Monday, July 09, 2012

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA KUPANDA MITI WA TANGA CEMENT


Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Kapt. Honest Ernest Mwanossa akipanda mti kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa upandaji miti katika eneo la kiwanda cha Tanga Cement, Pongwe, Tanga juzi. Jumla ya miti 13600 imepandwa katika mradi huo uliogharimu kiasi cha shs milioni 42.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendegu (katikati) akiwa na Ofisa Mawasiliano wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor (kushoto) na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Kapt. Honest Ernest Mwanossa (kulia) baada ya kuzindua mradi wa upandaji miti katika eneo la kiwanda cha kampuni hiyo jijini Tanga juzi. Jumla ya miti 13600 imepandwa katika mradi huo uliogharimu kiasi cha shs milioni 42.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Fedha wa kampuni ya Tanga Cement, Edgar Mlenge akipokea mwenge kutoka kwa wakimbizaji katika eneo la kiwanda chao wakati wa uzinduzi wa mradi wa upandaji miti katika eneo hilo jijini Tanga mwishoni mwa wiki. Jumla ya miti 13600 imepandwa katika mradi huo uliogharimu kiasi cha shs milioni 42.
Ofisa Utawala wa Tanga Cement, Changwa Mjella, akipokea mwenge wa uhuru ulipowasili katika eneo la kiwanda chao tayari kwa hafla ya uzinduzi wa mradi wa miti. Mikaratusi 10000 na mitiki 3600 imepandwa katika eneo hilo.