Thursday, June 26, 2014

BALOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA RASILIMALIWATU SERIKALINI

 
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

 Kaimu Mkuu Mkoa wa Dodoma Bi Fatma Salum Ally (katikati) akiwakaribisha wageni waalikwa wa mkutanomkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mkoani Dodoma, kabla ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) kufungua mkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu .
 Katibu Mkuu Ofisi Rais, Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi (katikati) akimkaribisha mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala.
 
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue  (haypo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.