C H U O C H A E L I M U Y A B I A S H A R A (CBE)
"CHINI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA"
MKUTANO WA CBE ALUMNI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
KAMPASI YA MBEYA
Mkuu wa Kampasi ya Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Mbeya, Dionize A. Lwanga , Akizungumzia Mikakati na maandalizi ya awali ya Kutimiza Miaka 50 ya Chuo hicho, na Mkutano Mkubwa utakaofanyika Mwezi Octoba ambao utawakutanisha wanafunzi wote waliowahi kusoma chuo hicho ili kujadiliana mambo kadha wa kadha wakati wanajiandaa na miaka hiyo 50 na kutengeneza Alumni Association.
Afisa Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mbeya akizungumza Jambo wakati wa Majadiliano juu ya maandalizi ya Kikao cha mwezi Octoba.
Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mbeya Akizungumza jambo wakati wa mazungumzo mafupi juu ya Maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika Octoba
Majadiliano yakiwa yanaendelea
MKUU WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA ANAWATANGAZIA WAHITIMU WOTE WA MIAKA YA NYUMA NA WA SASA WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA WANAOISHI KATIKA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA WANA JUMUIA YA CBE (CBE ALUMNI) UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 4, 10, 2014 KATIKA VIWANJA VYA MBEYA HOTEL, JIJINI MBEYA, KUANZIA SAA 7.00 MCHANA. BAADA YA MKUTANO KUTAKUWA NA CHAKULA CHA PAMOJA.
MIONGONI MWA MAMBO YATAKAYOFANYIKA SIKU HIYO NI PAMOJA NA:
1) KUUNDA ALUMNI ASSOCIATION KWA NYANDA ZA JUU KUSINI
2) KUCHAGUA VIONGOZI WA ALUMNI ASSOCIATION WA KANDA
3) KUPATA TAARIFA YA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CBE
4) MADA KUHUSU MCHANGO WA CBE KATIKA KUENDELEZA BIASHARA NCHINI
5) MADA KUHUSU CBE ILIPOTOKA, ILIPO KWA SASA NA CBE IJAYO
6) KUBADILISHANA UZOEFU NA MAWAZO (NETWORKING)
MADA HIZI ZITAWASILISHWA NA WAKUFUNZI, WAHITIMU, WANAFUNZI NA WADAU WENGINE WA CBE.
TAFADHALI, UPATAPO TAARIFA HII MJULISHE NA MWENZIO.
PAMOJA TUNAWEZA
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA MKUU WA KAMPASI YA MBEYA
BARUA PEPE: dir.mbeya@cbe.ac.tz
Simu :025- 2500571
:0654- 878704, 0717 -288874, 0655- 080858