Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB)uliyofanyika jijini Arusha
Mkuu wa Mkoa Arusha Magessa Mulongo akiongea katika uzinduzi huo
HALMASHAURI mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Aidha kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha miradi hiyo ikiwemo ya wananchi kukataa kulipwa fidia kwa taratibu za sheria za nchi ili kutoa maeneo ya kuchimbwa changarawe, kokoto na kuchota maji.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale wakati akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) uliofanyika katika ukumbi wa naura springs mjini hapa.
Alisema kuwa,kumekuwepo na changamoto kubwa sana zinazosababishwa na wananchi na baadhi za halmashauri katika utekelezaji wa miradi hiyo hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo yaliyowekwa.