Mmoja wa washiriki wa Semina ya Fursa akiuliza swali kwa Meza kuu ya watoa mada kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kuku.
Mwakilishi kutoka Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Ally Mkulemba akizungumza faida mbalimbali za kujiunga na shirika hilo la NSSF,alisema kuwa vijana wanapaswa kuamka kwa sasa na kuanza kuzichangamkia fursa zitokanazo na shirika hilo,ikiwemo mikopo,bima ya Aya na mengine kwa maendeleo na ujenzi wa maisha bora
Msanii wa Bongofleva Baba Levo,ambaye pia ni mmoja wa mabalozi wa shirika hilo la NSSF,akielezea yeye na wasanii wenzake wanavyonufaika na fursa mbalimbali zipatikanazo na shirika,Baba Levo amewataka wasanii mbalimbali ambao bado hawajajiunga na shirika hilo wakiwemo na vijana mbalimbali wafanye hivyo sasa,kwani shiriki hilo linatoa fursa nyingi za kuwawezesha vijana kuwapa wigo mkubwa wa kutimiza ndoto za maisha yao
Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakimsikiliza Msanii mahiri wa Mashairi pichani,Mrisho Mpoto,alipokuwa akizungumza ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.