Wednesday, July 15, 2015

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI YOMBO VITUKA DAR



TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI YOMBO VITUKA DAR
 Diwani wa Kata ya Vituka, Kenny Makinda (kulia), akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Mwajuma Mikorota wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  ya kukabidhi kisima cha maji katika eneo la Nasizi, Vituka kwa Limboa, Temeke, Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (katikati),  akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Haisha Juma wakati wa hafla ya TBL,  ya kukabidhi kisima cha maji katika eneo la Nasizi, Vituka kwa Limboa, Temeke, Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Ali Limboa ambaye ni wa eneo la Limboa.
 Akina mama wakazi wa eneo la Kwa Limboa, Temeke,Dar es Salaam, wakiteka maji baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi kisima cha maji kilichojengwa na kampuni hiyo katika Nasizi, Vituka, wilayani Temeke. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika

 Mkurugenzi Mtendaji wa wa Kampuni ya Mo Resources Ltd, Onesmo Sigalla iliyojenga kisima hicho, akimuonesha Ofisa Uhusiano wa  TBL, Dorris Malulu ramani ya kisima hicho.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kushoto) na Diwani wa Kata ya Vituka, Kenny Makinda wakifungulia maji kwenye bomba wakati wa hafla ya TBL kukabidhi msaada wa kisima katika Serikali ya Mtaa wa Vituka kwa Limboa, Temeke, Dar es Salaam
 Mama mkazi wa Yombo Vituka akifurahia baada ya kuteka maji katika kisima hicho. Kushoto ni Dorris Malulu wa TBL aliyekabidhi kisima hicho.
Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Yombo Vituka, Mary Jailos akimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, kwa msaada wa ujenzi wa kisima uliotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi wa mtaa huo.