Tuesday, November 11, 2014

Matumizi ya simu za mkononi kuongeza uzalishaji na mapato ya wakulima 30,000 nchini


Matumizi ya simu za mkononi kuongeza uzalishaji na mapato ya wakulima 30,000 nchini
Maelfu ya wakulima wadogo nchini wataanza kunufaika na maisha yao kuwa murua kutokana na ubunifu wa matumizi ya Teknolojia,habari na Mawasiliano ambao umelenga kuwakwamua kiuchumi,ushirikiano wa  taasisi zenye lengo la kuwakomboa wakulima kupitia teknolojia umezinduliwa leo nchini.

Wakulima wadogo wa Tanzania watanufaika kiteknolojia kupitia huduma inayojulikana kama Kilimo Club.Kwa huduma hii wataweza kutumia huduma ya M-Pesa kutuma na kupokea fedha ikiwemo kufanya malipo wakati huo huo wataweza kutumia huduma salama na rahisi ya kuweka pesa kwenye simu ijulikanayo kama M-Pawa,vilevile wataweza kufanya mawasiliano ya simu kwa viwango vya gharama ya chini kiasi cha shilingi 400/=.

Kama ilivyo maazimio ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuwa mwaka huu wa 2014  ni "Mwaka  wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo Katika ngazi ya familia",Vodacom Tanzania inaendelea kuwawezesha na kutambua mchango wa wakulima wadogo au kilimo cha ngazi ya familia.Sekta ya kilimo inachangia asilimia 80 ya pato la Taifa ndio maana kupitia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania,Olam International,Connected Farmers Alliance na Techno Serve uliozinduliwa  rasmi nchini leo umelenga kuongeza  uzalishaji kwa wakulima.

Mbali na wakulima kunufaika na kutuma na kuweka pesa kwa njia ya  M-Pesa,wakulima wa Tanzania watanufaika kwa kupata ushauri wa kitaalamu wa kilimo kupitia ujumbe mfupi wa maneno katika simu zao, habari za mipango ya  baadaye katika sekta ya kilimo,taarifa za masoko na taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkuu wa  kitengo cha Masoko na Mawasiliano  wa Vodacom,Kelvin Twissa anasema, "Mawasiliano ya simu hutoa fursa maalum za kumwendeleza binadamu kuanzia kuwezesha upatikanaji wa taarifa za elimu na afya hadi kuongeza uzalishaji kutoka sekta ya kilimo".

Kupitia ushirikiano wa aina hii,Vodacom inaendelea kuwawezesha wakulima  wadogo kwa  kuwaongeza ujuzi ,kupata taarifa sahihi na kwa wakati mwafaka na kufanya malipo na kuweka fedha zaokwa njia rahsi na nafuu popote walipo hata sehemu za vijijini.Maisha ya wakulima yanazidi kuwa murua kutokana na ushirikiano huu.

"Kwa maana hiyo teknolojia ya matumizi ya simu za mkononi imewezesha wakulima kurahisisha shughuli zao.Ushirikiano huu utaleta mabadiliko makubwa kwa wakulima wengi hususani sehemu za vijijini ambapo watajifunza mbinu mpya za kilimo na kuongeza uzalishaji na kuweza kujipatia  vipato zaidi ya hapo awali.Vodacom inawajibika kutumia ubunifu wa kiteknolojia kuinua maisha ya wakulima wadogo nchini".Alisema Twissa.

Asilimia kubwa ya watu maskini hapa nchini  huishi katika maeneo ya vijijini,wengi wao wakitegemea kilimo kwa sehemu ya vipato au kwa vipato vyao vyote.Kwa hiyo kukua kwa sekta ya kilimo kumeonyesha uwezo wakupunguza kiwango cha umaskini mara mbili ilikinganishwa na athari ya kukua kwa sekta nyingine.Mfano halisi ni hapa Tanzania,lakini tofauti na nchi zilizoendelea wakulima wake hawana teknolojia na miondo mbinu ya hali ya juu ya kutegemea.Vodacom iko mstari wa mbele  kubadili hali hii.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa (kulia) akiongea katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya"Kilimo klabu"inayolenga kuwawezesha wakulima wadogowadogo zaidi ya 30,000 nchini (kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu. Jinsi ya kupata huduma hii piga nyota *149*01# chagua cheka vuna.