Sunday, August 09, 2015

Rais Kikwete amewaaga rasmi wakulima na wakazi wa mikoa ya Kusini.



Rais Kikwete amewaaga rasmi wakulima na wakazi wa mikoa ya Kusini.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete amewaaga rasmi wakulima na wakazi wa mikoa ya kusini na kuongeza kuwa Tanzania ina hifadhi ya kutosha ya chakula na ziada na hakuna mtanzania atakayekufa kwa njaa na akawataka watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura October 25 na kutokubali kuhadaiwa na baadhi ya watu wanaozunguka mitaani kwa lengo la kuchukua vitambulisho vya wapiga kura.
Rais Kikwete ameitumia fursa ya kuwaaga wakulima na wakazi wa mikoa ya kusini kwa ujumla kwa kuelezea mafanikio na changamoto mbalimbali katika kipindi chake cha miaka kumi wakati wa kufunga maonesho ya wakulima maarufu kama nane nane yaliyofanyka kitaifa mkoani Lindi na kusisitiza kuwa Tanzania ina akiba ya kutosha ya chakula.
 
Aidh Dr.Kikwete mbali ya kukemea viongozi aliowaita ni mchwa wanaotafuna fedha za ushirika na kuwafaya wakulima kukosa masoko ya uhakika ya mazao yao na hivyo kuwafanya kuendelea kuwa masikini amezungumzia pia suala la mchakato wa kuelekea katika uchaguzi mkuu kwa kuwataka watanzania kujitokeza kupiga kura na kuhifadhi kadi zao za kupigia kura na kutokubali kurubuniwa na wajanja wa mitaani.
 
Rais Kikwete ametumia mtindo wa kipekee kwa kuwaita baadhi ya mawaziri jukwaani kueleza kile ambacho serikali yake haijakitekeleza ambapo waziri wa mambo ya nje Mh.Bernard Membe amesema mahusiano baina ya Tanzania na nchi nyingine ni mazuri na kwamba Tanzania haina mpango wa kuingia katika vita na nchi yeyote na badala yake hitilafu zozote za  kidiplomasia zitatuliwa kwa njia ya kidiplomasia.
 
Katika matukio mengine rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete amezindu rasmi benki ya maendeleo ya kilimo,kuzindua mradi wa  maji mkoani lindi pamoja na ujenzi wa nyumba ya mfano za walimu wenye lemgo la kumaliza tatizo la nyumba za walimu ambapo pia Dr.Magufuli amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi katika ofisi za CCM mkoani Lindi kwa kuwaomba kuwa wamoja licha ya changamoto mbalimbali za kura za maoni.