Thursday, February 28, 2013

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA TBS




WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA TBS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof.  CUTHBERT F. MHILU, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania, TBS kuanzia tarehe 18 Februari, 2013.
Kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.  Dkt.  Abdallah Omary Kigoda (Mb), ameteua Wajumbe kumi na moja wa Bodi hiyo. Wajumbe walioteuliwa na mahali wanapotoka ni kama ifuatavyo.
S/N
JINA
TAASISI  ANAKOTOKA
01.
Bw.  Geofrey Simbeye
Mwakilishi wa TPSF
02.
Bi.  Fatma Riami Diwani
Mwakilishi wa Viwanda Vidogo na Vya kati
03.
Bw.  Michael Kamba
Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
04.
Dkt. Pamela L. Sawa
Mwakilishi wa Wizara ya Afya
05.
Bi.  Magdallena Utouh
Mwakilishi wa Tume ya Ushindani
06.
Bw. Jasson B.B Bagonza
Mwakilishi wa Wizara ya Fedha
07.
Bw. Juma Rajabu
Mwakilishi wa Umoja wa wajumbe wenye uelewa wa masuala ya Viwango
08.
Bw. Rashid A. Salum
Mwakilishi wa Umoja wa wajumbe wenye uelewa wa masuala ya Viwango, Zanzibar
09.
Prof.  Ntegua Mdoe
Mwakilishi Vyuo vya Elimu ya Juu
10.
Dkt.  Fidea L. Mgina
Mwakilishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara
11.
Bw. Leandry Kinabo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu


Uteuzi wa wajumbe hawa, unaanza mara moja.
Imetolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara
S.L.P 9503
DAR ES SALAAM.

Wednesday, February 27, 2013

Nafasi za Kazi Leo hii kama 47

  1. Head of Corporate Credit Vice President-Barclays 
  2. Head of Treasury Sales Assistant Vice President-Barclays
  3. Driver (GS-3)
  4. Freelance Sales Executives-EATV
  5. Southern Highlands Schools School Bursar   
  6. Project Manager, Resilience ,Dar es Salaam, Tanzania
  7. Project Manager, Governance , Dar es Salaam, Tanzania
  8. UNICEF Human Resources Assistant, GS-5, DHR, New York
  9. Monitoring & Evaluation and Strategic Planning profile for placements in Rwanda.....
  10. Borlaug Institute Regional Director for Sub-Saharan Africa Programs
  11. OCHA EA Humanitarian Affairs Officer - Reports (P3)
  12. Senior programme inception manager
  13. SSA for the Preparation of Adolescent and School Health Policy and Strategy
  14. Design and preparation of a life skills-based resource package targeting out ...
  15. Action Contre la Faim DEPUTY COUNTRY DIRECTOR - Ethiopia   
  16. INTERSOS Construction Expert     
  17. INTERSOS Urban Planner   
  18. UMCOR Monitoring and Evaluation Manager, International Development    
  19. UMCOR Water, Sanitation, Health & Hygiene (WASH) Technical Officer
  20. Associate Program Officer, Workplace-Tanzania     
  21. Program Officer, Family Planning and Reproductive Health , Tanzania 
  22. Junior Finance Officer in Ethiopia 
  23. External Assessment: Linking Farmers to Markets , Nsanje, Malawi
  24. Communications / PR Officer
  25. Monitoring and Research Officer 
  26. Finance and Administration Officer
  27. Resource Mobilisation Officer 
  28. Director, East African School of Aviation  
  29. Kenya Civil Aviation Authority Senior Procurement Officers
  30. Communication Manager for the International
  31. Institute or Refrigeration (IIR)
  32. Deputy Director of the International Institute of Refrigeration (IIR)
  33. Centenary Bank Call Centre Supervisor
  34. Air Uganda Flight Attendants
  35. Solutions Architect - Dar-es-Salaam
  36. Accountant - Dar-es-Salaam
  37. Regional Sales Manager (OPCO) - Dar-es-Salaam
  38. Sales Operations Manager - Dar-es-Salaam
  39. Medical Research Council Jobs Feb 2013 
  40. Manager - Smile Retail (OPCO) - Dar-es-Salaam
  41. SENIOR CIVIL ENGINEER (ROADS AND BUILDINGS) JOBS  
  42. ASSISTANT ENGINEERING OFFICER (CIVIL) JOBS
  43. Policy and Youth Intership with the United Nations Volunteers Office in New York
  44. Business Continuity Management (BCM) Specialist
  45. UNDP Specialist, Finance Solutions Architecture
  46. USAID/Tanzania Irrigation, Rural Roads And Infrastructure Specialist 
  47. Restless Development Tanzania Jobs March 2013

