Thursday, April 16, 2015

AFRIKA KUSINI WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA GHASIA ZA UBAGUZI


AFRIKA KUSINI WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA GHASIA ZA UBAGUZI
Waandamanaji wakipinga ghasia za kibaguzi dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.
Raia aliyejeruhiwa kutokana na ghasia dhidi ya raia wa kiwageni Afrika Kusini.
Maelfu ya raia katika Mji wa Mashariki wa Durban nchini Afrika Kusini wanafanya maandamano kupinga ghasia za hivi majuzi dhidi ya raia wa wageni.
Takriban watu watano wameuawa tangu wiki iliopita katika ghasia dhidi ya raia wa wageni kwa kile kilichodaiwa kuwa wageni hao wanachukua nafasi za kazi kwenye makampuni, mashirika na serikali jambo ambalo wenyeji (raia wa Afrika Kusini) wamekuwa wakikosa fursa hizo za kazi japo wako nchini mwao.
Hofu ya kusambaa kwa ghasia inaendelea kutanda jambo ambalo linaleta ukosefu wa Amani nchini humo.
Mjini Johannesburg, wamiliki wa maduka kutoka mataifa ya mbalimbali yakiwemo ya Ethiopia, Somalia na mataifa mengine ya Afrika wamefunga biashara zao wakihofia kuporwa, maduka kuchomwa moto nap engine kuuawa.
Rais wa Afrika kusini Bw. Jacob Zuma amelaani vikali ghasia hizo na anatarajiwa kulihutubia bunge la nchi hiyo baadaye hii leo.
Ikumbuke kuwa mnamo mwaka 2008 watu 62 waliuawa kufuatia ghasia za kibaguzi juu ya raia wa wageni zilizolikumba taifa hilo.
CHANZO NA BBC