WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza nia ya kuusaka Urais kiaina ili kukwepa rungu la chama chake cha CCM.
Kauli hiyo inamaanisha kuwa Membe hatawania tena Ubunge katika jimbo lake la Mtama mkoani Lindi. Ili uwe waziri lazima uwe Mbunge wa jimbo au mbunge wa kuteuliwa, kutokana na kauli hiyo inamaana kuwa hatagiombea nafasi hizo na badala yake mpango wake wa kuwania Urais upo pale pale.
Akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Membe amesema hatorudi katika nafasi hiyo tena baada ya kumaliza nafasi yake baada ya kumaliza muda wake.
"Sitakuwa tena Waziri wa Mambo ya Nje, hata iweje. Sitakuwa na mkutano tena na nyinyi kwa vyovyote vile. Hili ni Baraza langu la Mwisho kushiriki," amesisitiza Membe.
Hata hivyo Membe hakutaka kusema kama ameamua kwa vyovyote vile hatakuwa waziri wa wizara hiyo, atakuwa nani?.
Wakati Membe ikitoa kauli hiyo, tayari kifungo cha miezi 12 alichopewa na CCM pamoja na makanda wengine sita wa chama hicho kwa madai ya kuanza kampeni za urais mapema kinyume na taratibu za chama hicho kikiwa kimemalizika.
Mbali na Membe, makada wengine sita wa CCM, waliopewa kifungo ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Stephen Wasira, January Makamba na Edward Lowassa.