Tuesday, November 11, 2014

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MAJAJI WA MAHAKAMA TANZANIA WAENDELEA KUFANYIKA JIJINI MWANZA



MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MAJAJI WA MAHAKAMA TANZANIA WAENDELEA KUFANYIKA JIJINI MWANZA
Mkutano Mkuu wa Majaji wa Mahakama ya Tanzania unafanyika kwa siku tatu (3) kuanzia tarehe 10 Novemba ,2014 hadi tarehe 12 Novemba,2014 katika Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza. 

Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dr.Asha Rose Migiro kwa niaba ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kauli Mbiu ya Mkutano wa Mwaka huu ni "KUJITATHMINI KAMA NJIA BORA YA KUIBORESHA MAHAKAMA".Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Mwaka huu Wah. Majaji wamepata nafasi ya kujadili mambo yafuatayo na kuyatolea Maazimio:-Taarifa kuhusu Mashauri:Ahadi,Mikakati,Mafanikio na Changamoto,Kuendesha na Kusimamia Mashauri Mahakamani:Mtazamo na Wajibu wa Jaji.

Hali ya Mashauri kwa baadhi ya Kanda za Mahakama Kuu,Hali ya Mashauri katika Mahakama ya Rufani:Mafanikio na Changamoto kwa 2012-2014.Mahakama inavyotazamwa na Wadau,Ukaguzi wa Mahakama na mnalalamika Yanayojirudi:Suluhisho la kudumu,Mfumo mpya wa usimamizi wa ubora wa kazi:Faida na Changamoto zake,Rushwa,Maadili na mienendo ya Watumishi wa Mahakama na Kesi za Uchaguzi na umuhimu wa Mahakama kujipanga mapema.
Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Dr. Asha Rose Migiro wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na Jaji Mkuu wa Mahakama wa Tanzania Mhe. Othman Chande wa kwanza Kutoka kushoto walio kaa mstari wa mbele na Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Zanzibar Mh. Makungu Watatu kutoka kushoto mstari wa mbele,wakiwa pamoja na waheshimiwa Majaji Wengine wakiwasikiliza kwa makini Wakuu wa Taasisi za haki Jinai wakitoa hotuba zao namna Taasisi zao zinavyoshirikiana na Mahakama katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo athiri utoaji haki na namna ya kutatua changamoto hizo.
Waheshimiwa Majaji wakiwasikiliza kwa Makini Wadauu Wakuu wa Taasisi za Haki Jinai (hawako pichani) wakati wa Mdahalo wa Kuibua Changamoto na Utatuzi wake Kati ya Mahakama na Mdau husika ili kuboresha utoaji wa haki.
Kamishna Jenerali wa Magereza bwana John C. Minja wa kwanza kushoto akiwa pamoja na Wadau Wengine Wakuu wa Mahakama kabla ya kuanza kutoa hotuba namna ya Jeshi la Magereza linavyo shirikiana na Mahakama katika kutatua changamoto zinazozikabili ili kuboresha utoaji wa haki.Wa pili kushoto katika picha ni Inspekta Jenerali wa Polisi bwana Ernest Mangu.Na Watatu kutoka kulia katika picha ni Naibu Mwana Sheria Mkuu wa Serkali Mhe.George Masaju.Wadau Wakuu wa Mahakama ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serkali,Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mwendesha Mashtaka (DPP),Ofisi ya Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa. (TAKUKURU), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza,Chama cha Wanasheria ((TLS).Picha zote na Mpiga picha wa Magereza Makao Makuu ya Magereza.