Mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Mhe. Dr. Hammis Kingwangala leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti katika jumuiya ya wazazi taifa.
Dr Kingwangala mmoja kati ya wabunge machachari katika bunge la Tanzania, amechukua fomu hiyo leo asubuhi katika ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza.
Akiongea na mtandao wa www.fpluss.blogspot.com amesema kuwa amefikia hatua baada ya kuwa na dhamira ya kweli na msukumo kutoka ndani yake.
Amesema kama mbunge kijana anaamini akipewa ridhaa ya kuongoza jumuiya hii ya wazazi ataleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na nyinginezo.
Dr Kingwangala amesema kuwa mabadiliko yapo popote duniani na kusema kuwa yeye akishirikiana na viongozi wenzake wakipewa nafasi ya kuongoza wataifanya jumuiya hiyo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi taifa iko wazi kwa sasa na Dr Kingwangala anakuwa mtu wa kwanza kuchukua fomu kugombea nafasi hii kubwa katika jumuiya hiyo.
Mtandao wa www.fpluss.blogspot.com anamtakia kila lililo jema katika kugombea nafasi hiyo.