Tuesday, December 02, 2014

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA WATAALAMU WA UGAVI JIJINI ARUSHA



NAIBU WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA WATAALAMU WA UGAVI JIJINI ARUSHA
Mwandishi wetu,Arusha

WIZARA ya Fedha, imeitaka Bodi ya Wataalam wa Ugavi na Manunuzi nchni  (PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia thamani halisi ya fedha na kuwataka waajiri kuacha mara moja kuwaajiri watu wasio na sifa kufanya kazi hizo

Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua mkutano wa tano wa mwaka wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la Mikutano la AICC jijini Arusha ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao.

Amesema katika bajeti ya mwaka 2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni 20 kati ya hizo asilimia 65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee katika kudhibiti mapato ya serikali yasitumike vibaya.

Awali Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya mkutano huo "Thamani halisi ya fedha za Manunuzi" ikilenga kuhakikisha serikali inapata huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua uchumi wa nchi.

Amesema Bodi hiyo imezalisha wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali ambayo ni sawa na asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri watumishi wasiosajiliwa na Bodi hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa Siku mbili unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC, jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa Siku mbili wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)  unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC jijini Arusha.
Baadhi ya Maafisa Ugavi na Ununuzi wakisoma nyaraka mbalimbali za mkutano huo leo jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Clemence Tesha(kulia)akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima kwa hotuba nzuri.
Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wazi wa Fedha