Saturday, April 18, 2015

MENGI Ashtushwa na Taarifa za yeye Kutaka Kuiangusha Serikali ya Kikwete



MENGI Ashtushwa na Taarifa za yeye Kutaka Kuiangusha Serikali ya Kikwete

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Dr Mengi amesema ameshtushwa na taarifa zinazomshutumu kuiangusha serikali ya Rais Kikwete.

Habari hizo zilichapishwa na gazeti la 'TAIFA IMARA' likieleza mipango ya Mengi kumwadabisha Rais JK hata baada ya kumaliza muda wake.

Mengi amesema Rais alipewa taarifa hizo na Zitto Kabwe (kwa mujibu wa gazeti hilo) na anashangaa kuona mpaka sasa Kurugenzi ya mawasiliano ikulu haijakanusha.

Mengi ameendelea kusema kuwa Rais ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote kwa hiyo kutokanushwa kwa tuhuma hizo kunampa hofu ya maisha yake kwa sasa.