Tuesday, February 26, 2013

Nafasi za Kazi leo hii

  1. Buzwagi Gold Mine Reliability Engineer
  2. East African Growers Jobs March 2013
  3. BBC Media Action Project Manager, Resilience in Tanzania
  4. ETIHAD AIRWAYS General Manager IN Kenya
  5. Linguistics Assistant ,Tugen, Chonyi and Upper Pokomo
  6. IT Support Assistant
  7. Senior Researcher and Office Manager in Kenya
  8. ARC Program Officer Intern (Somalia Program)
  9. Across-Sudan Volunteer Project Administrator
  10. Agribusiness Market/Value Chain Development Specialist , South Sudan
  11. Nutrition Programme Manager , South Sudan
  12. TECHNICAL ASSISTANT GRADE IV - 1 POST- DEPARTMENT OF GEOLOGY
  13. TUTORIAL FELLOW, DEPARTMENT OF REAL ESTATE AND CONSTRUCTION MANAGEMENT-1 POST
  14. TECHNOLOGIST GRADE ABC - 1 POST- SCHOOL OF PHYSICAL SCIENCES
  15. JUNIOR TECHNOLOGIST GRADE IV, DEPARTMENT OF HUMAN ANATOMY
  16. Expressions of interest: Innovation Fund Programme in Tanzania
  17. DRIVER GRADE IV, TRANSPORT & GARAGE DEPARTMENT
  18. ICAP Tanzania Senior Research Advisor , Kagera
  19. Across-Sudan HR Manager
  20. Global Protection Cluster Internship
  21. Akilah Institute for Women Hospitality Management Instructor
  22. Akilah Institute for Women Entrepreneurship Program Director
  23. MIDIMAR JOB OPPORTUNITIES FEB 2013
  24. Rwanda National Police Jobs Feb 2013
  25. Miracle Corners Rwanda Country Director
  26. Stanbic Bank Sourcing Specialist/Procurement Officer
  27. Country Director Sinapis Group - Kenya
  28. Manager Financial Crime Risk ("FCR") Operations Standard Chartered Bank - Kenya
  29. Fairmont Hotels & Resorts Director, Operations
  30. Chief of Party / Local Capacity Building , East Africa
  31. Tangazo la Kazi Mbalimbali
  32. Microsoft Country Manager - Kenya
  33. GRANTS ACCOUNTANT - (1 POSITION)
  34. INTERNAL AUDITOR (1 POSITION)
  35. HEAD – MONITORING & EVALUATION (1 POSITION)
  36. Africa Point IT Internship

Sunday, February 24, 2013

Watoto Wa Viongozi Kusoma “Academia” Chanzo Cha Matokeo Mabovu Shule za Kata


Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama "Academia" inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano.

 "Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo" .

Mdee aliongezea kusema hii yote inachangiwa na mipango ya serikali iliyowekwa kwa kiwango kikubwa sana cha fedha kushindwa kutekelezeka au kusimamiwa ipasavyo ili yaweze kutekelezeka na kutolea mfano wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari.

(MMES II) ambao serikali ilitenga Shilingi bilioni 200 wakati huo kiwango cha ufaulu daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa 37% ikiwa na malengo kiwango kipande hadi 70% lakini ilipofika 2009 kiwango cha ufaulu kikashuka hadi 17%, 2011 kikashuka tena hadi 9% na mwaka jana kikazidi kudidimia mpaka 5%.

Mdee alisisitiza kuwa tatizo kubwa linalozikabili shule za kata ni miundombinu ya shule na maslahi ya walimu kwa kusema "Kinachojitekeza sasa ni mrundikano wa frustration za walimu, wamekata tamaa kabisa kwa sababu vipato vyao ni vidogo sana, lakini pamoja na kuwa vidogo vile wanavyotakiwa kuvipata kutokana na vipato kuwa vidogo hawavipati , na zaidi wakati walimu wanasema wanadai serikali inasema hawadai".

Mheshimiwa Halima Mdee alimalizia kwa kusema anadhani ni wakati sasa kama taifa lazima serikali iamue inataka kufikisha wapi elimu kwa kuwepo bajeti inayotosheleza mahitaji na kuzingatia hali halisi ya maisha na soko, na kusisitiza uwepo wa mitaala inayoeleweka tofauti na hivi sasa ambapo waalimu wanasema wanapokea maelezo tu na kujiandalia wenyewe mitaala. Pia alisisitiza uwepo wa mgawanyo wa walimu bila upendeleo kwa kila shule tofauti na sasa ambako kuna shule hazina walimu wa kutosha na pia uwepo mamlaka ya usimamizi wa elimu yenye nguvu.

Mahojiano yote yanapatikana katika: http://www.hulkshare.com/81arza49bg5c

Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali.
Mtangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango na Mbunge wa Kawe Halima Mdee baada ya kipindi.
Fina Mango akimuuliza Halima Mdee swali wakati wa mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Makutano.

YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA,REFA AOKOLEWA NA POLISI



Kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa 'Barthez' akiwa amedaka mpira mbele ya kiungo wa Azam FC, Humphrey Mieno na nyuma yake ni kiungo mwingine wa timu hiyo, Khamis Mcha 'Vialli', huku beki wake, Kevin Yondan (kushoto) akiwa tayari kutoa msaada katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 1-0.

Wachezaji wa Yanga, kutoka kulia Haruna Niyonzima, Oscar Joshua na Athumani Iddi 'Chuji' wakijadiliana wakati mchezo uliposimama kwa muda ili Barthez atibiwe baada ya kuumia

Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast, akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Yanga, Kevin Yondan.

Niyonzima (8) aliyeshikana mikono na Hamisi Kiiza akielekea eneo la mashabiki wa Yanga kushangilia baada ya kufunga

Mabeki; David Mwantika wa Azam mbele akikabiliana na Kevin Yondan wa Yanga

John Bocco akimiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' 

Mchezaji bora wa mechi ya leo; Haruna Niyonzima akiwa ameupitia mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Azam, Seif Abdallah 

Hamisi Kiiza kushoto akigombea mpira na David Mwantika, kulia ni Chuji na Salum Abubakar 'Sure Boy'

Jerry Tegete akipiga shuti huku David Mwantika akiweka mguu

Kipa Ally Mustafa 'Barthez' akiinuka baada ya kutibiwa na Daktari, Nassor Matuzya. Mbele yake ni Yondan akimfuatilia

Simon Msuva akienda chini baada ya kupigwa kwanja na beki wa Azam

Kikosi cha Azam leo 

Kikosi cha Yanga leo

Barthez amelala chini baada ya kuumia, huku mshambuliaji wa Azam, John Bocco 'Adebayor' akizungumza na refa Hashim Abdallah


Niyonzima akimtoka Mieno

Barthez anadondoka na mpira baada ya kuudakia juu

Hamisi Kiiza akimueleza jambo beki wa Azam, Mwantika wakati kipa Mwadini Ally akiwa amelala chini baada ya kuumia. Wengine kushoto ni Didier Kvumbangu na refa Hashim Abdallah

Barthez akiwapanga mabeki wake (hawapo pichani) wakati Azam wanapga mpira wa adhabu

Kavumbangu akipasua ukuta wa Azam

Kiiza kushoto akiwatoka mabeki wa Azam

Chuji akinawa maji kupoza mishipa ya kichwa

Kocha wa Azam, Stewart Hall akitoka uwanjani kinyonge baada ya mechi

Refa Hashim Abdallah akisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya mechi 

Wachezaji wa Azam wakimzonga refa wakimtuhumu kumaliza mechi kabla ya muda

Kocha wa Yanga, Ernie Brandts wa Uholanzi akiwapungia mikono mashabiki wake baada ya mechi

Hamisi Kiiza kulia akigombea mpira na beki Joackins Atudo wa Azam

Msuva akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam

Joackins Atudo akimuondoa njianui Msuva 

Jerry Tegete akimtoka Salum Waziri wa Azam

Tegete amepiga tik tak mbele ya mabeki wa Azam

Niyonzima akiambaa na mpira mbele ya wachezaji wa Azam

Niyonzima anamtoka Mcha

Niyonzima anamtoka Mcha

Viungo bora; Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam akigombea mpira na Frank Domayo wa Yanga. Nyuma ni Chuji akiwa tayari kuingilia

Sure Boy anaambaa na mpira pembeni ya Tegete

Frank Domayo akimvisha kanzu Kipre Tchetche

Sure Boy anamtoka Kavumbangu

Sure Boy anawatoka viungo wa Yanga Domayo na Chuji kulia. Mbele ni Yondan(PICHA ZOTE NI KUTOKA BONGOSTAZ.COM

Saturday, February 23, 2013

GLORIOUS WORSHIP TEAM KUADHIMISHA MIAKA 2 J'PILI HII ATRIUMS HOTEL



Mmoja wa kiongozi wa kundi la 'Glorious Worship Team akiongea jambo na Wandishi wa habari hawapo pichani

Kundi la 'Glorious Worship Team, wakiimba nyimbo
WASANII wa kundi la nyimbo za injili nchini 'Glorious Worship Team' keshokutwa Jumapili, Februari 24 mwaka huu wataadhimisha sherehe ya kutimiza miaka miwili ya kueneza injili ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya The Atrium, iliyopo Sinza Afrika Sana. Kiingilio katika hafla hiyo ni shilingi 5,000/= na wote mnakaribishwa.

Shirika la Utangazaji nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited,wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam.



