa Zaidi sisi masikini wakitanzania, huku tukijengewa chuki na serikali na watawala kwa upenyo wakushuka uzalendo na kiasi cha kusema watu kuikimbia nchi kwa vijana ni kawaida kutafuta maisha ughaibuni na kusema hii nchi sasa si ile ya NYERERE bali ni ya watawala makatili mno. Lakini kwa muktadha ule ule wa kidemokrasia ambao hata rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya tatu Mh. Benjamin Mkapa aliyasema pale alipo chagiza kabla kuteuliwa Dk Jakaya Kikwete ndani ya CCM kuwa achaguliwe mgombea ambaye vijana na wapiga kura wengi wanamtaka kitu ambacho kilipelekea Dk. Kikwete kushinda kwa kishindo ndani ya chama na hata katika uchaguzi mkuu 2005. Sasa zifuatazo ni sababu ambazo Lowassa atapitishwa kugombea URAIS kwani wanachama na watanzania wanamuhitaji.


1.MRITHI SAHIHI WA MWL. NYERERE KATIKA VITA DHIDI YA UJINGA

Edward Lowassa ni mwana siasa Pekee ambae ndani ya CCM,anaefaham Vission ya Mwalimu Nyerere 1961 Mwalimu alitangaza maadui watatu (1)Ujinga (2)Maradhi (3) Umasikini. Mwalimu katika miaka yake 24 alisimamia swala moja Elimu ya Kujigetemea na baada ya kuondoka mfumo huu uliharibika,Ili kupambana na Adui hao Mwalimu alianzisha Vijiji vya Ujamaa,msingi hapa ili kuongea Uzalishaji,huduma ya afya na Shule, akajenga shule za msingi katika kila kijiji. Mwaka 2005 Edward Lowassa aliamua kufufua upya utekelezaji wa Dira ya Mwalimu nayo ni kuwekeza kwenye Elimu na Kupambana na maadui 3.Alisimamia Ujenzi wa Miundo Mbinu ya Elimu kila kata( sekondari),Kupanua elimu ya Chuo Kikuu, Kusukuma Ujenzi wa vyuo vya kada ya kati (Veta) ili kujenga Kada la kati ya wataalam wa Ufundi mbali mbali, Kupanua Vyuo vya Ualimu ili kuziba pengo la upungufu wa waalim,mambo haya hayana tofauti mapambano alianzisha Mwl Nyerere baada ya uhuru kupambana na maadui watatu. Elimu imekua Agenda kuu ya Edward lowassa,Anaamini katika hilo Jambo kuwa msingi wa kupambana na Umasikini,Elimu itasaidia Uzalishaji,Elimu Itapambana na Maradhi,Elimu Itaondoa Ujinga miongoni mwa Jamii yetu, hii ni sababu pekee itakayo ifanya CCM kumpitisha kurudisha taswira ya chama.


2. MAAMUZI MAGUMU NA MAKINI KATIKA UONGOZI

Kwa kipindi kirefu sasa ndani ya nchi yetu tuna tatizo la maamuzi katika utekelezaji wa sera za serikali, viongozi wamekuwa wazito mno kutekeleza makubaliano ya vikao vyao wakiogopana au hata rushwa kutawala miongoni mwao hivyo kushindwa kutekeleza maamuzi hayo. Edward Lowassa ni kiongozi ambaye kwa kipindi chake alicho kuwa madarakani ameonyesha kuwa si kigeugeu kwa maana ya kwamba mara zote ambazo baraza la mawaziri katika vikao vyake vya ndani walipo fika makubaliano yeye alitekeleza, Utekelezaji wa ujenzi wa chuo kikuu Dodoma. Taarifa za ndani za viongozi zilionyesha ugumu mno wa utekelezaji wa sera hii ya chama, Lowassa ilifikia hatua kuwaeleza viongozi mbalimbali waandamizi katika ngazi za maamuzi na utekelezaji kama yeyote anaona ujenzi wa chuo kile hauwezekani aandike barua ya kujiuzulu na akabidhi kwake ampatie Rais Dk.Jakaya Kikwete, kitu ambacho kiliongeza ujasiri wa utekelezaji wa sera na sasa tunaona watoto wa masikini wakipata elimu. Alivunja mkataba wa city water, mkataba ambao ulifanya serikali kushtakiwa lakini na hata kuleta nafuu katika upatikanaji wa majia ndani ya jiji la dar es salaam pia bila kusahau alivunja mkataba wa kimataifa katika usambazaji wa maji kanda ya ziwa kitu kilicho mfanya mpaka aogepeke na jumuia za kimataifa akiwa anatetea haki ya Mtazania kwa hakika ni mzalendo na mtu pekee ndani ya CCM hii ya DK. Jakaya na Kinana anaefaa kuipeleka dira ya taifa mbele.

