Sunday, September 23, 2012

WAKRISTO WAKUMBUSHWA KUZIFAHAMU NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU.



 Mchungaji wa kanisa la EAGT Msumbiji Mtumishi wa Mungu Seth Nkomwa akihubiri kanisani hapo leo katika ibada kubwa ambayo amehubiri somo la Kuujua Uungu wa Roho Mtakatifu.
 Wakristo waiimba wimbo wa kuabudu wakati wakijiandaa kusikiliza neno la Mungu ambalo limekuwa faraja kwa wote waliofika kanisani hapo katika ibada ya leo.
 Huu ni upande wa kina mama ambao ni Jesh kubwa la Mungu wakiwa na nyuso za furaha kabisa katika ibada ya jumapili ya leo.
 Acheni watoto waje kwangu maana ufalme wa Mungu ni wao, ndivyo inavyoonekana pichani watoto wakipata flashi mbele ya kamera yetu katika kanisa la EAGT Msumbiji leo.
                                    Mwonekano wa wakristo kanisani hapo leo.
                          Hapa wakisikiliza neno la Mungu kwa umakini sanaaa.
 Ukiwa kanisani lazima uwe na Biblia yako ili uweze kufunua katika vifungo ambavyo vinahubiriwa katika ibada.
 Victor Band nayo ikiimba kwa nguvu katika ibada hiyo ambayo ilikuwa na Nguvu kubwa za Mungu ambazo Mungu alizishusha kanisani hapo leo.
 Michael Band kama wanavyoonekana hapo wakiwajibika stejini kama walivyonaswa na kamera ya mtandao wa www.fpluss.blogspot.com
 Hiyo ni moja kati ya staili ambayo jina lake halikufahamika kwa haraka ila nadhani waweza kujiua jina la staili yenyewe?
 Michael Paulo akionekana mbele ya kamera yetu akiwa na furaha ya ajabu katika ibada kanisani hapo leo.
 Fundi Mitambo Mr. Beston Nkomwa akiwajibika katika kuhakikisha mitambo inakwenda vizuri ili sauti iweze kusikika vizuri kama inavyotakiwa.
 Kwaya ya EAGT Msumbiji wakiwapa raha na faraja wakristo waliofika katika ibada ya leo katika kanisa la EAGT Msumbiji ambako waimbaji hawa maarufu kama Dawa ya Ndoa wanapatikana.
Kama kawaida yao wawapo stejini huwa hawafanyi kosa lolote ila zaidi ya kukupa faraja na bubujiko la nyimbo zenye matumaini katika maisha yako.
 Mama Kingi mmoja kati ya wakristo waandamizi kanisani hapo akisikiliza neno la leo kuhusu Mungu za Roho Mtakatifu.
Mmoja kati ya watu waliofika kanisani hapo kutoka katika Mkoa wa Geita ili waweze kufanyiwa maombi kutokana na uvimbe katika tumbo lake leo katika ibada iliyofurika Nguvu za Roho Mtakatifu.

Wakristo wote wamekumbushwa kuzifahamu nguvu za Roho Mtakatifu zinavyofanya kazi katika maisha ya Mkristo na kuujua uweza wake katika utendaji wa kila siku kwa Mtu aliye na uhitaji wake ili aweze kushinda mapito na misukosuko yote katika dunia hii yenye dhiki na adha nyingi.

Hayo yamesemwa na Mtumishi wa Mungu Mchungaji Seth Nkomwa katika ibada ya jumapili katika kanisa la EAGT Msumbiji ambalo linapatikana maeneo ya Msumbiji Nyasaka katika Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza leo.

Akihibiri mahubiri kutoka kitabu cha Mwanzo 1- 2 na 1 Wakorintho 2, 10- 16 kanisani hapo leo, Mchungaji Nkomwa amesema kuwa mkristo akijua nguvu za Roho Mtakatifu zilivyo hatasumbuka na shida, magonjwa na dhiki mbalimbali ambazo zinawapata wakristo hapa duniani maana Roho Mtakatifu yupo kuwasaidia katika mapito yote.

Amesema Elimu dunia haiwezi kumsaidia mtu au pesa wala kitu kingine zaidi ya nguvu za Roho Mtakatifu maana nguvu hizo hazishindwi kitu chochote hata kama kuna giza la namna gani nguvu za Roho Mtakatifu ni kiboko ya kila nguvu za Kipepo na Mizimu.

Pia amesema mtu wa mwilini hawezi kujua uweza wa nguvu za Roho Mtakatifu mpaka awe amekubali kuokoka na kupokea nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu maana yeye yuko mwilini na Roho Mtakatifu hakai sehemu chafu.

Aidha amesema mkristo akiwa na nguvu za Roho Mtakatifu, atamjulisha kila mbinu Shetani anayoitumia kumshambulia katika maisha yake na kuifahamu mitego ya shatani yote na jinsi ya kuepukana nayo.

Amesema kuna watu wanamkufuru Roho Mtakatifu kinyume na jinsi ilivyo na kusema kuwa Biblia inasema kuwa mtu atayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa, hivyo kuwaomba wakristo wote kuwa kumkubali Roho Mtakatifu ambaye ndiye msaidizi wa kila Mkristo.

Katika ibada hiyo iliyokuwa upako na wakristo wengi, kwaya na bendi mbalimbali kama EAGT Msumbiji, Victor Bendi, na Michael Bendi zimehudumu kanisani hapo na kuimba nyimbo zenye upako ambazo zimewabariki wote waliofika kanisani hapo.