Sunday, August 09, 2015

Jeshi la Polisi la kiri madhaifu yake katika utendaji kazi wake hapa Nchini.



Jeshi la Polisi la kiri madhaifu yake katika utendaji kazi wake hapa Nchini.
Serikali imekiri vitendo vya ufanikishwaji wa  mauji na uporaji wa silaha Katika vituo  mbalimbali vya polisi hapa nchini vinasababishwa na uzembe wa Askari polisi kutokua makini wawapo  kazini ,ulevi na kukaribisha watu Wasiowajua undani wao wakiwa wamebeba silaha.
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mh.pereira ame silima ameyasema hayo Wakati akifunga mafunzo ya awali ya jeshi la polisi na uhamiaji katika chuo Cha taaluma ya Polisi Moshi(mpa).
 
Amesema askari polisi wengi wamejisahau wawapo kazini kutokana na baadhi Yao kulala ,kutowatilia shaka watu wanaoingia katika vituo vya polisi ,kutofanya ukaguzi jambo ambalo linasababisha askari kuvamiwa na wahalifu Kiholela.
 
Kwa upande wake naibu mkuu wa jeshi la polisi nchini abrahaman kaniki Amepiga marufuku kwa askari wa jeshi la polisi kujihusisha na ushabiki,itikadi za kisiasa na wagombea wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Naye mkuu wa chuo cha taaluma ya polisi moshi(mpa)afande matanga mbushi Amesema jumla ya askari polisi na uhamiaji 126 kati 3610 waliojiunga na Jeshi hilo waliachishwa mafunzo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu Wa nidhamu.
 
Baadhi ya viongozi wa dini waliotoa nasaha zao wamesema tatizo la rushwa na Ukosefu wa maadili kwa watumishi wa uuma umesababisha wananchi wengi kukosa Haki zao zao za msingi.