3. MPAMBANAJI ALIAZIMIA KUFUTA UMASIKINI

Lowassa ni Mwana siasa Pekee ndani ya CCM ambae Anaamini UMASIKINI si sifaa bora kwa Mtanzania kujisifia,Umasikini si Sifa ya Kiongozi,Umasikini unaendana na udhalilishaji na Ujinga na Maradhi,ni mwana Siasa pekee ambae hasifiii umasikini kwani ni vita katika vita kuu za taifa hili tangu tunapata uhuru. Hii imekuwa hulka ya viongozi kadhaa hasa wabunge wetu hutuhadaa wakisema tuwape ridhaa ya kutuongoza kwa sababu wao ni masikini wenzetu, siasa sasa ya leo na kimataifa imebadilika mno tukiangalia mataifa makubwa hata madogo , viongozi ni wale wenye majibu sahihi katika kuufuta umasikini na si kujisifia kuwa wewe ni masikini tukupe ridhaa tena ridhaa ambayo utahakikisha kujinufaisha wewe na famia yako kwanza, na CCM sasa inataka kujenga uchumi imara uchumi ambao utafuta umasikini kwa kumpa Mtanzania Elimu, kuimarisha miundombinu na kufungua biashara tujifunze haya toka Kenya waungwana.Pia ni miongoni mwa sababu zinazo wavutia wana CCM kumpa ridhaa ya kupeperusha bendera.

4.ANAPENDWA NA WATANZANIA WOTE NA WANAMUHITAJI

Ni mtu ambaye ana mvuto mkubwa kwa watanzania na ana sifa ya kuwa muadilifu, mtendaji mzuri, mbunifu, huheshimu mawazo ya wengine, anaijua Tanzania, Mfuatiliaji wa kazi, anatabia ya kuwapa watu matumaini Mpambanaji (fighter) na anaheshimika kikanda na kimataifa. Ni Mtanzania pekee anayependwa na kukubalika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndani na nje ya chama chake. Ni mtu ambaye ana Aura ya aina yake na huleta matumaini unapokaa naye na kusikiliza.Ni kweli kabisa..Edward Lowassa (is the chosen one) kaatika uhai wa siasa ya chama chochote inatakiwa kuwa na gombea anaye uzika, anayekubalika na ambaye ni tumaini la mahitaji wananchi husika, Lowassa amekidhi vigezo vyote na hakika anafaa ndani ya CCM na ndio chaguo sahihi kama chama kinahitaji uhai wa muda mrefu.

5.KIONGOZI ALIYEPITIA MENGI NA ANAYEIJUA NCHI.

Lowassa ni kiongozi alie pitia mengi kama rais wa awamu ya pili alhajj Ali Hassan Mwinyi kufikia hatua ya kujiuzulu na kuwajibika kama kiongozi ambaye anjua fika maadili ya kiongozi wa umma, Lowassa amengia katika mfumo wa chama na serikali tangu mwaka 1977 ambapo imepita miaka Zaidi ya 30 akipambana na shida na mahitaji ya watanzania, mwenyekujua nini Watanzania wanahitaji, mtu ambaye amepitia mengi na kuwa na ufahamu wa kutosha wa serikali na chama chake kiasi cha kufanya kuwa kiongozi pekee kwa sasa anayekijua chama na serikali. Chama cha Mapinduzi kimekosa mtu mwenye sifa hizi mtu ambaye amepitia mikiki mikiki ya kina katika kuwatetea wananchi, kiongozi ambaye amepambana mpaka na mahafidhina ndani ya chama na kiongozi ambae si rahisi kumpelekesha, kiongozi huyu ameweza kuwa adui mkubwa wa mahafidhina kwa sababu hana si ya woga dhidi yao, hawafumbii macho na naweza sema huyu ni kama TAKUKURU kwa mahafidhina sababu hafumbii macho machafu.

MWISHO.
Watanzania tunahitaji kiongozi ambae atakuwa mrithi sahihi wa serikali ya awamu ya tatu, mtu ambae atatuongoza katika kukabiliana na mahitaji yetu yaani nini watu wa namanyere, uvinza nantumbo na Tanzania kwa ujumla nini wanataka, Mtu ambaye atakuwa msikivu na mpambanaji wa mahitaji yetu , nashauri wote kwa pamoja tuwajadili watu wanaoweza kuiongoza nchi yetu bila kejeli, matusi au woga na aina yeyote ya kufumbia macho machafu , kuukuza uzalendo ni pamoja na kuukana woga wa kivuli chako. MUNGU IBARIKI TANZANIA.