Shirika la Utangazaji nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited,wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam. Msaada huo ni sehemu ya marejesho ya faida inayoipata kwa jamii (CSR). 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana amesema Jamii inayo wajibu wa kusaidia makundi ya watoto wenye ulemavu nchini ili kuwapa faraja na wajione nao ni sehemu ya jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi moja ya mashine inayotumiwa na watoto walemavu wa macho kuandikia kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mang'enya wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi sehemu ya magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Mratibu wa Elimu Kata ya Gerezani, Seraphina Mdamu kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited walipokwenda kutoa msaada huo shuleni hapo, Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Shule .
 Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, joyce Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana kuhusu maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang'enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine wa Vita Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.
 Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya kompyuta zinazotumiwa na wanafunzi walemavu kusomea wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. 
Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana sehemu ya vitabu vya Maktaba ya watoto hao walemavu wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga.hiyo, Anna Mang'enya na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa pili kulia).


Hii ndio Miji yenye gharama kubwa zaidi duniani


 
LONDON, Uingereza
MIJI ya Sydney na Melbourne ni miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa na gharama kubwa zaidi za maisha duniani.
Miji hiyo ambayo iko nchini Australia, imeingia katika nafasi ya tano bora.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kitengo cha Kiintelijensia cha Uchumi Duniani (EIU), gharama za maisha katika miji hiyo imezidi hata miji ya Ulaya na Marekani.
Bara la Asia na Australia lina miji 11 kati ya 20 iliyotajwa kuwa na gharama za juu za maisha duniani, huku miji minane ikitoka Ulaya na mmoja ukitoka America ya Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kitengo hicho, licha ya bara la Amerika ya Kaskazini kuwa na nchi maarufu na zenye uchumi wa juu, hakuna hata mji mmoja ulioweza kuingia kwenye 20 bora.
Katika utafiti uliofanyika miaka 10 iliyopita kulikuwako na  miji sita kutoka barani Asia, 10 kutoka Ulaya na minne kutoka Marekani katika 20 bora kwenye orodha ya miji 131 yenye gharama za juu kwenye nchi 93 duniani.
Katika utafiti  uliotolewa mwaka huu, Jiji la Tokyo limeshika nafasi ya kwanza likiliweka pembeni Jiji la Zurich ambalo lilikuwa kwenye nafasi hiyo na kuporomoka hadi kufikia nafasi ya saba.
Hii ni kutokana na sera za udhibiti wa mapato ya ndani ya nchi ya Uswiz kushuka.
Mji wa Osaka nchini Japan unashikilia nafasi ya pili katika orodha hiyo.
Jon Copestake, mhariri wa jarida la EIU alisema moja kati ya mabadiliko yaliyojitokeza ilikuwa ni kupanda kwa gharama nchini Australia, kulikouweka Mji wa Sydney kushika nafasi ya tatu huku Melbourne ikishika nafasi ya tano. Mji wa Oslo wa Norway ukishika nafasi ya nne. "Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, miji ya Australia haikuweza kuingia hata kwenye hamsini bora. Sijawahi kuona upandaji huu wa ghafla," Copestake aliliambia Reuters.
"Lakini hii inatokana na kukua kwa uchumi kunakoendana na mfumuko wa bei pamoja na  kuimarika kwa Dola ya Australia dhidi ya Dola ya Marekani. Wageni wanaofika hapo huona kuna tofauti kubwa ya kimaisha huku wenyeji wakizoea maisha ya juu.
Kupanda kwa gharama barani Asia
Utafiti huo ulifanyika kwa kuangalia gharama za zaidi ya bidhaa 160 ukilenga kwenye vyakula, mavazi, huduma za nyumbani, usafiri na vitu vidogovidogo.
Copestake haikushangaza sana kwa Mji wa Tokyo kurejea kwenye miji ya inayoongoza, hii ni kutokana na kukua kwa uchumi wa Japan jambo linalosababisha kuongezeka kwa gharama za mahitaji muhimu kama vile mapango ya nyumba, mishahara na hata bei za nishati ya mafuta.
Tangu mwaka 1992 Tokyo imekuwa kwenye sita bora huku miji ya  Zurich, Paris na Oslo ikidaiwa kushika nafasi ya kwanza.
Miji mingine iliyoingia kwenye 10 bora kwa mwaka 2013 ni Singapore, Zurich, Paris,Caracas na Geneva.
Akizungumzia kuhusu nchi za Ulaya, Copestake alisema woga wa kushuka kwa uchumi wao na kuimarika kwa Euro kumechangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa gharama za maisha kwa miji ya bara hilo, huku kwa Mji wa Carcas kumetokana na kukua kwa udhibiti wa viwango vya ubadilishaji wa fedha.