Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira akizungumza katika hafla fupi iliyowashirikisha baadhi ya wanasheria wa jiji la Mwanza kujadili bia za windhoek pamoja na maendeleo ya jiji hilo. Halfa hiyo ilikwenda sanjari na kila mgeni mualikwa kuchangia mada.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (katikati), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mmiliki wa The Joint Pub iliyopo Isamilo jijini Mwanza.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira (kulia), akisisitiza jambo katika hafla hiyo. Kulia ni Mmiliki wa The Joint Pub, iliyopo Isamilo jijini Mwanza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Hafla ikiendelea.
Mdau wa Windhoek jijini humo naye alikuwepo
kwenye hafla hiyo.
Wanasheria wa jiji la Mwanza wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwanasheria Mtalemwa (wa pili kushoto), akiwa na wanasheria wenzake wakifurahia Windhoek.
Kikao na hafla vikiendelea.
Dotto Mwaibale
BAADHI ya Wanasheria wa jiji la Mwanza wamesema unywaji wa bia ya Windhoek utasaidia kujenga afya za wanywaji kwani imetengenezwa kwa ubora wa juu ukilinganisha na bia zingine.
Wanasheria hao waliyabainisha hayo jijini Mwanza katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Mabibo kwa ajili ya kujua changamoto mbalimbali kutokana na soko la bia za Windhoek na Windhoek Draught na kupata maoni ya wadau wa vinywaji hivyo iliyofanyika jijini humo mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa wanasheria hao, alisema kwa muda mrefu na familia yake amekuwa akitumia Windhoek na ajawahi kupata shida yoyote kwani inachangamsha akili tofauti na bia zingine.
Bia hii haiwezi kumfanya mtumiaji ajisikie vibaya hata akinywa kiasi kikubwa na ndio maana mimi na wenzangu tunatumia bia hizi za windhoek.
"Iwapo tutajenga tabia ya kunywa bia hii hakika utafanya kazi zetu kwa uhakika hata tukiwa makazini kwani haitoi harufu mdomo na kulewesha ni vizuri tukaiunga mkono Kampuni ya Mabibo Bia " alisema Mwanasheria huyo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira aliwaomba wanamwanza kuiunga mkono Kampuni ya Mabibo Bia kwa kununua vinywaji vyake kwani mpango wa kampuni hiyo ni kujenga kiwanda ambapo kitakuza uchumi wa mkoa wa Mwanza na kutoa ajira kwa vijana.
"Hatuwezi kukamilisha ndoto zetu za kujenga kiwanda bila ya nyinyi kutuunga na kupata mrejesho mzuri wa mauzo ya bidhaa zetu tuungeni mkono kwa kununua Windhoek Lager na Windhoek Draught zenye namba ya MB66 ubavuni ambazo ndizo halali katika soko la Tanzania na si vinginevyo" alisema Fr James. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)