Sunday, April 19, 2015

Ghala lenye dawa zilizopigwa marufuku na zilizokwisha muda wake wa matumizi limekamatwa Mwanza.



Ghala lenye dawa zilizopigwa marufuku na zilizokwisha muda wake wa matumizi limekamatwa Mwanza.
Maofisa zaidi ya 30 kutoka mamlaka ya chakula na dawa na baraza la Famasi Tanzania wamekamata ghala lenye dawa za serikali,zilizopigwa marufuku na zilizokwisha muda wake wa matumizi zenye thamani ya shilingi milioni 97 zikiwa zinamilikiwa na mfanyabiashara wa jijini mwanza CHARLES MBUSIRO kinyume cha sheria.
Ghala hilo lililopo eneo la ilemela jijini mwanza limekutwa likiwa limesheheni zaidi ya 120 za dawa ambazo ni sawa na tani 42 zikiwemo dawa za serikali za Kenya na Uganda, dawa za misaada, dawa zilizopigwa marufuku nchini kama vile klorokwini ya sindano, amodiaquine na gripe water -dawa nyingine zilizokutwa ndani ya ghala hilo na kwenye duka lake la dawa lililopo Natta barabara ya nyerere ni pamoja na ambazo hazijasajiliwa na TFDA na azisizoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya dawa.
 
Meneja wa usalama wa dawa wa TFDA Kissa Mwamwitwa ndiye aliyeongoza zoezi hilo liliendeshwa chini ya usimamizi mkali wa askari polisi wenye silaha za moto.
Baadhi ya maofisa wanaotekeleza operesheni hiyo, wakiwemo wanasheria kutoka TFDA na baraza la famasi tanzania pamoja na meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Florent Kyombo wakizungumzia tukio hilo wamesema taratibu za kisheria zinafanyika ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa.
 
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kahasa ilemela Richard Peter alikuwa shuhuda wakati maofisa hao wa TFDA, baraza la famasi tanzania na askari polisi walipokuwa wakitekeleza zoezi hilo kwenye ghala la dawa ambalo linasemekana bado halijasajiliwa na TFDA huku mmliki wake charles mbusiro akitoroka kwa kuruka ukuta na kutokomea kusikojulikana.