Tuesday, November 11, 2014

WANANCHI WA MUHEZA WAHAMASIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII, ZAIDI YA KAYA 65 ZENYE WANACHAMA 390 WAHAMASIKA NA KUJIUNGA PAPO HAPO



WANANCHI WA MUHEZA WAHAMASIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII, ZAIDI YA KAYA 65 ZENYE WANACHAMA 390 WAHAMASIKA NA KUJIUNGA PAPO HAPO
  Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu kushoto akipokea risiti ya malipo mara baada ya kujiunga kuwa mwanachama wa mfuko wa afya ya Jamii (CHF) leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye Kata ya Potwe wilayani humo anayemkabidhi risiti hiyo ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe wilayani humo Dr.Samweli Mudhihiri ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasika na kujiunga papo hapo. PICHA ZOTE NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
 Picha namba moja ni  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu akisisitiza, jambo wakati uzinduzi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) kwenye kata ya Potwe wilayani Muheza uliofanyika leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasiska na kujiunga papo hapo.
 Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390
walihamasika na kujiunga papo hapo.
 MAAFISA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wahamasika kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi
kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa muda wa siku kumi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wilayani Muheza George Mhada kushoto akipokea fedha kutoka kwa Diwani wa Kata ya Potwe katikati Rashid Mdachi  anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) wilayani humo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.



MAAFISA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wahamasika kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi
kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa muda wa siku kumi.