Monday, September 10, 2012

WAZIRI MEMBE ATEMBELA WILAYA MPYA YA NYASA, AANGALIA MPAKA KATI YA TZ NA MALAWI


 
Akisalimiana na mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma Daud Masiko ambaye pia ni kamanda wa takukuru mkoani Ruvuma.

 
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kushoto,akisalimiana na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe  katika uwanja wa ndege wa Songea wakati Waziri huyo alipooongoza ujumbe wa wataalamu kuangalia mpaka kati ya Tanzania na nchi jirani ya malawi katika ziwa nyasa ambapo kumekuwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili juu ya uhalali wa umiliki wake
 
  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe akisalimiana na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki kabla ya kutembelea ziwa nyasa jana kuangalia mpaka kati ya Tanzania na Malawi ambao umeleta mgogoro mkubwa juu ya nani mmiliki halali kati ya nchi hizo.
 
 Baadhi ya wananchi  katika kijiji cha Lituhi wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani kuhusiana na mzozo ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika ziwa Nyasa.
 
 Mkuu wa Brigedi ya kusini Songea Kanali John Chacha akisamiliana na Waziri wa Mambo ya nje  na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe mjini Songea.
 
 Wananchi wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani kuhusiana na mzozo ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika ziwa Nyasa.
 
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza na wazee wa mji mdogo wa Lituhi wilayani Nyasa hawapo pichani juu ya ufahamu wao kuhusu mpaka halali wa nchi mbili za malawi na Tanzania uliopo katika ziwa nyasa Katikati Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe.
 
  Mzee Gidion Ndembeka kulia akimuonesha Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernad Membe kitabu chenye mipaka halali kati ya Malawi na Tanzania iliyopo ndani ya Ziwa Nyasa.
 
Mzee aliyefahamika kwa jina moja la Ngatunga akizungumza jana wakati wa ujumbe wa wataalamu kutoka Serikalini ulipotembelea ziwa nyasa wilayani nyasa Ruvuma ili kupata ushahidi wa mmiliki halali wa ziwa nyasa ambalo limeziingiza katika mgogoro Malawi na Tanzania.
Picha na Muhidin Amri.