Saturday, April 18, 2015

MADAHARA YA UNENE NA SHIDA YA MATIBABU



MADAHARA YA UNENE NA SHIDA YA MATIBABU
Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa
kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara
makubwa kiafya hata vifo.


Unene hupimwa kwa kutumia kipimo


kinachotambulika kitaalamu kama BMI
(yaani uzito kwa Kilogram kugawa kwa
urefu kwa mita mara mbili).


Tatizo la unene uliopindukia huweza
kusababisha mhusika kutengwa katika
jamii, kubaguliwa, kudhihakiwa hata
kunyanyapaliwa hivyo kuleta madhara
kisaikologia kwa mgonjwa.
Sababu za unene uliopindukia ni pamoja
kurithi. Mtoto aliyezaliwa na wazazi wanene,
ana asilimia 80 ya kuwa mnene, aliyezaliwa
na wazazi wembamba, ana asilimia 10 ya
kuwa mnene.

Utamaduni na ukosefu wa nidhamu katika
vyakula, pia unachangia unene uliopindukia.
Mfano; kuna ongezeko kubwa la watoto na
vijana wanene kwa sasa mijini kuliko vijijini.
Madhara yaletwayo na unene uliopindukia
ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na
kulika kwa jointi hasa za miguu, maumivu
kiunoni na katika nyonga, shinikizo la damu,
kisukari, pia kukosa usingizi kutokana na
kubanwa kwa hewa.

Mengine ni athma, kiungulia, mafuta mengi
mwilini, magonjwa ya moyo na moyo
kushidwa kufanya kazi na mawe katika
kibofu cha nyongo.
Wagonjwa hujikuta wakishindwa
kufanyakazi vyema ili kujipatia kipato, hivyo
kuwa tegemezi, kunyanyapaliwa pia huleta
matatizo ya kisaikologia kama nilivyoeleza
awali.

Matibabu ya ugonjwa huu ni pamoja na
kubadili mfumo na aina ya maisha. Hii ni
pamoja na kuwa na nidhamu katika chakula
na kufanya mazoezi. Ni wazi kwamba
wazazi na watoto wanaoishi mjini,
wanakabiliwa na tatizo hili, kutokana na
maisha ya mfumo mgando ( kula-kazi bila
jasho-kulala, au kula-kusoma-kulala).

Dawa pia zinapa


tikana na zinasaidia
kupunguza uzito walau kwa asilimia 10 kwa
mwaka, lakini hufanyakazi vyema iwapo
mfumo wa maisha utabadilishwa.
Matibabu ya muda mrefu ya tatizo hili na
ambayo husaidia mgonjwa kwa kiwango
kikubwa ni kufanyiwa upasuaji. Upasuaji
katika tumbo ndiyo tiba mwafaka kwa
unene uliopindukia.