Saturday, April 18, 2015

HALI YA UCHUMI TANZANIA SASA NI SHWARI



HALI YA UCHUMI TANZANIA SASA NI SHWARI
1
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier walipokutana katika mikutano hii ya kipupwe inayoendelea hapa Mjini Washington DC.Wengine ni ujumbe kutoka Tanzania pamoja na timu ya wataalam kutoka Benki ya Dunia.


2

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akifuatilia kwa makini maswalialiyokuwa akiulizwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier hayupo kwenye picha. Kulia ni katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw.
3
Ujumbe wa Mkutano huo kutoka pande zote mbili yaani Tanzania na Benki ya Dunia, wakimsikiliza kwa makini Mchumi mwandamizi kutoka Benki ya Dunia.
4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier kabla ya kikao kuanza rasmi.
5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akiandika kwa makini hoja na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akijibu na kueleza kwa umakini hoja na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
…………………………………………………
Wakati Tanzania ikiendelea kupambana na umaskini , Benki ya Dunia imesema kuwa," tumefurahishwa sana na mwenendo mzuri wa usimamizi wa fedha na bajeti". Hayo yalisemwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier katika mkutano ambao waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum alikuwepo.
Mambo mbalimbali yalizungumziwa katika mkutano huo ambapo suala la upatikanaji wa fedha kusaidia bajeti ya serikali lilipewakipaumbele.Maboresho katika Sekta ya umeme nalo jambo mojawapo liliopewa uzito kwani Nchi wahisani wamepata moyo wakuachia misaada baada ya kuona Serikali imeweza kulishughulikia suala zima la IPTL.
" Nchi wahisani wamekubali kuendelea kutoa misaada kwa asilimia mia, hii ni kwa sababu tu! serikali yenu imekubali kuchukua hatua dhidi ya tatizo la IPTL", alisema Philippe.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhe. Mkuya alisema kuwa, suala la kuboresha Pension nalo lilizungumziwa na chombo hiki kitasaidia serikali katika kuboresha malipo ya uzeeni (pension) na kuwezesha mashirika ya "pension" ili yaweze kuwa na uwezo wa kusaidia wastaafu. Aidha tumekubaliana kuwa watatusaidia katika suala zima la kuboresha uwazi serikalini na mazingira ya biasha Tanzania.Aliongeza Mkuya.
Jambo lingine lililochukua uzito katika majadiliano hayo ni suala la kufanya ukaguzi Bandarini. Hili limejitokeza baada ya kubainika kuwa kuna baadhi ya wafanya biashara sio waaminifu hivyo benki ya Dunia imeitaka Serikali kuangalia upya maamuzi ya mwanzo ya serikali yakuto kagua mizigo, na kusema kuwa wanasubiri majibu juu ya kubadilisha utaratibu wa mwanzo. Tanzania imekubali kukaa kwa pamoja Wizara na Fedha na TRA ili kurudisha majibu na mkakati ambao kama serikali watakuwa wamekubaliana.
"Kumekuwa na madai mengi ambayo yanadaiwa na makandarasi na wafanyabiashara wadogo, tutajitahidi kuyalipa iliyaishe lakini kwa wale wenye nyaraka halali, tunaenda kupiga marufuku kwa Afisa masuuli wote kuwa kuanzia sasa hakuna kufanya malipo yoyote kama hakuna fedha kwa ajili ya shughuli hiyo".Alisema Mkuya.
" Hii itasaidia kupunguza madeni. Ninasema haya kwani ndicho kitu tulichokubaliana kwenye mkutano huu". Alisistiza Mkuya.
Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.
Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
16/04/2015