Akina mama wajawazito kote nchini wameshauriwa kutotumia dawa za kienyeji kwaajili ya kuongeza nguvu za uchungu wakati wa kujifungua hali ambayo imekuwa ikihatarisha maisha yao na kupelekea vifo kwa akinamama wengi nchini.
Akiongea katika hospital ya Kagondo mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera Thomas Ruta amewataka akinamama wajawazito kufika katika vituo vya afya mara kwa mara ili waweze kuchunguzwa afya zao na kuongeza kuwa hospital ya kagondo imekuwa na umuhimu mkubwa katika mkoa huo na taifa kwa ujumla kwani kutokana huduma bora zinazo tolewa katika hospital hiyo kumesaidia kuipunguzia mzigo hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera ambayo ilikuwa ikipokea mamia ya wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali kila kukicha.
Kwa upande wake Rais na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Jhpigo kutoka nchini marekani ambalo limekuwa likijishughuli katika kutoa huduma za afya ya uzazi kwa akina mama na watoto walio chini ya miaka mitano Leslie Mancuso ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na huduma zinazotolewa kwa akinamama na watoto katika hospital ya hospital hiyo na kwamba shirika hilo sasa lita jikita zaidi katikakuongeza vifaa tiba katika hospital hiyo ikiwemo huduma ya usafiri kwa wagonjwa kwaajili ya kunusuru vifo kwa akinamama wajawazito na watoto.
Nae muunguzi afisa muunguzi wa wodi ya akinamama wajawazito PASCHAZIA HENRY amesema pamoja na huduma zinazotolewa katika hospitali lakini bado kuna changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa wahudumu kwani kunawakati wanapokea wagonjwa wengi kupita kiasi huku katibu wa hospital hiyo JOSHUA JOSEPH akiwataka akina mama wajawazito kuepukana na imani potofu za kutumia dawa za kuongeza nguvu ya uchungu wakati wakujifungua kwani zimekuwa zipelekea vifo kwa akinamama wengi nchini badala yake wafike katika hospital pamoja na vituo mbali vya afya ili waze kupata ushauri nasaa juu ya afya ya uzazi kwa mama na watoto.